Kikao cha intaneti (webinari) chini ya anuani ya "Hija; Mhimili wa Qur'ani na Kufungamana na Gaza", kitaandaliwa na Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA) Jumatatu Juni 10 saa kumi na mbili asubuhi kwa saa za CET.
Watoa mada katika semina hiyo ya mtandaoni watajadili masuala yanayohusiana na changamoto kuu katika ulimwengu wa Kiislamu, uungaji mkono kwa wananchi madhulumu wa Palestina na mapambano yao dhidi ya Wazayuni kwa kuzingatia mafundisho ya Qur'ani Tukufu, matokeo ya Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa. na jukumu lake katika kuliweka hai suala la Palestina, na ulazima wa kusisitiza Bara'at (kukiweka mbali) na adui Mzayuni katika Hija ya mwaka huu, miongoni mwa mengine.
Profesa wa Chuo Kikuu cha Tehran Mohammad Ali Azarshab, Mkuu wa Jumuiya ya Wanazuoni wa Kiislamu nchini Lebanon Sheikh Ghazi Hunaina, Mkuu wa Umoja wa Wanazuoni wa Ahl al-Bayt wa Uturuki Ghadir Akaras, Mkuu wa Baraza la Ushauri la Jumuiya za Kiislamu la Malaysia (MAPIM) Muhammad Azmi Abdulhamid, na Mtaalamu wa Uislamu kutoka Canada John Andrew Morrow atahutubia mtandao huo.
Webinari hii itarushwa moja kwa moja kutoka katika ukurasa wa IQNA kwenye tovuti ya Aparat chini ya anuani ya https://www.aparat.com/iqnanews/live
4219681