IQNA

Mufti Mkuu wa Oman atoa wito wa Umoja wa Waislamu dhidi ya Wazayuni

21:05 - May 10, 2026
Habari ID: 3482224
IQNA – Mufti Mkuu wa Oman ametoa wito kwa Waislamu kusimama kwa umoja katika kukabiliana na mashambulizi ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika ardhi za Kiislamu.

Katika ujumbe aliouchapisha kwenye mtandao wa X siku ya Jumamosi, Sheikh Ahmed Al‑Khalili alilaani mashambulizi ya Wazayuni dhidi ya Ukanda wa Gaza, Iran na maeneo mengine ya ulimwengu wa Kiislamu.

Alitoa wito kwa Waislamu wote kudumisha umoja ili kukabiliana na mashambulizi ya Israel. “Tunalaani vikali uvamizi wa kikatili wa Kizayuni dhidi ya Gaza yetu pendwa,” aliandika. Alisisitiza kuwa Waislamu wote wanapaswa kusimama katika safu moja kukabiliana na mashambulizi dhidi ya Gaza, Iran au sehemu yoyote ya ardhi ya Waislamu, kwa kuwa Umma wa Kiislamu ni umma mmoja.

21:05 - 2026/05/10

Sheikh Al‑Khalili ameongeza kuwa umoja huo unapaswa kudhihirishwa kwa kupinga uonevu na uvamizi, kusaidiana katika njia ya haki, na kuuangamiza uovu na batili.

“Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Msaidizi na Mlinzi wa waja Wake,” Sheikh Al‑Khalili aliongeza.

3497398/

Habari zinazohusiana
captcha