
Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la habari la IQNA, likinukuu tovuti ya Al‑Sumaria News, nchi hizo tatu, Uturuki, Singapore na Oman, zimetangaza kwa msingi wa mahesabu ya unajimu au astronomia kwamba kuonekana kwa hilali ya Ramadhani jioni ya Jumanne hakutawezekana, na kwamba uwezekano wa kuonekana kwa macho bila darubini utathibitika jioni ya Jumatano.
Uturuki, katika kubainisha miezi yote ya Hijria, hutegemea kikamilifu mahesabu ya awali ya unajimu, huku suala la uwezekano wa kuonekana kwa hilali kwa jicho au darubini maalulumu pua likijumuishwa ndani ya mahesabu hayo. Nchi hiyo hutangaza kuanza kwa mwezi mpya wa Hijria pale ambapo, kwa mujibu wa mahesabu, kuna uwezekano wa kuiona hilali kwa macho bila darubini au kwa kutumia darubini kutoka eneo lolote duniani linaloshiriki sehemu ya usiku na Uturuki.
Upeo huu wa kijiografia unajumuisha ulimwengu mzima wa Kiarabu na Kiislamu, Bahari ya Atlantiki, pamoja na sehemu kubwa ya Amerika ya Kaskazini na Kusini.
Kwa mujibu wa mahesabu ya unajimu ya Urais wa Masuala ya Kidini wa Uturuki (Diyanet), kuonekana kwa hilali jioni ya Jumanne tarehe 17 Februari hakutawezekana kutoka eneo lolote katika ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu, wala hata kutoka bara la Amerika. Kwa msingi huo, Uturuki imetangaza siku ya Alhamisi, tarehe 19 Februari, kuwa mwanzo rasmi wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Habari inayohusiana:
Vilevile, Baraza la Masuala ya Kiislamu la Singapore hutegemea mahesabu ya awali ya unajimu katika kutathmini uwezekano wa kuonekana kwa hilali ndani ya nchi hiyo. Kwa kuwa siku ya Jumanne mwezi ulizama kabla ya jua kuchwa, jambo lililofanya kuonekana kwa hilali kuwa jambo lisilowezekana, Singapore nayo imetangaza siku ya Alhamisi, tarehe 19 Februari, kuwa mwanzo wa Ramadhani.
Kwa mujibu wa taarifa hizi, nchi ambazo hadi sasa zimetangaza rasmi tarehe ya kuanza kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni Singapore, Uturuki na Oman, ambazo zote zimekubaliana kuwa Alhamisi, tarehe 19 Februari, ndiyo siku ya kwanza ya Ramadhani.
4334220