
Kwa mujibu wa ripoti, Sheikh Al‑Khalili aliandika katika ukurasa wake wa binafsi kwenye mtandao wa kijamii wa X kwamba amefurahishwa na uteuzi wa haraka wa kiongozi mpya wa Mapinduzi ya Kiislamu, na akatoa pongezi zake kufuatia tukio hilo.
Ameongeza kuwa anatumaini kuwa kiongozi huyo ataendelea kufuata njia ya baba yake katika kuunga mkono jamii ya Wapalestina, pamoja na kusimama dhidi ya Uzayuni unaozidi kudhoofika.
Sheikh Al‑Khalili pia ameomba dua akisema: Mwenyezi Mungu awahifadhi waja Wake Waislamu popote walipo katika rehema na ulinzi Wake.
Baada ya kuuawa shahidi kwa Ayatullah Sayyid Ali Khamenei katika shambulio la kigaidi la Marekani na Israel tarehe 10 Ramadhani sawa na 28 Februari, Baraza la Wataalamu la Iran tarehe 8 Machi 2026 lilimchagua Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei kuwa Kiongozi mpya wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran.