IQNA

Uchambuzi wa Mapambano Dhidi ya Uzayuni katika Qur’ani / 11

Sharti la Ushindi wa Mwisho Dhidi ya Adui kwa Mujibu wa Qur’ani

15:39 - March 20, 2026
Habari ID: 3482076
IQNA –IQNA-Katika sehemu ya kumi na moja ya mfululizo wa maandishi ya uchambuzi wa Qur’ani kuhusu matukio ya hivi karibuni, simulizi ya vita vya Talut katika Qur’ani Tukufu inachunguzwa, na jinsi ushindi wa mwisho unavyokuja baada ya kupita kwenye mitihani ya kimungu.

Katika sehemu hii tunasoma kwamba sharti la ushindi ni kusafishwa kwa mtihani wa uongozi wa kimungu (wilayah), kuachana na mapenzi ya dunia, na kuondoa hofu ya chochote isipokuwa Mwenyezi Mungu. Kufuatia uvamizi wa Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran ulioanza tarehe 10 ya mwezi mtukufu wa Ramadhani na  kupelekea kuuawa shahidi Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, mfululizo wa uchambuzi wa mtazamo wa sasa kwa mwanga wa Qur’ani na riwaya umewasilishwa kwa wasomaji.

Katika sehemu ya kumi na moja, mada ni ushindi wakati wa vita na imani thabiti katika uongozi wa kimungu, kama ifuatavyo: Kila tukio lina angalau simulizi tatu: simulizi ya happa  duniani inayozingatia takwimu, idadi na mikakati; simulizi yenye kivuli cha kishetani inayoongeza hofu na mashaka; na simulizi ya mbinguni inayofunua safu ya kimungu na kiroho iliyo ndani ya matukio.

Qur’ani Tukufu haisimulii historia ya Bani Isra’il kama hadithi za zamani tu, bali kama kioo cha kuangalia hali ya leo. Simulizi ya Qur’ani kuhusu kukutana kwao na adui linaonyesha kuwa ushindi au kushindwa hauko katika idadi au vifaa, bali katika imani, subira na yakini juu ya nusra ya Mwenyezi Mungu.

Aya ya 246 ya Surah Al‑Baqarah inasimulia hali ya Bani Isra’il baada ya Nabii Musa (A.S.), walipokuwa katika dhiki ya uhamisho na dhuluma, walimuomba nabii wao awateulie kamanda wa vita, lakini baadaye walipitia mitihani mingi. Nabii wao alipomteua Talut (Sauli), kijana mchungaji, maskini na asiyejulikana, kuwa kiongozi wao, walipinga wakisema: “Atakuwaje kiongozi wetu ilhali hana utajiri wala cheo?” Nabii wao aliwakumbusha kwamba Mwenyezi Mungu ndiye aliyemchagua, na kwamba alikuwa na elimu pana na nguvu ya mwili inayostahili uongozi wa kijeshi: “…na amemzidishia ukunjufu wa ilimu na kiwiliwili…..” (Al‑Baqarah: 247). Mitihani iliendelea. Jeshi lilipofika kwenye mto wakiwa na kiu, Talut aliwaambia wasinywe maji isipokuwa kwa kujichotea kwa kiganja. Hapa ndipo kipimo cha utiifu kilipoanza. Akasema: “Asinywaye ni wa upande wangu” na “atakayekunywa kupita kiasi si wa upande wangu”. Wale waliokunywa kiasi kidogo kwa kiganja walikuwa katikati hawakukataliwa wala kukubalika kikamilifu.

Katika hatua inayofuata, walipokutana na jeshi la Jalut (Goliath) lililokuwa na silaha na nguvu nyingi, wengi walishikwa na hofu na kusema: “Leo hatuna uwezo wa kupambana na Jalut na jeshi lake.” Lakini kundi dogo lililokuwa na mtazamo wa mbinguni limesema: “…Makundi mangapi madogo yameshinda makundi makubwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu yu pamoja na wenye kusubiri..” (Al‑Baqarah: 249) Hatimaye, Nabii Daud, ambaye wakati huo alikuwa kijana mchungaji, alimrushia Jalut jiwe kwa kombeo na akamuangusha, na jeshi la adui likavunjika nguvu.

Simulizi hili inaonyesha kuwa kupita mtihani mmoja hakutoshi. Wengine walimkataa kiongozi kwa sababu ya umaskini wake; wengine walishindwa katika mtihani wa tamaa ya tumbo; na wengine walivunjika moyo walipokutana na adui.

Lakini wale waliokubali uongozi wa walii wa Mwenyezi Mungu, wakapita kando ya mali za watu na za umma bila tamaa, na wakadumu imara mbele ya mashambulizi na teknolojia za juu, ndio waliokuwa wanaostahili ushindi wa mwisho. Imam al‑Baqir (A.S.) anasimulia kwamba wale waliobaki waaminifu kwa Talut hadi mwisho walikuwa watu 313.

4340951

Kishikizo: uzayuni qurani tukufu
captcha