IQNA

Kiongozi: Watu wa Iran ni washindi wa hakika katika uwanja wa mapambano

11:03 - April 10, 2026
Habari ID: 3482133
IQNA-Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Mojtaba Hosseini Khamenei, amesema kuwa watu wa Iran ni “washindi wa hakika” katika uwanja wa mapambano, akiongeza kwamba Iran haijawahi kutaka vita, lakini pia haitapuuza haki zake halali.

Ametoa kauli hiyo Alhamisi usiku katika ujumbe uliotolewa kwa mnasaba wa siku ya arubaini tangu kuuawa shahidi kwa Imam Khamenei katika vita vya uchokozi vilivyoanzishwa bila sababu dhidi ya Iran na vilivyolazimishwa na tawala za kigaidi za Israel na Marekani. Ujumbe huo pia ulijumuisha hoja muhimu zinazohusiana na Vita vya Tatu ya Kulazimishwa.

Ayatullah Hosseini Khamenei amesema kwamba Vita vya Tatu ya Kulazimishwa vimefungua ukurasa mpya wa nguvu ya taifa, na kwamba jina la Iran ya Kiislamu sasa linazidi kupanda na kupata uzito katika medani ya kimataifa. Ameongeza kuwa inaonekana wazi kwamba Iran inazidi kuwa “nguvu kubwa,” huku Uistikbari wa kimataifa ukizidi kudhoofika, jambo alilolitaja kuwa “neema ya Mwenyezi Mungu.”

Akitoa shukrani kwa wananchi kwa kujitokeza mitaani kwa nyusiku arubaini mfululizo kuunga mkono majeshi ya Iran, amewahimiza waendelee na msimamo huo, akisema kwamba uwepo wa mamilioni ya watu ni miongoni mwa nguzo za nguvu ya taifa na ni miongoni mwa mambo yenye athari katika majadiliano ya kisiasa na kidiplomasia.

Amesema: “Kwa siku na nyusiku arubaini, wafuasi na Umma wa Kiongozi Shahidi, Imam Khamenei, wamekuwa wakishuka juu ya vichwa vya Mafirauni kama mipira ya moto.”

Akizihutubu nchi jirani za kusini mwa Iran, amesema: “Mnashuhudia muujiza.” Amezihimiza zichunguze kwa makini, zielewe mambo kwa uwazi zaidi, zisimame upande ulio sawa, na zisiwe na imani kwa ahadi za mashetani.

Ameongeza: “Bado tunasubiri jibu linalofaa kutoka kwenu, enyi majirani zetu wa kusini, ili tuweze kuonyesha undugu na nia njema zetu kwenu. Hili halitawezekana isipokuwa mtakapoachana na madola ya kibeberu ambayo hayakosi fursa ya kuwadhilisha na kuwanyonya.”

Kuhusu wale walioishambulia Iran, amesema Iran bila shaka itadai fidia kamili kwa uharibifu wote uliosababishwa, pamoja na malipo ya damu kwa mashahidi na fidia kwa majeruhi wa vita.

Pia amesema kwamba Iran kwa hakika itaingiza usimamizi wa Lango Bahari la Hormuz katika hatua mpya. Kiongozi Muadhamu amesisitiza kuwa: “Hatukuwahi kutaka vita, wala hatutaki vita; lakini kwa vyovyote vile hatutaacha haki zetu halali,” na ameongeza kuwa katika suala hili Iran inaiona Safu nzima ya Muqawama kama harakati iliyoungana.

Ifuatayo ni matini kamili ya ujumbe wa Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei.

 

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

Hakika Sisi tumekupatia ushindi ulio wazi; ili Mwenyezi Mungu akusamehe makosa yako yaliyotangulia na yatakayofuata, akukamilishie neema Yake juu yako, akuongoze katika njia iliyonyooka, Na Mwenyezi Mungu akunusuru nusura yenye nguvu. (Qur’ani 48:1-3)

Sasa zimepita siku arobaini tangu mojawapo ya jinai kubwa kabisa zilizofanywa na maadui wa Uislamu na Iran, na tangu mojawapo ya majonzi mazito zaidi katika historia ya taifa hili—majonzi ya shahada yenye kuumiza moyo ya kiongozi mtukufu wa Mapinduzi ya Kiislamu, baba wa taifa la Iran, kiongozi wa Umma wa Kiislamu, na kiongozi wa wanaotafuta haki katika zama hizi: Sayyid, shahidi mkuu wa Iran na wa Mrengo wa Muqawama, Khamenei Mkuu—Mwenyezi Mungu aitukuze roho yake safi.

