IQNA

Uchambuzi wa Mapambano Dhidi ya Uzayuni katika Qur’ani / 13

Wayahudi wanavyoibua mifarakano miongoni mwa Waislamu

21:03 - March 23, 2026
Habari ID: 3482083
IQNA – Katika muktadha wa vita vinavyoendelea ambavyo vilianza katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, upande mmoja unasimama Iran ya Kiislamu, na upande mwingine wapo Marekani, utawala wa Kizayuni, pamoja na vituo vyao vilivyoko katika nchi za Waarabu Waislamu za Asia ya Magharibi.

Je, Qur’ani Tukufu inasema nini kuhusu mgawanyo huu?

Inasimuliwa kwamba Myahudi mmoja aliposhuhudia umoja wa Waislamu katika mji wa Madina, hususan baina ya makabila mawili ya Aws na Khazraj, alipanga njama na akawatuma watu fulani kuwachochea kwa kuwakumbusha mambo ya zamani. Mtume Muhammad  (SAW) alitoa wito wa kuwataka Waislamu watulie, akawatahadharisha, na akawafahamisha juu ya hila ya adui. Ndipo zikateremshwa aya za 98–100 za Surah Aal‑Imran kuhusiana na tukio hilo.

Qur’ani Tukufu inasema: “Enyi mlio amini! Mkiwat'ii baadhi ya walio pewa Kitabu watakurudisheni kuwa makafiri baada ya Imani yenu.” (Aal‑Imran: 100).

Neno “baadhi” hapa linaashiria sehemu ya Wayahudi. Kauli “watakurudisheni nyuma muwe makafiri” inaeleza namna ambavyo Waislamu wanaweza kuingia katika hali ya ukafiri kwa sababu ya uchochezi wa Wayahudi. Inawezekana pia kwamba “ukafiri” hapa unarejea uadui na chuki za zama za Jahiliyyah; kwani imani huwa ni chanzo cha mapenzi na undugu, ilhali ukafiri huwa ni chanzo cha mgawanyiko na uhasama.

Kwa hakika, aya hii inawaonya Waislamu kwamba iwapo wataathiriwa na maneno yenye sumu ya maadui na kufuata vishawishi vyao, haitachukua muda mrefu kabla imani yao kudhoofika na kurejea katika hali ya ukafiri. Hii ni kwa sababu adui huanza kwanza kuwasha moto wa chuki baina yao, kuwageuzana dhidi ya wenzao, na kuendeleza vishawishi hivyo hadi wakajikuta wamejitenga kabisa na mafundisho ya Uislamu.

Katika aya inayofuata inasemwa: “Na vipi mkufuru hali nyinyi mnasomewa Aya za Mwenyezi Mungu na Mtume yuko kati yenu?”

Maana yake ni kwamba Mtume Muhammad (SAW) anaposoma aya za Mwenyezi Mungu kwenu, zisikilizeni kwa makini na zitafakarini. Msipozielewa, rejeeni kwa Mtume (SAW).

Kwa kuizingatia aya hii katika zama zetu, maana yake ni kwamba ili kuyakanusha mashaka na fitna wanazozieneza Wayahudi, ni lazima kushikamana na aya za Mwenyezi Mungu na kurejea katika Sunnah ya Mtume (SAW).

Hivyo basi, Waislamu duniani kote wanapaswa kuwa na utambuzi wa kina kuhusu ni upande upi wanaosimama katika mvutano uliopo kati ya Iran na utawala wa Marekani na  utawala wa Kizayuni.

3496804/

Kishikizo: uzayuni qurani
captcha