IQNA

Uchambuzi wa Mapambano Dhidi ya Uzayuni katika Qur’ani / 16

Msaada wa Mwenyezi Mungu hufika baada ya waumini kuchukua hatua

20:29 - March 26, 2026
Habari ID: 3482093
IQNA – Aya ya 39 ya Surah Al‑Hajj katika Qur’ani Tukufu inaeleza kwamba Waislamu wanapaswa kufanya yale yaliyo ndani ya uwezo wao, kisha wasubiri nusura ya Mwenyezi Mungu.

Baada ya Mtume Mtukufu  Muhammad (SAW) kukataa ombi la baadhi ya Waislamu waliotaka kujibu uadui wa washirikina wa Makka—kwa sababu wakati huo hawakuwa wamepewa ruhusa ya kupigana—Mwenyezi Mungu akateremsha Aya ya 39 ya Surah Al‑Hajj:

Wameruhusiwa kupigana wale wanao pigwa vita kwa sababu wamedhulumiwa - na kwa yakini Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kuwapa ushindi.”

Baadhi ya wafasiri wanaiona aya hii kuwa ndiyo aya ya kwanza iliyompa Mtume Muhammad  (SAW) ruhusa yaJjihad na kupigana kwa silaha, kwa kuwa kazi ya Mtume ilikuwa na hatua kadhaa:

  1. Kulingania katika njia ya haki, kusafisha nyoyo na kukuza misingi ya imani.
  2. Kuunda na kuandaa jeshi la waumini.
  3. Kujilinda au kukabiliana na adui inapolazimu.

Katika aya iliyo tangulia, Mola Mtukufu alikuwa tayari amewaahidi waumini kwamba “Hakika Mwenyezi Mungu huwakinga walio amini. (Aya ya 38, Surah Al‑Hajj).

Kisha katika aya hii (Aya ya 39), akatoa ruhusa ya jihad; ikimaanisha kwamba Waislamu wasidhani kuwa wanaweza kukaa majumbani mwao tu na kungoja nusura ya Mwenyezi Mungu bila kuchukua hatua. Nusura ya Mola hushuka baada ya mja kusimama, kuamka na kufanya jitihada.

Mwisho wa aya unakamilishwa kwa ahadi ya ushindi:

“Na hakika Mwenyezi Mungu Ana uwezo wa kuwapa ushindi.”

Hii yafundisha kuwa Waislamu wanapaswa kutumia kila njia walizojaaliwa katika dunia hii, na wanapofikia mwisho wa uwezo wao, hapo ndipo husubiri kwa yakini nusura ya Mola wao. Hivi ndivyo Mtume wa Uislamu (SAW) alivyoendesha mapambano yake yote, kwa kusimama imara, kufanya jitihada, kisha kutawakkal, and ndiyo sababu alipewa ushindi katika kila hatua.

 

3496840

Kishikizo: uzayuni qurani tukufu
captcha