IQNA

Rais wa Brazil avishwa skafu ya jadi ya Kipalestina (Keffiyeh)

10:01 - February 07, 2026
Habari ID: 3481899
IQNA – Katika ishara ya kimaadili na ya kidiplomasia inayoonesha mshikamano na watu wa Palestina, Rais wa Brazil Luiz Inácio Lula da Silva alivaa keffiyeh ya Kipalestina.

Hatua hiyo ya kiishara ilifanyika wakati wa hafla ya kuwasilishwa kwa hati za utambulisho za balozi mpya wa Palestina nchini Brazil, Marwan Jibril.

Tukio hilo linaakisi msimamo endelevu wa Brazil katika kuunga mkono haki za Wapalestina pamoja na kuimarisha uhusiano wa pande mbili kati ya Brasilia na Palestina.

Katika hafla hiyo rasmi, Rais wa Brazil alimvua keffiyeh aliyokuwa ameivaa mabegani mwake na kumvika balozi mpya wa Palestina shingoni, mara baada ya kukabidhiwa hati zake za uwakilishi wa kidiplomasia.

Mwezi Julai mwaka jana, Brazil iliungana na kesi ya mauaji ya halaiki (genocide) iliyowasilishwa na Afrika Kusini katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) dhidi ya utawala wa Israel, kuhusiana na vitendo vya kikatili vinavyotekelezwa katika Ukanda wa Gaza.

Rais Lula da Silva amekuwa akiilaumu hadharani Israel mara kwa mara kwa kile alichokitaja kuwa ni mauaji ya halaiki dhidi ya raia wa Gaza, na ametoa wito kwa utawala wa Kizayuni kuacha kujisitiri nyuma ya simulizi ya kujiona mhanga ili kuhalalisha mauaji ya kimfumo dhidi ya watoto na wanawake.

3496319

Kishikizo: brazil palestina
captcha