Kwa siku arobaini sasa, roho tukufu ya kiongozi wetu shahidi imekuwa katika ukaribu wa Mwenyezi Mungu, ikiwa mgeni katika karamu ya Mawalii, Siddiqin na Mashahidi. Wakati huohuo, au kufuatia tukio hilo, idadi kubwa ya wenzake, makamanda, wapiganaji wa Uislamu, pamoja na raia wenzao waliodhulumiwa, kuanzia watoto wachanga wa siku chache hadi wazee wa miaka mingi, nao pia wamepata fadhila hiyo kubwa.

Kwa muda wa siku na usiku arobaini sasa, Mwenyezi Mungu Mtukufu amemwita kiongozi wa umma huu kwenye miadi ya ukaribu Wake. Hata hivyo, safari hii—kinyume na yaliyotokea katika zama za Kalīmullāh (Nabii Mūsā)—wafuasi wa kiongozi huyo shahidi pamoja na umma wake waliinuka kwa ajili ya kusimamisha haki na kupambana na batili. Wamesimama imara kama milima dhidi ya Sāmiri na ndama wake, na wakashuka juu ya wavamizi na Mafirauni wa zama hizi kama lava ya moto inayowaka.

Kwa siku na usiku arobaini sasa pia, wenye kiburi ulimwenguni wamevua nyuso zao bandia za udanganyifu na uongo, na wameonyesha wazi sura zao mbaya na za kishetani, aa mauaji, dhulma, uvamizi, uongo, majivuno ya kifirauni, mauaji ya watoto, utawala wa mabavu, na ufisadi.

Lakini mkabala wa hilo, kwa siku arobaini mchana na usiku, wana wa kishujaa wa Imam Khomeini Mkuu na wa Khamenei mpendwa aliyeuawa shahidi, pamoja na wafuasi wa Uislamu halisi wa Mtume Muhammadi (SAW), wamekuwa wakihudhuria kwa juhudi na ujasiri wa kipekee katika viwanja, mitaa na ngome za mapambano. Licha ya majeraha na hasara zilizosababishwa na mashambulizi ya kinyama ya adui, wamegeuza vita vya tatu vya kulazimishwa kuwa fursa ya kuwa katika Medani ya Hamasa ya Tatu ya Ulinzi Mtakatifu.

Taifa la Iran lililo na ufahamu na lenye uangalivu limeonyesha kwamba, ingawa linaomboleza kwa huzuni kubwa ya kuachana na kiongozi wake shahidi, limefuata nyayo za warithi wa moja kwa moja wa Ashura ya Husayni, likageuza majonzi kuwa hamasa, na maombolezo kuwa mashairi ya mapambano. Haya yote yamemwacha adui aliyejizatiti kwa silaha pande zote akiwa katika mshangao na kukata tamaa, huku watu huru wa ulimwengu wakiwa hawana budi ila kutoa heshima zao na pongezi (kwa taifa la Iran).

Wakati huu, ujinga na upumbavu wa Nguvu za Kiburi cha Kimataifa (Istikbari) umepelekea kwamba Esfand 1404 (Februari/Machi 2026) iwe mwanzo wa ukurasa mpya katika kuimarika na kuinuka kwa jina la Iran na Mapinduzi ya Kiislamu.

Bendera ya Iran ya Kiislamu haijainuliwa tu ndani ya mipaka ya ardhi yetu, bali pia imepandishwa ndani kabisa ya nyoyo za watu wanaotafuta haki ulimwenguni kote.

