IQNA

Wanazuoni wa Qur’ani katika Ulimwengu wa Kiislamu walaani hujuma ya Marekani na Israel dhidi ya Iran

15:48 - April 07, 2026
Habari ID: 3482123
IQNA – Baadhi ya wanazuoni na maqari mashuhuri wa Qur’ani Tukufu kutoka sehemu mbalimbali za ulimwengu wa Kiislamu katika siku za karibuni wametangaza msimamo wao wa kulaani vikali uvamizi ulioanzishwa na Marekani pamoja na utawala wa Kizayuni dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Wanazuoni na maqari maarufu wa Qur’ani kutoka nchi mbalimbali wametuma jumbe wakilaani mashambulizi hayo ambayo yamesababisha kuuawa kwa mamia ya Wairan, akiwamo pia Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Shahidi Imam Sayyid Ali Khamenei.

Miongoni mwa waliotuma jumbe hizo ni  Sheikh Ahmed Ahmed Nuaina, Sheikh Abdel Fattah Tarouti, Sheikh  Taha Abdel Wahab, Sheikh  Ahmed Shazli, Sheikh Ahmed Abdel Wahab Tantawi, Sheikh  Abdel Nasser Harak, Yasser Abdul Basit Abdul Samad na Abd Sheikh el Karim Saleh kutoka Misri. Wengine waliotuma jumbe zao ni Sheikh Aqeel Munawwar na Sheikh Mukhlis Hanafi kutoka Indonesia, Sheikh Muhammad Ali Atfay kutoka Morocco, Sheikh Omar Boussadeh kutoka Algeria,  Sheikh Talal Mismar ,Sheikh Adel Khalil kutoka Lebanon, Sheikh Sedagdad Ali kutoka  Pakistan, Sheikh Rizwan Darwish kutoka Syria na Sheikh Ali Saffar kutoka Iraq.

Katika jumbe zao, walitoa pole na rambirambi kwa watu wa Iran na kuiombea nchi hiyo kupata ushindi dhidi ya wale waliowashambulia.

Tawala katili za Marekani na Israel zilianzisha mashambulizi makubwa ya kijeshi dhidi ya Iran bila kuchokozwa. Katika siku ya kwanza ya vita hivyo vya kulazimishwa mnamo Februari 28 sawa na 10 Ramadhani, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Imam  Khamenei pamoja na makamanda kadhaa waandamizi waliuawa shahidi. Aidha maadui hao wenye kutekeleza ugaidi wa kiserikali, katika siku hiyo hiyo, walishambulia shule ya msingi wa Shajara Tayyiba katika mji wa Minab kusini mwa Iran na kuua watoto wasiopungua 165.

Tokea siku hiyo, katika kujibu kujibu mashambulizi hayo ya kidhalimu, Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limefanya operesheni za kujibu mashambulizi, likilenga vituo vya Marekani na Israel katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu pamoja na kambi zao za kijeshi zilizo katika ardhi za baadhi ya nchi za eneo, kwa kutumia mawimbi ya makombora na ndege zisizo na rubani. Iran inalipiza kisasi kwa mujibu wa haki yake ya kimataifa ya kujilinda.

3497000

captcha