IQNA

Uchambuzi wa Mapambano Dhidi ya Uzayuni katika Qur’ani / 10

Uhusiano kati ya Utakaso wa Waumini na Maangamizi ya Taratibu ya Makafiri

13:11 - March 19, 2026
Habari ID: 3482073
IQNA – Kuna uhusiano wa kina kati ya kuangamizwa kwa makafiri na kusafishwa kwa waumini; kadiri daraja ya imani inavyopanda, ndivyo kiwango cha ukafiri kinavyozidi kuwa kikali.

Yaani, waumini hujaribiwa kupitia kuwepo kwa makafiri, na kwa sababu ya ukuaji na kukomaa kwao, makafiri nao hujikuta wakikabiliana na imani imara ya waumini.

Qur’ani Tukufu, katika Aya za 140–141 za Suratul Aal ‘Imran, zinazozungumzia matukio ya Vita vya Uhud, inawasilisha mtazamo wa kimaendeleo (process perspective). Mtazamo huu hauishii katika uchambuzi wa tukio kwa wakati mmoja tu, bali unaweka misingi ya mtazamo mpana wa kimataifa na kufafanua mchakato wa hatua nne:

1.  Kutenganishwa na kupanga safu kati ya waumini na makafiri,

2.  Kuweka mifano na kuinua bendera za uongofu,

3.  Utakaso na usafishaji wa ndani wa waumini,

4.  Maangamizi ya taratibu ya makafiri.

Kwa hakika, hatua hizi hutokea kwa wakati mmoja. Yaani, wakati baadhi ya watu wanapitia kauli ya Mwenyezi Mungu: “Ili Allah awajue walioamini”, wengine wanapitia: “Na ili Allah awateue mashahidi miongoni mwenu.” Waumini wanapokuwa katika hali ya “Ili Allah awajaribu walioamini,” makafiri nao wanakuwa katika hali ya “Na ili Allah awaondoe makafiri.”

Pia kuna uhusiano kati ya maangamizi ya taratibu ya makafiri na majaribio ya waumini. Kadiri kiwango cha imani kinavyopanda, ndivyo kiwango cha ukafiri kinavyozidi; yaani, kuongezeka kwa ukafiri ni matokeo ya matendo ya waumini waliotakasika zaidi. Kwa maneno mengine, waumini hujaribiwa kupitia makafiri, na kwa sababu ya kukua kwao, makafiri huathiriwa na uwepo wa waumini. Hapo hujitokeza daraja mpya na kali zaidi ya ukafiri. Kama ilivyokuwa kwa Ibilisi alipopatwa na mtihani wa Nabii Adam (AS) na akaanguka hadi daraja la chini kabisa.

Kwa mujibu wa Allamah Tabatabaei, maangamizi ya makafiri yalianza tangu Vita vya Uhud na yakakamilika kwa ushindi wa Makka. Kama vile uchunguzi na mtihani ulivyo wa taratibu, ndivyo haki nayo inavyojitokeza kwa taratibu. Bani Israil walikuwa na historia ndefu ya ukafiri na mauaji, lakini walifikia kiwango kibaya zaidi cha ukafiri kupitia mauaji ya halaiki, kuua watoto wachanga, na kuwanyima watu chakula na maji.

Rais wa Marekani, Donald Trump, ambaye katika kipindi cha kwanza cha utawala wake alitoa amri ya kuuawa shahidi Qassem Soleimani, sasa katika kipindi chake cha pili amemuua shahidi Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu pamoja na  makamanda na wanafikra wakubwa wa Uislamu; kwa hiyo, kwa mtazamo huu, kambi hii ya makafiri wa zama hizi inakaribia kuangamia na waumini hatimaye watapata ushindi.

 3496762/

 

Kishikizo: uzayuni qurani tukufu
captcha