
Wakati wa Vita vya Khandaq, Mtume Muhammad (SAW) alipokuwa akichimba handaki pamoja na kundi kubwa la Waislamu, wanafiki walikuwa wakirudi majumbani mwao bila hata kuwajali Waislamu waliokuwapo. Ama Waislamu wa kweli walikuwa wakimuomba Mtume (SAW) ruhusa, kisha kurejea katika medani mara tu walipomaliza haja iliyowatoa.
Qur’ani Tukufu, katika Aya ya 62 ya Surah An‑Nur, inakosoa kundi la kwanza kwa kusema:
“Hakika Waumini wa kweli ni walio muamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake; na wanapo kuwa pamoja naye kwa jambo la kuwakhusu wote hawaondoki mpaka wamtake ruhusa.”
Maana ya “jambo la kuwakhusu au jambo kubwa” hapa ni kila jambo muhimu linalohitaji watu kukusanyika pamoja na kushirikiana; kwa hivyo, pale uongozi unapoona kuwa uwepo wa Waumini ni muhimu ili kulitatua jambo fulani, haifai kwa yeyote kuondoka bila ruhusa ya uongozi.
Aya inaendelea kusema:
“Kwa hakika wale wanao kuomba ruhusa, hao ndio wanao muamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na wakikuomba ruhusa kwa baadhi ya mambo yao, mruhusu umtakaye miongoni mwao, uwaombee msamaha kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemmu.”
Aya hii inaonesha kuwa imani inahusiana kwa karibu na kuheshimu ruhusa ya Walii wa Mwenyezi Mungu (kiongozi halali). Kauli “baadhi ya kazi au mambo yao” inaashiria kwamba ruhusa hiyo hutolewa kwa sababu muhimu tu.
Mtume (SAW) pia alikuwa akitoa ruhusa kwa kuzingatia hali ya jambo husika na athari ya uwepo au kutokuwepo kwa mtu. Hata kama ruhusa inatolewa, bado kuna haja ya kumuomba Mwenyezi Mungu msamaha na rehema, kwa sababu mtu ametoa kipaumbele kwa jambo lake binafsi juu ya kazi ya pamoja.
Kwa mfano, katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, uwepo mkubwa wa watu katika barabara kwa ajili ya maandamano ya kuunga mkono mfumo wa Kiislamu wakati wa vita umechukuliwa kuwa ni mfano wa “jambo kubwa la pamoja”, kwani umesaidia kushinda njama za maadui na kuwatia moyo wale walioko katika medani ya mapambano; hivyo kutokuwepo bila katika medani bila idhini ni jambo lisilokubalika.
3496958