IQNA

Uchambuzi wa Mapambano Dhidi ya Uzayuni katika Qur’ani / 14

Kuja kwa Mwokozi Kunahitaji Ahadi Nzito

19:32 - March 24, 2026
Habari ID: 3482086
IQNA-Kama ilivyokuwa kwa Nabii Ya‘qub (A.S.) alipoweka sharti la kuchukua ahadi thabiti mbele ya Mwenyezi Mungu kabla ya kumruhusu Benyamini aondoke, vivyo hivyo kuja kwa Mwokozi aliyeahidiwa kunahitaji ahadi nzito na ya kweli kutoka kwa Umma unaomsubiri.

Wana wa Nabii Ya‘qub (A.S.) walimwambia baba yao:

Wakasema: Ewe baba yetu! Una nini hata hutuamini kwa Yusuf? Na hakika sisi ni wenye kumtakia kheri!?”

(Qur’ani, Surah Yusuf: 11)

Lakini walivunja uaminifu huo. Ndiyo maana, walipotaka kumchukua Benyamini, Nabii Ya‘qub (A.S.) akasema:

“Je, nikuaminini kwa huyu ila kama nilivyo kuaminini kwa nduguye zamani? (Yusuf)?”

(Surah Yusuf: 64)

Yaani: mlifanya nini kwa Yusuf (A.S.) hata leo mnataka nimkabidhi mwingine?

Hii ni Sunnah ya Mwenyezi Mungu inayotumika pia kwa Mawalii Wake. Tunapomuomba Mwenyezi Mungu (Subhanahu wa Ta‘ala) atujaalie kudhihiri kwa Mwokozi Aliyeahidiwa, Imam Mahdi (Mwenyezi Mungu Aharakishe Kudhihiri Kwake Kwa Faraja.), swali huibuka:

Mlifanya nini kwa Mawalii waliotangulia, akiwemo Imam Hussein (A.S.), na ni kwa kiasi gani mliwasaidia?

Nabii Ya‘qub (A.S.) aliweka sharti akisema:

Akasema: Sitampeleka nanyi mpaka mnipe ahadi kwa Mwenyezi Mungu kwamba lazima mtamrejesha kwangu, ila ikiwa mmezungukwa..”

(Surah Yusuf: 66)

Leo, ikiwa Umma wa Kiislamu unasubiri kudhihiri kwa Imam Mahdi, basi dua na madai pekee hayatoshi. Kinachohitajika ni ahadi ya kweli, yenye vitendo. Umma lazima upite mtihani wa subira, uthabiti na uaminifu.

Kama vile subira na ujasiri wa watu wa Palestina na Yemen ulivyodhihirika kwa ulimwengu, ndivyo pia imani na ujasiri wa watu wa Iran ulivyoonekana wazi katika maandamano ya Kimataifa ya Siku ya Quds mwaka huu. Walipiga nara za Allahu Akbar hata wakati makombora yaliposhuka, bila kumuogopa yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu, na wakaonyesha kuwa hawatarudi nyuma katika kulinda ahadi na maadili ya Kiislamu.

Kujitolea maelfu ya mashahidi, kuanzia wapiganaji katika uwanja wa mapambano hadi watoto wachanga wa siku chache, uliojaa sauti za kutisha za mabomu yanayoharibu nyumba, shule na miundombinu, inaweza kuhesabiwa kuwa ni ahadi za uthabiti hadi kudhihiri kwa Mwokozi aliyeahidiwa.

Na wale wananchi wa Iran wanaojitokeza kila usiku katika viwanja vya miji, wakifanya dua na kumkumbuka Mtume wa Mwenyezi Mungu, Muhammad (SAW.) na Ahlul-Bayt wake (AS), hujiuliza kwa sauti ya moyoni:

“Kwa nini nusra ya Mwenyezi Mungu haijafika?”

Lakini wakisikiliza kwa masikio ya imani, watasikia bishara hii tukufu:

“Lini nusura ya Mwenyezi Mungu itakuja? Jueni kuwa nusura ya Mwenyezi Mungu ipo karibu.”

(Surah Al-Baqarah: 214)

3496816

Kishikizo: uzayuni qurani tukufu
captcha