IQNA

Wahafidhi Qur'ani kutoka mataifa 53 ya Afrika washiriki katika Mashindano ya Qur’ani na Sunnah

14:33 - April 26, 2026
Habari ID: 3482165
IQNA – Mji mkuu wa Senegal unaandaa raundi za awali za Mashindano ya kuhifadhi Qur’ani Tukufu na Sunnah ya Mtume Muhammad (SAW).

Raundi za utangulizi za toleo la pili la mashindano hayo yanayojulikana kama 'Mashindano ya Mlinzi wa Misikiti Miwili Mitukufu la Kuhifadhi Qur’ani Tukufu na Sunnah ya Mtume (SAW)' zilianza Dakar siku ya Ijumaa.

Mashindano hayo yanafadhiliwa na Wizara ya Mambo ya Kiislamu, Da‘wah na Uongozaji ya Saudi Arabia, yakiwakutanisha washiriki 100 wanaowakilisha mataifa 53 ya Afrika.

Kupitia Ofisi ya Mshauri wa Masuala ya Dini katika Ubalozi wa Saudi Arabia nchini Senegal, na kwa ushirikiano na Mamlaka Kuu ya Awqaf, mpango huu unalenga kuhimiza hifdhi ya Qur’ani na Sunnah pamoja na kukuza maadili ya msingi ya Kiislamu kupitia ushindani wenye afya na adabu.

Kwa mujibu wa waandaaji, mashindano hayo ni miongoni mwa programu kuu za kimataifa za wizara hiyo, yakilenga kuimarisha uhusiano wa kiutamaduni na kiroho barani Afrika, na kukuza ari ya ubora na kujitolea miongoni mwa vijana wa Kiafrika katika kuhudumia Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah ya Mtume Wake (SAW).

3497228

captcha