“Kwa heshima na kumbukumbu ya Kiongozi marehemu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei (Mwenyezi Mungu amridhie), tunatarajia kuwa mrithi wake mtukufu (Mwenyezi Mungu amhifadhi) atapewa tawfiq na msaada wa Mwenyezi Mungu katika kulitumikia taifa kubwa la Iran, kuzuia madhara ya wenye nia ovu, na kulinda umoja pamoja na mshikamano wa kitaifa,” ulisema ujumbe huo.
Baada ya kuuawa shahidi kwa Ayatullah Sayyid Ali Khamenei katika shambulio la Marekani na Israel tarehe 10 Ramadhani sawa 28 Februari, Baraza la Wanazuoni Wataalamu la Iran tarehe 8 Machi 2026 lilimchagua Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei kuwa Kiongozi mpya.
Katika kujibu uchokozi wa Marekani na Israel, uliosababisha pia kuuawa shahidi kwa baadhi ya makamanda waandamizi wa kijeshi pamoja na mamia ya raia, Iran ilianzisha Operesheni “Ahadi ya Kweli 4”, ikitekeleza mashambulizi makubwa ya makombora na droni dhidi ya malengo ya Israel na kambi za Marekani katika eneo la Asia Magharibi au Mashariki ya Kati.
3496726