 Sifa na stadi za Kiongozi Shahidi

Tukio hili ni fursa nzuri ya kuwasilisha utambulisho mfupi wa kiongozi huyo mtukufu. Tunazungumzia kuhusu mtu ambaye, licha ya kuwa mashuhuri sana, hakutambuliwa kwa undani kadiri alivyostahili. Wote wanajua kwamba kiongozi wetu shahidi alikuwa faqihi mwenye utambuzi wa nyakati, mujahid mwenye basira na asiyechoka, thabiti na imara kama mlima; mwanazuoni mtendaji na wa kiroho, mtu wa dhikr, tahajjud na unyenyekevu katika kuomba mbele ya Mola Mlezi, na mwenye kushikamana na kutawassal kwa dhati kwa dhati tukufu za Ma’sumīn, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao wote, akiwa na imani ya dhati katika ahadi za Mwenyezi Mungu.

Miongoni mwa sifa zake nyingine ni mapenzi yake makubwa kwa Iran na juhudi zisizokoma za kuimarisha zaidi uhuru wa Iran azizi. Pamoja na hayo, alisisitiza sana umoja wa kauli na mshikamano wa kitaifa. Maisha yake yote aliyatumia katika juhudi za kusimamisha mfumo wa Kiislamu na kuhakikisha uimara na uendelevu wake; na wakati huo huo, kwa mtazamo wake, Jamhuri ya Kiislamu bila wananchi wake haikuwa na maana.

Pamoja na kuwa na mamlaka na nguvu, alikuwa pia na kiwango kikubwa cha weledi na upole wa fikra katika mtazamo wake wa mambo. Alitoa umuhimu wa pekee kwa uwezo na vipaji vya nchi, hasa vijana. Vilevile alitilia mkazo elimu, teknolojia na maendeleo yanayopatikana kupitia njia hiyo.

Kwa familia tukufu za mashahidi, majeruhi wa vita na wapambanaji waliojitolea kwa ajili ya dini na taifa, alikuwa na heshima na thamani ya pekee. Katika nyanja mbalimbali alikuwa na tajriba nyingi na zenye thamani kubwa, zilizojikusanya mara nyingi katika kipindi cha miongo kadhaa, pamoja na sifa nyingine nyingi zinazoweza kuunda orodha ndefu sana.

Katika siku hizi, katika baadhi ya vyombo vya habari mara kwa mara huzungumziwa kuhusu kipaji chake cha sanaa, uelewa wake wa sanaa na uwezo wake wa kukuza na kuhimiza sanaa. Ingawa kipengele hiki peke yake kinaweza kumpa mtu thamani kubwa ya kipekee, na bila shaka kwa kiongozi wetu mpendwa kilikuwepo kwa maana halisi na katika kiwango cha juu, hata hivyo kikilinganishwa na vipengele vingine vya utu na sifa zake, huonekana kuwa kidogo.

Mimi binafsi nawafahamu kutoka kwake sanaa sanaa na stadi mbalimbali.

Miongoni mwa ustadi mkubwa wa kiongozi huyo, ambao mara chache hupewa uzito unaostahili, ni sanaa ya kulea na kujenga jamii kupitia uundaji wa fikra, roho na hisia za makundi makubwa ya watu na tabaka mbalimbali za kijamii.

Ustadi mwingine wake ulikuwa katika kuanzisha taasisi na miundo ya kimfumo kwa malengo maalumu; jambo ambalo hasa katika miaka ya mwanzo ya kipindi chake cha uongozi alilitekeleza kwa kuangalia mbali na kuona upeo wa siku zijazo.

Pia miongoni mwa ustadi wake ulikuwa juhudi za kuimarisha na kuzipa nguvu zaidi taasisi na miundo ya kijeshi ya nchi, jambo ambalo taifa la Iran limeona na kunufaika na matokeo yake chanya katika vita viwili vya hivi karibuni vilivyolazimishwa dhidi ya nchi hii.

Vilevile, uwezo wa ubunifu na uanzilishi katika nyanja mbalimbali—iwe za kielimu, kimkakati au za utungaji wa sera, ulikuwa miongoni mwa ustadi wake mwingine. Sehemu ya hilo inaonekana katika uandaaji wa sera kuu za mfumo wa nchi.

