IQNA

Uchambuzi wa Mapambano Dhidi ya Uzayuni katika Qur’ani/5

Sheria ya Mungu isiyobadilika katika Mapambano ya Kisasa ya Ahzab

21:07 - March 11, 2026
Habari ID: 3482043
IQNA – Kwa mujibu wa aya za Surah Al-Fath na Al-Ahzab katika Qur’ani Tukufu, Mwenyezi Mungu Mtukufu amekusudia kwamba kila wakati maadui wanapoanzisha uhasama, na upande wa haki ukadumu thabiti, basi kurudi nyuma na kushindwa kwa mhalifu huwa ni jambo lisilokwepeka na lisilobadilika.

Sunna hii ya Kimungu (Sheria ya Allah)  husambaratisha mbegu za kukata tamaa katika nyoyo za waumini, na badala yake hubadilisha mshtuko wa kuwapoteza viongozi wao kuwa imani yenye nguvu zaidi, na kujiweka katika hali ya kukubali kwa moyo wote mapenzi ya Mwenyezi Mungu.

Kurudi Nyuma kwa Adui: Ahadi Thabiti ya Mwenyezi Mungu katika Surah Al-Fath

Baada ya mashambulizi ya utawala wa Kizayuni na Kimarekani, na kuuawa shahidi kiongozi mwenye hekima wa Mapinduzi ya Kiislamu, tafakuri mbalimbali zimewasilishwa kufafanua hali ya sasa kwa misingi ya Qur’ani. Tafakuri ya sita ndiyo hii:

Qur’ani Tukufu inasema katika Aya ya 22 ya Surah Al-Fath:

“Na lau makafiri wangelipigana nanyi, bila shaka wangeliigeuza migongo yao (wakakimbia); kisha hawangempata mlinzi wala msaidizi.”

Aya inayofuata inaeleza:

“Hii ndiyo njia ya Mwenyezi Mungu ambayo imekwisha pitika, na hutopata kamwe katika njia ya Mwenyezi Mungu mabadiliko.”

‘Sheria ya Kimungu’ (Sunnatullah) maana yake ni hakika isiyopingika , kanuni ya kudumu na ya ulimwengu mzima. Kama ilivyosisitizwa katika aya ya pili, sheria ya Mungu haibadiliki kamwe. Hivyo, Mwenyezi Mungu anatuhakikishia: ikiwa adui atashambulia na ninyi msirudi nyuma, basi kwa mujibu wa sheria hii ya kimungu, bila shaka watalazimika kuondoka kwa fedheha. Sharia hii inatumika katika vita vyote vya kihistoria.

Kiongozi aliyeuawa kishahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu alifafanua kwamba, ikiwa sisi ndio tunaoanza mashambulizi, basi sheria hii ya kimungu haitoi ahadi ya ushindi wa lazima , msaada wa Mungu unaweza kuja, lakini ushindi kamili hauhakikishwi. Hata hivyo, pale adui anapokuwa ndiye muanzilishi wa uhasama, ndipo sheria hii ya kimungu hufanya kazi kwa utimilifu. Na usemi katika aya ni makini: haijasema kuwa adui “ameshindwa,” bali “amegeuza mgongo na kurudi nyuma.”

Mapambano ya Ahzab: Kuongezeka kwa Imani na Kunyenyekea

Wakati wa Vita vya Shirikisho (Ahzab), waumini walipoona majeshi ya adui yameungana dhidi yao, walisema:

“Hili ndilo Mwenyezi Mungu na Mtume Wake walilotuhidi, na hakika Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wamesema kweli.”

Na Qur’ani ikaendelea kusema:

“Na hili lilizidisha tu imani yao na kujinyenyekeza kwa Mungu.”

(Surah Al-Ahzab, Aya ya 22)

Kwa hiyo, katika hali kama hizo, sheria ya kimungu isiyobadilika huhakikisha kurudi nyuma kwa adui pale waumini wanaposimama imara katika haki; na utimilifu wa ahadi za Mwenyezi Mungu huzidisha kina cha imani katika nyoyo zao.

“Na hili lilizidisha tu imani yao na kujinyenyekeza (kwa Mwenyezi Mungu).”

3496712

captcha