IQNA

Nchini Bangladesh

Udhaifu wa Wanafunzi wa Madrasah katika ujifunza Qur’ani waibua changamoto ya kuajiri walimu

17:50 - April 16, 2026
Habari ID: 3482143
IQNA – Waziri wa Elimu wa Bangladesh, Ehsanul Haque Milon, amesema kuwa ingawa viwango vya kufaulu katika madrasah ni vya juu, elimu sahihi ya Qur’ani bado haijaimarika vya kutosha, jambo ambalo sasa limekuwa kikwazo katika ajira ya walimu wa masomo ya dini.

Waziri aliyasema hayo siku ya Jumatano (Aprili 15) alipohutubia kikao na makatibu wa vituo vya mtihani wa SSC na mitihani mingine ya daraja sawa katika eneo la Sylhet, kilichofanyika katika Chuo cha Serikali cha Wanawake cha Sylhet.

Akasema: “Kwa sasa kuna nafasi takribani 9,000 za walimu wa masomo ya dini, lakini hatuwezi kuzijaza kwa sababu waombaji hawana elimu ya kutosha ya Qur’ani Tukufu.”

Aidha, waziri alieleza kuwa mfumo wa elimu umeporomoka kwa kiwango kikubwa. Alikumbusha mchango wa Rais Shahidi Ziaur Rahman, akisema kuwa ndani ya siku 16 tu tangu kuwa Waziri wa Elimu, aliweza kuanzisha mpango wa kulipia 50% ya mishahara ya walimu (MPO). Pia alitaja kufanya kazi na Begum Khaleda Zia, na akaeleza kuwa kama mageuzi ya elimu ya wakati huo yangelidumu kwa kipindi cha miaka 17–18 iliyopita, kuporomoka kwa kiwango cha elimu kusingalitokea.

Dkt. Milon aliongeza kuwa elimu ya maadili na dini imepungua sana katika mfumo wa sasa. Akasema kuwa serikali inataka kuanzisha elimu ya maadili (ya kidini) katika shule na vyuo ili kuziba pengo hilo na kuimarisha malezi bora ya wanafunzi, kwa mujibu wa mielekeo ya jamii.

3497111/

captcha