Pia alikuwa na uwezo wa kubuni maana kupitia uundaji wa wakati muafaka wa istilahi na miunganiko mipya ya maneno yenye ubunifu; kila mojawapo likibeba na kuzaa mkusanyiko mkubwa wa maana, na kutoka humo ikajengeka mijadala na mwelekeo wa fikra katika jamii.

Na miongoni mwa ustadi huo pia kulikuwa na kipaji kilichozaliwa kutokana na kusafishwa kwa roho yake tukufu kupitia shida, mitihani na majaribu, na kutokana na subira na uimara wake katika njia ya haki, nacho ni uwezo wa kutabiri matukio ya siku za usoni. Kama ilivyo katika kauli: “Muumini hutazama kwa nuru ya Mwenyezi Mungu.”

Orodha ya stadi zake ni ndefu na haiwezekani kurodosha yote katika muhtasari huu mfupi.

Stadi zote hizi na fadhila hizo hazikuwa na chanzo kingine isipokuwa neema na inayah maalumu za Mwenyezi Mungu, pamoja na uangalizi wa pekee wa bwana wetu na mababu zake watoharifu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao wote. Huenda ikasemekana kwamba kile kilichovuta inayah na uangalizi huu kuelekea kwake ni juhudi na Jihadi yake isiyokoma na yenye ikhlasi katika njia ya kuinua neno la haki.

Mbali na magumu ya mapambano dhidi ya mfumo wa usaliti wa utawala wa Pahlavi, alipewa pia fursa nyingine ya kipekee katika njia ya kutekeleza wajibu wake, jambo ambalo kwa kawaida watu wengi hawalijui. Ilikuwa imekadiriwa kwamba Sayyid huyo kijana, aliyekuwa na kiu kubwa ya elimu na pia hamu ya kuitia elimu hiyo katika vitendo, wakati baba yake mtukufu alipokuwa akikabiliwa na hatari ya kupoteza uwezo wa kuona, baada ya miaka mingi ya kukaa katika vikao vya wanazuoni wakubwa na walimu mashuhuri, aliacha nyuma mazingira yote ya wazi yaliyoweza kumpa maendeleo makubwa ya kielimu na mustakabali wenye matumaini huko Qum, na kwa kutegemea fadhila za Mwenyezi Mungu akajitolea kikamilifu kumhudumia baba yake.

Neema ya Mwenyezi Mungu, kufuatia kujitolea huku, ilidhihiri kwa namna hii: ghafla Sayyid Ali Khamenei, akiwa bado chini ya miaka thelathini, akaibuka kutoka Khurasan kama jua linalochomoza, na upesi akahesabiwa miongoni mwa nguzo za fikra na mapambano. Wakati huohuo, katika elimu za kawaida pia alipiga hatua za kuonekana; kiasi kwamba, katika miaka ya miongo ya sabini, taasisi ya kijasusi ya SAVAK ilimwita “Khomeini wa Khurasan.” Napenda kusisitiza kwamba mwendo huu wa kupaa, kibatini  na kidhahiri, kwa mtukufu huyo uliendelea hata katika hatua zilizofuata.

Sasa, tukitazama upande wa kujifunza kutoka kwa mienendo ya wakubwa, hasa shakhsia ya aina hii, yafaa mno tuchukue sifa ya kheri ya moyo safi baina yetu na moyo wa kuhuishiana na kusaidiana (muwāsāt) kuwa ndiyo njia yetu.

 Sifa hii, ikiambatana na mtazamo wa kutumaini rehema pana ya Mwenyezi Mungu, ndiyo tofauti kuu kati ya yule anayesimama chini ya bendera ya haki na wale wanaozunguka bendera ya batili.

Bila shaka, kufuatilia mwenendo huu kutafungua milango ya mbingu na kushusha aina mbalimbali za msaada wa Kimungu usioonekana: kuanzia kunyesha kwa mvua ya rehema, hadi kupata ushindi dhidi ya adui, na hata kupiga hatua katika nyanja za elimu na teknolojia.

