
Katika mahojiano na IQNA, Muhammad Ali Jabin alisema kuwa kazi hiyo itakuwa “utetezi wa kitamaduni kwa ajili ya muqawama wa Kiislamu na wananchi wa Iran.”
Tangazo hilo limekuja kufuatia kipande cha video kilichotolewa hivi karibuni na qari mashuhuri wa Kuwait, Mishari Rashid al-Afasi, ambapo alijaribu kuhalalisha uvamizi wa Marekani na utawala haramu wa Israel dhidi ya Iran na kukosoa hatua za kulipiza kisasi za Iran.
Jabin amesema kazi hiyo itaonesha kuwa mhimili wa muqawama haupo tu katika uga wa siasa na mapambano ya kijeshi, bali pia katika uwanja wa sanaa ya Qur’ani, kasida na kusimama katika kutetea haki.
Amebaini kuwa usomaji wa Qur’ani na Ibtihal ni silaha ya kiroho dhidi ya usomaji usio na roho na uliopotoka, akisisitiza kuwa Qur’ani inapaswa kusomwa kwa nia ya imani, si kwa ajili ya faida za kidunia.
Ameongeza kuwa hakuna shaka kuwa maadui wa Uislamu, wakiwemo Wazayuni, na washirikina wa Marekani na Israel, wanaendeleza mashambulizi yao dhidi ya muqawama wa Kiislamu katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Lebanon, na Yemen.
Amelaani kauli za al-Afasi dhidi ya Iran, akisema hakuna nchi duniani inayosimama dhidi ya dhulma na uchokozi kama Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Jabin amesisitiza kuwa: “Sisi hapa Misri hatuna uhusiano wowote na msimamo au itikadi za qari huyo. Wamisri kwa ujumla wanakataa dhulma na uchokozi huu dhidi ya Iran."
Habari inayohusiana
Aidha amesema kuwa watu wa Misri wanawapenda Ahlul-Bayt (AS) na kwamba taifa lao limewahi kuwa vitani dhidi ya utawala wa Kizayuni wa kibeberu wa Israel.
Marekani na utawala wa Israel walizindua vita vya uchokozi dhidi ya Iran tarehe 28 Februari, ambapo mamia ya Wairani, wakiwemo raia, waliuawa shahidi. Miongoni mwa mashahidi alikuwa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei.
Vikosi vya Majeshi ya Iran vilijibu kwa mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani kwa muda wa wiki kadhaa, yakilenga ngome za kijeshi na kiuchumi za Israel na Marekani katika nchi uvamizi na Ghuba ya Uajemi, na kusababisha hasara kubwa katika zaidi ya mashambulizi 100 ndani ya siku 40.
4348425