IQNA

Malengo ya Israel dhidi ya Iran hayatatimia, asema Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki

15:00 - January 12, 2026
Habari ID: 3481794
IQNA – Akizungumzia machafuko yanayodaiwa kuungwa mkono na Israel katika miji ya Iran, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki alisema kuwa malengo ya utawala wa Israel ndani ya Iran hayatoweza kutimia. Hakan Fidan amesisitiza kuwa utawala wa Tel Aviv hautafanikiwa katika njama zake dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.

Katika mahojiano na kituo cha habari cha TRT siku ya Jumamosi, Fidan alisema matarajio ya Israel kuona mfumo wa Kiislamu wa Iran ukiporomoka kupitia mbinu kama hizi ni jambo lisilowezekana. Akirejea hamu ya muda mrefu ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, na utawala wake ya kutaka mabadiliko ya uongozi nchini Iran, mwanadiplomasia huyo wa juu wa Uturuki alisema kuwa jambo hilo “sasa halijifichi tena,” lakini akasisitiza kuwa walikosea katika makadirio yao kuhusu muitikio wa wananchi wa Iran.

Fidan aliongeza kuwa taifa la Iran lina ufahamu wa kisiasa uliopevuka, na kwamba watu wa Jamhuri ya Kiislamu wanajua vyema nini, vipi, na kwa kiwango gani wanapaswa kuitikia masuala yanayowakabili. Aidha, aligusia shinikizo na hatua za kupinga Iran zinazochukuliwa na Marekani na washirika wake wa Magharibi, akiwatuhumu kwa kufanya hali iwe ngumu zaidi kwa kuweka masharti yasiyo ya kimantiki kila mara Iran inapochagua njia ya mazungumzo.

Kauli ya Uturuki ilikuja baada ya mji mkuu Tehran na miji mingine kadhaa kushuhudia vurugu kali siku za Alhamisi na Ijumaa usiku, ambapo waharibifu wanaodaiwa kuungwa mkono na Israel na Marekani walichoma moto mali za umma na binafsi, na kusababisha uharibifu mkubwa.

3496031

Kishikizo: uturuki iran israel
captcha