Katika siku hizi, inasikika mara kwa mara kwamba makundi mbalimbali ya watu wetu wapendwa, kwa haki na kwa hisia za huzuni kubwa, wanamkumbuka huyo mtu wa kipekee wa zama zake, na taratibu, vipengele vingi zaidi vya johari inayong’aa ya utu wake mtukufu vinazidi kudhihirika.

Vilevile, azma ya kufuata mienendo mahususi ya kiongozi huyo inazidi kuenea; Kwa mfano, watu wetu wapendwa wamejifunza kutoka kwa ngumi yake iliyokunjwa wakati wa shahada yake.

Na sasa, ngumi yake iliyokunjwa imekuwa alama ya pamoja ya imani na yakini kwa wengi wao. Hivyo basi, imeonekana tena wazi kwamba athari ya shahidi ni kubwa zaidi kuliko ile ya mtu aliye hai.

Sauti yake yenye mwangwi katika kuwaita watu kwenye tauhidi, kutafuta haki, na kupambana na dhulma na ufisadi sasa inasikika kwa nguvu zaidi, na ujumbe wake unapenya ndani zaidi kuliko ilivyokuwa alipokuwa hai.

Zaidi ya hayo, tamaa ya moyoni ya shahidi huyu mwenye heshima kubwa—nayo ilikuwa ustawi na heri ya taifa hili pamoja na mataifa mengine ya Kiislamu—sasa imekaribia zaidi kutimia kuliko wakati wowote uliopita.

Ushindi wa taifa shujaa la Iran katika vita vya tatu vilivyolazimishwa

Ndugu zangu wa taifa, wanaume na wanawake, leo, hadi kufikia hatua hii ya hamasa ya Ulinzi Mtakatifu wa Tatu, kwa ujasiri kabisa inaweza kusemwa kwamba nyinyi, taifa shujaa la Iran, mmekuwa washindi wa hakika katika uwanja huu.

Leo, dalili za kuchomoza kwa Jamhuri ya Kiislamu kama nguvu kubwa zimeonekana wazi mbele ya macho ya wote, na vilevile kuingia kwa madola ya kiistikbari duniani katika mteremko wa udhaifu kumekuwa dhahiri.

Bila shaka hii ni neema ya Mwenyezi Mungu, iliyotolewa kwa taifa la Iran kwa baraka ya damu ya kiongozi wetu shahidi, pamoja na mashahidi wengine waliovaa sanda ya damu, raia wetu waliodhulumiwa, na maua yaliyokatwa ya Shule ya Shajarah Ṭayyibah ya Minab. Neema hii imekuja pia kufuatia dua na unyenyekevu wa wananchi wote mbele ya Mola Mlezi, pamoja na uwepo wao wa kujitolea katika viwanja, mitaa na misikiti, na kwa sababu ya kujitolea kwa dhati na ikhlasi, bila kudai chochote, kwa wapiganaji wa Uislamu walio tayari kujitoa mhanga katika Jeshi la Walinzi (Sepah), Jeshi la Kitaifa, vikosi vya Polisi, maafisa wa usalama wasiojulikana, na walinzi wa mipaka.

Neema hii, kama neema nyingine yoyote, inapaswa kushukuriwa ili idumu na ikue, kama ilivyosemwa: “Mkishukuru, hakika Nitakuzidishieni (Qur’ani 14:7).” Shukrani ya kivitendo kwa neema hii ni juhudi zisizokoma katika kufikia Iran yenye nguvu.

Umuhimu wa kuendelea uwepo wa wananchi katika medani

Kile ambacho katika hatua ya sasa kinaonekana kuwa cha lazima ili kufikia kauli mbiu hii na lengo la kimkakati la kiongozi shahidi, ni kuendelea kwa uwepo wa wananchi wetu wapendwa, kama ilivyokuwa katika siku zile arobaini walizozipitia. Uwepo huu ni nguzo muhimu ya hadhi na nafasi ambayo leo Iran yenye nguvu imeisimamia.

