
Rais wa Masuala ya Kidini katika Msikiti Mtukufu wa Makkah na Msikiti wa Mtume (SAW) maarufu kama Al Masjid An Nabawi, ametangaza nafasi mbalimbali za kujitolea kwa msimu wa Hajj wa mwaka huu. Mpango huu unalenga kuimarisha ushiriki wa jamii, kukuza kazi za kujitolea, na kuimarisha zaidi utamaduni wa kujitolea ndani ya jamii.
Miongoni mwa majukumu ya kujitolea yaliyotangazwa ni: kutoa mwongozo na mafunzo ya kidini kwa mahujaji, kusaidia katika kupanga mistari ya swala, kufuatilia skrini na vifaa vya kielektroniki, kutoa huduma za tafsiri kwa wageni, kufanya kampeni za uhamasishaji wa waumini, na kuwatumikia wageni na mazuwaru wa Msikiti wa Mtume (SAW). Uongozi huo umewaalika wale wote wanaotamani kushiriki kujisajili kupitia Jukwaa la Kitaifa la Kazi za Kujitolea na kuwasilisha maombi kwa nafasi zilizopo.
3497380