IQNA

Uchambuzi wa Mapambano Dhidi ya Uzayuni katika Qur’ani / 20

Tawhidi ya Matendo; Thawabu kwa wapiganaji imara

18:43 - April 05, 2026
Habari ID: 3482120
IQNA- Mwenyezi Mungu anasema katika Aya ya 7 ya Surah Muhammad ya Qur’ani Tukufu kwamba: “Enyi mlioamini! Mkimsadia Mwenyezi Mungu, Atakusaidieni na Atathibitisha nyayo zenu.”

 

Mwenyezi Mungu amewaomba wanadamu msaada, ilhali majeshi ya mbingu na ardhi yako chini ya amri Yake, naye ni Mwenye enzi na Hekima zote. Kama asemavyo tena:

“Na hakuna ushindi ila kwa upande wa Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye hikima.” (Aal Imran: 126)

Kuitwa kwa mwanadamu kutoa msaada ni kwa ajili ya kuhamasishwa na kujaribiwa, na anapofaulu katika jaribio hilo hupata thawabu. Kwa mfano, kuhusu kupelekwa kwa wapiganaji katika uwanja wa vita (kama ilivyokuwa katika matukio ya kihistoria ya wakati wa Mtume Muhammad-SAW-), Qur’ani inasema:

“Piganeni nao; Mwenyezi Mungu Atawaadhibu(maadui) kwa mikono yenu na Awadhalilishe.” (At‑Tawbah: 14)

Lakini wanapokwenda vitani na kushuhudia msaada wa Mwenyezi Mungu katika namna ya kipekee, wanafikia kiwango cha juu zaidi cha maarifa ya kiroho. Ndipo Qur’ani inatoa tafsiri ya kina zaidi:

“Nanyi hamkuwaua wao, bali ni Mwenyezi Mungu ndiye aliyeuawa.” (Al‑Anfal: 17)

Yaani haikuwa nguvu za wanadamu pekee zilizoshinda; bali Mwenyezi Mungu ndiye aliyepangilia mambo ya uwanja wa vita na kuleta ushindi.

Hivyo basi, mwanzoni, ili kuwahamasisha na kuwaweka tayari Mujahidina, Mwenyezi Mungu anasema: piganeni, kwani Yeye atakusaidieni. Hivyo wanapoitikia mwito wa haki, thawabu ya juu kabisa wanayopewa ni kufikia elimu ya Tawhidi Afa’li (Kumpwekesha Mwenyezi Mungu au Tauhidi katika matendo).

Kupata ufahamu wa Tawhidi Afa’li ndiko kilele cha malipo anayotunukiwa mpiganaji mwenye subira na ikhlasi katika wakati ule wa kihistoria. Yaani anatambua kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Mlinzi wao na Mwenye uwezo wote; hata mshale utokao katika upinde hauwi tena kwa nguvu ya mpiganaji, bali:

“Si nyinyi mliourusha (mshale), bali ni Mwenyezi Mungu ndiye aliyeurusha.” (Al‑Anfal: 17)

3496968

Kishikizo: qurani tukufu uzayuni
captcha