Kwa hiyo, haitakiwi kudhaniwa kwamba kwa sababu ya tangazo la kuwepo kwa mazungumzo na adui, basi uwepo wa watu mitaani hauhitajiki tena. Bali hata kama, kwa dharura fulani, itafikiriwa kwamba awamu ya kimya katika uwanja wa mapambano ya kijeshi imefika, wajibu wa wananchi wote wanaoweza kuwepo katika  medani, mitaa na misikiti unaonekana kuwa mzito zaidi kuliko hapo kabla.

Bila shaka, sauti zenu katika medani na mitaani ina athari katika matokeo ya mazungumzo; kama vile idadi ya kushangaza na inayoendelea kuongezeka ya mamilioni ya washiriki katika harakati ya “Kujitolea Mhanga kwa Ajili ya Iran” pia ni miongoni mwa mambo yenye athari katika uwanja huu.

Kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, kutokana na mchango huu na kuendelea kwake, upeo unaosubiri mbele ya taifa la Iran unaashiria kujitokeza kwa enzi yenye fahari na kung’ara, enzi iliyojaa heshima, utukufu na ustawi kwao.

Kiongozi wetu shahidi alipokabidhiwa jukumu la uongozi, mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ulikuwa kama mche mchanga uliokuwa umepata majeraha mengi kutoka kwa maadui wa Uislamu na Iran, ingawa ulikuwa umevumilia yote kwa ustahimilivu. Hata hivyo, alipoliacha jukumu la uongozi wa umma baada ya takriban miaka 37, aliacha nyuma shajarah ṭayyibah, mti mwema ambao mizizi yake imejikita imara na matawi yake yameenea, yakitoa kivuli juu ya sehemu muhimu za eneo na dunia.

Mwelekeo wa kufikia Iran yenye nguvu zaidi unapita katika njia ya umoja kati ya makundi mbalimbali ya jamii, jambo ambalo yeye alisisitiza mara kwa mara. Sehemu muhimu ya umoja huu imejitokeza katika siku hizi arobaini zilizopita: nyoyo za watu zimekaribiana, hitilafu zilizokuwa kati ya makundi yenye mitazamo tofauti zimeanza kutoweka, na wote wamekusanyika chini ya bendera ya taifa. Kila siku idadi ya mkusanyiko huu inaongezeka na pia ubora wake unaimarika.

Wengi wa wale ambao bado hawajaweza kushiriki moja kwa moja katika uwepo huo, kwa nyoyo zao wapo pamoja na wako na msimamo mmoja katika kauli na hisia na makundi yaliyo katika viwanja.

Siku hizi watu wengi wanajaribu kuwa na mtazamo wa kiustaarabu kwa kutazama upeo wa mbali wa siku zijazo, na wanajitengenezea taswira ambayo si ya kubuni tu, bali imejengwa juu ya uhalisia wa sasa na wa baadaye. Hii ni sifa ambayo hadi muda si mrefu uliopita ilionekana kwa watu wachache tu, ambao kiongozi shahidi alikuwa mstari wa mbele miongoni mwao.

Kwa sababu hiyo hasa, kila mtazamaji anaweza kuona wazi ukuaji wa haraka, karibu wa kimiujiza, wa taifa hili. Na si ajabu kwamba siku hizi, yule mwanahekima mashuhuri na faqihi mkubwa wa zama zetu anapozungumza nanyi kuhusu hadhi hii tukufu, mara kwa mara hisia humzidi nguvu, kiasi kwamba sauti yake hukwama kooni na machozi yanazuia maneno yake kuendelea.

Baadhi ya nukta kuhusu majirani wa kusini: fidia ya madhara na diyah ya mashahidi

Hapa pia nawaambia majirani wa kusini wa Iran kwamba mnashuhudia muujiza. Basi uone vizuri, uelewe kwa usahihi, na simameni katika nafasi iliyo sahihi. Chukueni tahadhari na ahadi za uongo za mashetani wanaowadanganya. Bado tunasubiri kutoka kwenu mwitikio unaofaa ili tuweze kuwaonyesha udugu na nia njema tulizonazo kwenu.

