IQNA

Uchambuzi wa Mapambano Dhidi ya Uzayuni katika Qur’ani/6

Wakati nguvu ya mwanadamu vitani inapokuwa isiyo na mipaka

20:35 - March 10, 2026
Habari ID: 3482040
IQNA – Qur’ani Tukufu inabainisha kwamba kiwango cha imani ya mtu kwa Mwenyezi Mungu ndicho kinachoamua kiwango cha uwezo wake wa kutenda.

Kwa maneno mengine, Tawhidi (kumpwekesha Mwenyezi Mungu) husababisha uwezo wa mwanadamu kuongezeka kwa namna isiyo na kikomo.

Nabii Musa (Amani iwe juu yake) alipowaamrisha Bani Israil waingie katika Ardhi Takatifu, walikataa kwa hofu ya watu wenye nguvu waliokuwa wakiishi humo.

Wakasema: “Sisi hatutaingia humo kamwe mpaka wao watoke humo.” (Aya ya 22 ya Surah Al‑Ma’idah).

Hata hivyo,  Qur’ani Tukufu inawataja watu wawili waliokuwa na sifa maalumu: kwanza, walikuwa ni wachamungu waliomcha Mwenyezi Mungu peke yake na hawakumwogopa yeyote isipokuwa Yeye; pili, “Mwenyezi Mungu alikuwa amewaneemesha kwa fadhila Zake” , walikuwa wamebarikiwa kwa wilaya ya Kiungu (uangalizi na ulinzi wa Mwenyezi Mungu). Kwa sababu hiyo walikuwa na yakini kwamba wakishaingia humo, ushindi ungekuwa wa hakika.

Walisema: “Waingilieni kupitia lango; na mkishaingia humo, hakika mtakuwa washindi.” (Aya ya 23 ya Surah Al‑Ma’idah)

Aya hizi zinatufundisha kwamba kadiri imani yetu inavyokuwa imara zaidi, ndivyo nguvu tunayopewa inavyoongezeka. Tawhidi huinua nguvu ya mwanadamu mpaka kuvuka mipaka ya kawaida. Qur’ani inasema kwamba majeshi ya mbinguni na ya ardhini yote yako chini ya milki na amri ya Mwenyezi Mungu:

“Na majeshi ya mbingu na ya ardhi ni ya Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima.” (Aya ya 4 ya Surah Al‑Fath)

Ili kufahamu vyema namna mbingu na ardhi zinavyokuwa majeshi ya Mwenyezi Mungu, turejee kisa cha Firauni alipowafuatilia Bani Israil hadi baharini.

Bani Israil walipotoroka usiku na kufika pwani ya bahari, walijikuta wamezingirwa: mbele yao bahari, na nyuma yao jeshi la Firauni lililokuwa na silaha nzito. Wakati huo ikajitokeza mitazamo miwili: mtazamo wa kibinadamu wa Bani Israil waliopaza sauti wakisema: “Hakika sisi tumepatikana!” (Inna lamudrakun); na mtazamo wa kiimani wa Nabii Musa (Amani iwe juu yake) aliyesema kwa yakini:

“La hasha! Hakika Mola wangu yuko pamoja nami; ataniongoza.” (Aya ya 62 ya Surah Ash‑Shu‘ara)

Bahari ilipopasuliwa na jeshi la Firauni likaingia, yale yaliyokuwa nguvu yao yakageuka kuwa sababu ya maangamizi yao. Silaha zao za kushambulia na kujilinda , mavazi yao mazito ya chuma na vifaa walivyotegemea , vikawa sababu ya kuzama kwao, mpaka wote wakazama majini.

Aya hizi hazihimizi vita vya pupa au vya kukurupuka; bali zinahimiza kusimama imara juu ya maadili ya Kiungu, mipaka yake na majukumu yake. Na iwapo vita vitalazimishwa juu yako, uwe na yakini kamili kwamba Mwenyezi Mungu yu pamoja nawe.

3496700

captcha