IQNA

Mpango mpya katika Al Masjid An Nabawi waboresha ziara ya wageni

15:07 - June 01, 2026
Habari ID: 3482310
IQNA – Kwa lengo la kuizidisha safari ya kiroho ya mamilioni ya wanaouzuru Msikiti wa Mtume au Al Masjid An Nabawi huko Madina Al-Munawwara, umeanzishwa mpango wa mwongozo kwa wageni unaounganisha ukunjufu wa mapokezi na mafundisho ya dini.

Urais wa Masuala ya Kidini katika Masjid al-Haram jijini Makka na Al Masjid An Nabawi  umezindua mpango huo wa kuwakaribisha na kuwapokea wageni wa Al Masjid An Nabawi , huku ukiwapatia mwongozo wa kidini na maelekezo yatakayozidi kunufaisha safari yao ya kiroho.

Mpango huo unakusudia kuinua uelewa wa dini miongoni mwa wageni na kuwajulisha hukmu, fadhila na adabu zinazohusiana na ziara ya Msikiti wa Mtume, kupitia programu mbalimbali za uongofu na maudhui ya kielimu ya aina tofauti.

Vilevile, mpango huo unajumuisha ugawaji wa vifurushi vya zawadi zenye maelezo na nyenzo za mwongozo katika lugha mbalimbali, kwa kusudi la kuongeza maarifa ya dini kwa wageni na kuimarisha ujumbe wa uelimishaji na uhamasishaji unaoendelezwa na urais huo.

3497672

Habari zinazohusiana
Kishikizo: al masjid an nabawi
captcha