IQNA

Uchambuzi wa Mapambano Dhidi ya Uzayuni katika Qur’ani/7

Kigezo cha chini kabisa cha kutangaza ushindi vitani

19:37 - March 12, 2026
Habari ID: 3482050
IQNA – Kwa ajili ya kutangaza mwisho wa vita au ushindi katika mapambano dhidi ya Marekani na utawala wa Kizayuni, Qur’ani Tukufu inaweka misingi kadhaa ya uongozi na mwongozo.

Kwa mujibu wa misingi hiyo, Wali (Kiongozi aliyepewa mamlaka kwa amri ya Mwenyezi Mungu) hufanya uamuzi kulingana na hali halisi na mahitaji ya uwanja wa mapambano.

Kigezo cha chini kabisa cha kusitisha uadui kimeelezwa katika Aya ya 22 ya Suratul‑Fat’h:

“Na lau wale waliokufuru wangepigana nanyi, bila shaka wangeligeuza migongo yao wakakimbia.”

Maana yake ni kwamba ikiwa adui ndiye anayeanzisha vita, basi sheria ya Mwenyezi Mungu ni kwamba hatimaye atalazimika kurudi nyuma. Kwa hiyo, kila ushindi vitani si lazima uwe kuangamizwa kabisa kwa adui; kurudi nyuma kwa adui ndicho kiwango cha chini cha kumalizika kwa vita.

Hata hivyo, kurudi huko nyuma hakupaswi kuwa kwa heshima au kwa namna ya kishujaa, bali kuwe ni kwa sababu ya udhaifu na fedheha. Kama Qur’ani Tukufu inavyosema:

“Basi msilegee wala kutaka suluhu maana nyinyi ndio mtakao shinda...” (Aya ya 35 ya Suratu Muhammad)

Hiki ni kiwango cha chini tu cha kumaliza vita, na kinapaswa kukamilishwa kwa kuzingatia aya nyingine za Qur’ani. Kwa mfano, haiwezekani kufanya mkataba na watu wenye hiana, na ni wajibu kuchukua tahadhari ili kuzuia uvunjaji wa ahadi.

Hatua hizi zote zikitimia, adui hatakuwa na nafasi ya kujinasua. Kama Qur’ani inavyosema:

“Hawataona mlinzi wala msaidizi.”

Yaani hawatakuwa na mlinzi wa kuwatetea kikamilifu, wala mshirika wa kuwasaidia hata kwa kiasi , kama inavyoonekana katika hali ambapo mataifa mengi yamekataa kushirikiana na Marekani na utawala wa Kizayuni.

Hivyo basi, hatua za ushindi dhidi ya batili hupatikana kwa taratibu na kwa ngazi mbalimbali, na katika kila hatua lazima kuwe na lengo linalofaa. Utambuzi wa lengo hilo unategemea busara na hukumu ya Wali.

Na kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, katika hatua ya mwisho – kama Qur’ani Tukufu inavyobainisha , vyanzo vyote vya fitna vitaondolewa:

“Na wapigeni mpaka kusiwepo tena fitna, na dini iwe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu peke yake.” (Aya ya 39 ya Suratul‑Anfal)

3496725

Kishikizo: uzayuni qurani tukufu
captcha