IQNA

Uchambuzi wa Mapambano Dhidi ya Uzayuni katika Qur’ani / 21

Muujiza wa kuhurumiana na umoja wa watu wa Iran

15:52 - April 06, 2026
Habari ID: 3482122
IQNA – Miongoni mwa matukio makubwa yaliyotokea kutokana na damu ya shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Imam Khamenei, ni kuibuka kwa kuhurumiana na umoja wa watu wa Iran katika kutetea utambulisho wa nchi yao, jambo ambalo linatokana na mapenzi na irada ya Mwenyezi Mungu.

Qur’ani Tukufu inaamrisha umoja chini ya mhimili wa dini (yaani Qur’ani na Ahlul‑Bayt). Mwenyezi Mungu anasema:

“Na shikamaneni nyote pamoja na Kamba ya Mwenyezi Mungu wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu juu yenu pale mlipokuwa maadui, akaziunganisha nyoyo zenu, mkawa kwa neema Yake ndugu.” (Āl‑‘Imrān: 103)

Aya hii tukufu inaonesha kuwa kuunganishwa kwa nyoyo na kupatikana kwa umoja ni jambo lililo katika uwezo wa Mwenyezi Mungu peke yake.

Aidha, Qur’ani Tukufu katika Aya ya 63 ya Suratul‑Anfāl inamwambia Mtume Muhammad (SAW) kwamba hata kama angeitumia mali yote iliyomo duniani, asingeweza kuziunganisha nyoyo zao; bali Mwenyezi Mungu ndiye aliyefanya hivyo:

“Na akaziunganisha nyoyo zao. Lau ungelitoa yote yaliyomo ardhini usingeweza kuziunganisha nyoyo zao, lakini Mwenyezi Mungu ndiye aliyewaunganisha. Hakika Yeye ni Mwenye nguvu na Mwenye hikima.” (Al‑Anfāl: 63)

Kadhalika aya tukufu isemayo:

“Na waandalieni nguvu kadiri mwezavyo ili kuwatisha maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu.” (Al‑Anfāl: 60)

inahusu kila jambo linaloimarisha uwezo wa kujilinda na nguvu ya kijeshi. Miongoni mwa vipengele muhimu vya nguvu hiyo ni umoja wa taifa na kuepuka mifarakano na mgawanyiko mbele ya maadui.

Taifa lililogawanyika, hata likiwa na jeshi lenye nguvu, hubaki na udhaifu; kwani hitilafu zao huwafanya kupoteza nguvu na uthabiti. Kama Qur’ani Tukufu inavyosema:

“Na mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, wala msigombane, msije mkakata tamaa na nguvu zenu zikatoweka.” (Al‑Anfāl: 46)

Ingawa maadui wa Iran ya Kiislamu walijaribu kueneza mifarakano na kuwasha moto wa vita ndani ya miji kwa mipango na fitna mbalimbali,  zikiwemo njama za mapinduzi ya kijeshi mwanzoni mwa mwaka — hatimaye mipango hiyo ilishindwa mbele ya mpango wa Mwenyezi Mungu. Baada ya tukio la kuuawa shahidi kwa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika ofisi yake, watu waumini waliinuka kwa mshikamano, wakachukua udhibiti wa mitaa ya miji yao, na kuvunja njama za maadui.

3496978

Kishikizo: qurani tukufu uzayuni
captcha