Ametuma usomaji au qiraa yake ya Aya ya 18 ya Sura Al‑Fath ili kuonyesha mshikamano na taifa la Iran. Hatua hii imekuja wakati ambapo taifa la Iran linaendelea kuonesha ustahimilivu mkubwa katika kukabiliana na kile kilichoelezwa kuwa ni uchokozi unaoendelea wa Marekani na Israel dhidi ya nchi hii ya Kiislamu.