
Hapa chini ni sehemu ya barua hiyo:
Sisi, jamii ya wataalamu na wasomaji wa Qur’ani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, tunaandika barua hii kwa hisia za wasiwasi mkubwa na huruma kwa wasomi wa Qur’ani wa Umma wa Kiislamu, katika hali ambayo Iran ya Kiislamu imesimama mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya madhalimu na maadui wa haki duniani. Makundi ya muqawama, kuanzia Yemen hadi Gaza, na kutoka Lebanon hadi Iraq, yameungana na Iran katika kusimama dhidi ya dhulma.
Je, kosa letu ni lipi? Isipokuwa kushikamana na Qur’ani Tukufu na kukataa kunyenyekea mbele ya Mafirauni wa zama zetu?
“Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Je, mnatuchukia kwa sababu tu tumeamini kwa Mwenyezi Mungu, na kwa yale yaliyoteremshwa kwetu, na yale yaliyoteremshwa kabla? Na hakika wengi wenu ni waovu.” (Qur’ani 5:59)
Je, haifai kwa wasomi na wanaharakati wa Qur’ani Tukufu, kwa kufuata mafundisho ya neno la Mwenyezi Mungu, kuwatahadharisha wale wanaounga mkono na kushirikiana na kambi ya makafiri dhidi ya kushirikiana na maadui wa Uislamu?
Wajibu wa wale wanaojifunza na kufundisha Kitabu cha Mwenyezi Mungu wa kuinua sauti dhidi ya upotovu na kiburi cha madhalimu na mabebeu ni mkubwa zaidi kuliko wengine; kama vile Mwenyezi Mungu Mtukufu anavyowasifu “Rabbaniyyun” (waja waliomwelekea Mola wao) kwa sifa hii: “Lakini kuweni wanazuoni wa Mwenyezi Mungu, kwa sababu mlikuwa mnakifundisha Kitabu na mkawa mnakisoma.” (Qur’ani 3:79)
Leo, Qur’ani Tukufu inatuita kwenye wajibu na hatua. Ikiwa hatuna uwezo au utaalamu wa kuwepo katika uwanja mgumu wa mapambano, basi uwanja wa mapambano ya fikra na maneno unahitaji mchango wetu.
Bila shaka mnajua nani yuko upande wa haki katika mapambano haya. Tunajua pia kwamba nyoyo zenu zinaumia kwa dhulma ambayo madhalimu wachache wanawafanyia watu wa dunia.
“Na mna nini hata hampigani katika njia ya Mwenyezi Mungu na kwa ajili ya waliodhulumiwa miongoni mwa wanaume, wanawake na watoto wanaosema: ‘Mola wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhalimu, na utujaalie kutoka Kwako mlinzi, na utujaalie kutoka Kwako msaidizi.’” (Qur’ani 4:75)
Kama wataalamu wa Qur’ani na wasomi wa Umma wa Kiislamu, na kama wale wanaolijua neno lenye nuru la Mwenyezi Mungu, ni wajibu wetu kutoa wito kwa mataifa ya Kiislamu kuisimamia haki na kuifanya sauti ya Qur’ani isikike kwa wote, safari hii si kwa tilawa pekee, bali kwa vitendo na kwa kuvunja ukimya mbele ya adui wa Marekani na Kizayuni:
“…isipokuwa wale walioamini na wakatenda mema na wakamkumbuka Mwenyezi Mungu kwa wingi, na wakajitetea baada ya kudhulumiwa. Na wale waliodhulumu watajua mgeuko gani watakao geuka.” (Qur’ani 26:227)
Miongoni mwa waliotia saini barua hiyo ni pamoja na...
Abbas Salimi
Shahriar Parhizkar
Ahmad Abolqassemi
Karim Mansouri
Hashem Roghani
Mohammad Hossein Sabzali
Abbas Emam Jom’eh
Mohammad Hossein Saeedian
Mohammad Haj Abolqassem
Mohammad Javad Panahi
Hassan Rezaeian
Mahmoud Lotfiania
Ali Sayyah Gorji
Mohammad Reza Pourzargari
Qassem Razi’i
Ali Akbar Malekshahi
Mehdi Qarasheikhlou
Mansour Qasrizadeh
Hassan Rabeeian
Saleh At’harifard
Masoud Sayyah Gorji
Rahim Khaki
Hossein Rostami
Amin Pouya
Hamid Shakernejad
Hamidreza Ahmadi Vafa
Qassem Moqaddami
Jafar Fardi
Seyed Karim Mousavi
Reza Mohammadpour
Seyed Javad Hosseini
Saeed Parvizi
Vahid Nazarian
Karim Dolati
Masoud Nikdasti
Mohammad Javad Kashfi
Hamidreza Moqaddasi
Vahid Vakili
Mehdi Gholamnejad
Seyed Mostafa Hosseini
Mohammad Mehdi Bahrololum
Hamed Valizadeh
Seyed Mohammad Hosseinpour
Abbas Hashemi
Hadi Esfidani
na wengine wengi...
3496814