Hili haliwezi kutimia isipokuwa kwa nyinyi kujitenga na madole yenye kiburi (mabeberu) ambayo hayapotezi hata fursa moja ya kuwadharau na kuwapora.

Wote wanapaswa kujua kwamba, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, sisi hatutawaacha bila kuwawajibisha wale wavamizi waovu waliolishambulia taifa letu.

Kwa hakika tutadai fidia ya kila madhara yaliyosababishwa, malipo ya damu ya mashahidi, na diyah ya majeruhi wa vita hivi. Vilevile, kwa yakini, usimamizi wa Lango Bahari la Hormuz  utajumuishwa katika hatua mpya.

Sisi hatukutaka vita na wala hatutaki vita. Lakini kwa vyovyote vile hatutaacha haki zetu halali. Katika njia hii pia tunaangalia kwa umoja mzima Mhimili wa Muqawama (Mhimili wa Mapambano) kwa ujumla wake.

Mapendekezo kwa makundi yote ya taifa

Katika kipindi hiki, hadi tufikie yale yaliyo haki yetu, kwanza kabisa watu wote wa taifa wajitahidi kujaliana na kuzingatiana. Hii itasaidia kupunguza shinikizo linaloweza kufikia makundi mbalimbali ya jamii kutokana na upungufu ambao kwa kawaida huwa ni athari ya kila vita. Hata hivyo, upungufu huu, ambao katika upande wa pili wa mapambano wakati mwingine ni mkubwa zaidi, kwa fadhila ya juhudi za ndugu zenu wanaume na wanawake serikalini na katika taasisi nyingine, umeweza kusimamiwa kwa kiwango kikubwa.

Pili, ni muhimu kulinda masikio yetu, ambayo ni kama dirisha la akili na moyo, dhidi ya vyombo vya habari vinavyoungwa mkono na adui au vinavyoenda sambamba naye. Bila shaka vyombo havitaki mema kwa nchi na taifa la Iran, na jambo hili limethibitishwa mara nyingi. Kwa hiyo, aidha tuache kabisa kukabiliana navyo na kuvitumia, au angalau tukabiliane na yale wanayowasilisha kwa tahadhari kubwa na kwa shaka nyingi.

Tatu, taifa pendwa, ingawa baada ya kumalizika kwa muda wa maombolezo rasmi ya shahada ya kiongozi weny mtukufu mtavua mavazi ya huzuni, hata hivyo muendelee kuhifadhi ndani ya roho na mioyo yenu azma thabiti ya kulipiza kisasi kwa damu takatifu yake na ya mashahidi wote wa vita vya kulazimishwa vya pili na vya tatu, na daima mtakuwa mkisubiri na kutarajia kutimia kwa jambo hilo.

Katika hitimisho, kwa unyenyekevu namwelekea Bwana wetu, Imamu Mahdi (Mwenyezi Mungu Aharakishe Kudhihiri Kwake) kwa imani kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwa kutawassal kwa Maimamu Maasumu (rehema na amani ziwe juu yao), na kwa kufuata njia ya Kiongozi wetu Shahidi, tumesimama imara chini ya bendera yako tukikabiliana na mrengo wa ukafiri na Uistikbari (ubeberu).

Katika njia hii tumetoa mashahidi wenye thamani kutoka tabaka mbalimbali za jamii kwa ajili ya heshima na uhuru wa nchi, na kwa ajili ya kuinuliwa kwa Uislamu na Mapinduzi ya Kiislamu. Pia tumepitia hasara nyingine nyingi.

Sasa, kwa nafsi zetu zote, tunaweka matumaini yetu katika dua zako maalumu ili tupate ushindi wa wazi dhidi ya adui, iwe katika uwanja wa mazungumzo au katika medani ya mapambano. Tunaomba kwamba, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, sisi pamoja na wapinzani wetu tutaona hivi karibuni athari ya kimiujiza ya dua hizo, In shā’ Allāh.

 Was-salāmu ʿalaykum wa raḥmatullāhi wa barakātuh

Sayyid Mujtaba Hosseini Khamenei

20 Farvardin 1405

Aprili 9 2026

4345497/

captcha