IQNA

Uchambuzi wa Mapambano Dhidi ya Uzayuni katika Qur’ani/2

Uchujaji na Machipuko ya Mwisho wa Nyakati

17:48 - March 07, 2026
Habari ID: 3482026
IQNA- Katika Qur’ani Tukufu tunasoma hivi: “…Lau wanngelitengana , basi kwa hakika tungaliwaadhibu wale waliokufuru miongoni mwao kwa adhabu chungu.” (Al Fath: 25)

Mtu mmoja alimwuliza Imam Ja‘far al‑Sadiq (a.s.) kwa nini, kwa mujibu wa itikadi ya Kishia, Amir al‑Mu’minin ‘Ali (AS.) hakupigana katika tukio la Saqifah. Imam (AS) akajibu kwa kurejea aya hii tukufu.

Mpokezi akauliza: Makusudio ya “kutengana kwa makafiri na waumini” ni nini? Imamu (AS) akasema: Amana za waumini zimo katika viuno vya makafiri.

Hali ni kama hivyo pia kuhusu kudhihiri kwa al‑Qa’im (AS). Maadamu amana hizi hazijatoka katika viuno vya makafiri, yeye hadhihiri. Lakini baada ya kutoka, ndipo atakapodhihiri na kuwashinda maadui.

Kwa hakika, swali la mpokezi lilikuwa hivi: lau Amir al‑Mu’minin (AS) angesimamisha bendera ya vita katika tukio la Saqifah, kwa kawaida angepambana na watu wachache tu. Lakini katika vita vilivyotokea wakati wa ukhalifa wake, alilazimika kupigana na maelfu ya watu.

Siri ya kucheleweshwa huku katika simulizi ya matukio ni kutoa fursa kwa amana za Mwenyezi Mungu zikue na kustawi; yaani watu ambao wana uwezo na kipaji cha kulelewa na kuchipuka, lakini bado hawakuwa wamepata nafasi ya kukua.

Hata Mtume Mtukufu Muhammad (SAW) katika Ushindi wa Makka hakuruhusu kulipiza kisasi kwa watu wa mji huo ili kung’oa mizizi ya baadhi ya fitina za baadaye; kwa sababu bado miongoni mwa watu wa Makka na katika vizazi vyao kulikuwapo waumini.

Hata hivyo, mchakato wa uchujaji wa kidini kwa asili yake huchukua muda. Mara nyingi pia, machipuko mapya hayatokei katika jiografia ile ile ambako kuna kuanguka au kuporomoka; yaani inawezekana kuporomoka kukawa karibu nasi, lakini machipuko yakatokea upande mwingine wa dunia.

Kama tunavyoona leo, watu wengi wenye dhamiri huru katika nchi za Magharibi wanapaza sauti zao kupinga maovu ya Israel duniani, ikiwemo mashambulizi dhidi ya watu wasio na ulinzi nchini Iran, lakini wakati huo huo kuna kundi dogo ambalo huinua bendera ya Israel, wakishangilia na kusherehekea.

3496664

Habari zinazohusiana
captcha