Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, mpango wa Marekani uliopachikwa jina la Muamala wa Karne utakufa hata kabla ya Trump mwenyewe kufa na kuongeza kuwa, njia ya kukabiliana na mpango huo ni kusimama kidete na kufanya jihadi kishujaa taifa na makundi ya Palestina pamoja na uungaji mkono wa ulimwengu wa Kiislamu kwa taifa hilo.
Habari ID: 3472444 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/05
TEHRAN (IQNA)- Mgawanyiko mkubwa umedhihirika katika uga wa kisiasa Marekani wakati rais Donald Trump wa nchi hiyo alipokuwa akitoa hotuba ya kila mwaka mbele ya Bunge la Kongresi huku mchakato wa kumuondoa madakarani ukikaribia kumalizika.
Habari ID: 3472442 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/05
TEHRAN (IQNA) –Mwanazuoni wa ngazi za juu nchini Sudan amelaani vikali mkutano wa hivi karibuni wa wa Mkuu wa Baraza la Utawala la Sudan Luteni Jenerali Abdel Fattah al-Burhan na Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa Utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3472441 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/05
TEHRAN (IQNA) - Msikiti wa kwanza kabisa katika historia ya Slovenia umefunguliwa Jumatatu katika mji mkuu, Ljubljana baada ya Waisalmu kuvuka vizingiti ya kifedha na upinzani wa watu wenye mismamo mikali ya mrengo wakulia.
Habari ID: 3472439 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/04
RIPOTI
TEHRAN (IQNA)- Ripoti mpya imefichua kuwa, Saudia Arabia ilitumia mamluki wa Ufaransa kuua na kukandamiza Waislamu waliokuwa wameanzisha mwamko dhidi ya ufalme wa Saudi Arabia katika Msikiti Mtakatifu wa Makka (Al-Masjid Al-Haram) mwaka 1979.
Habari ID: 3472438 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/04
TEHRAN (IQNA) – Msikiti mkubwa zaidi katika eneo la Asia ya Kati uliojengwa katika mji mkuu wa Tajikistan, Dushanbe, utafungulwia rasmi mwezi ujao wa machi.
Habari ID: 3472437 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/03
TEHRAN (IQNA) - Katibu wa Jumuiya ya Kukurubisha Madhehebu ya Kiislamu amesema kuwa, Palestina ndio mpaka wa ulimwengu wa Kiislamu na kwamba suala la kuilinda na kuihami Palestina ni wajibu wa Kiqur'ani wa kila Muislamu.
Habari ID: 3472436 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/03
TEHRAN (IQNA) - Nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) zimepinga mpango wa 'muamala wa karne' uliopendekezwa na Marekani ambao unakandamiza haki za taifa la Palestina.
Habari ID: 3472435 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/03
TEHRAN (IQNA)- Kamanda mpya wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaendelea kuwaunga mkono Wapalestina na kuhakikisha kuwa ndoto zao za kuwa taifa huru zinafanikiwa.
Habari ID: 3472433 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/02
TEHRAN (IQNA) - Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameutaja 'Muamala wa Karne' kama mpango wa Marekani wa kufedhehesha, aibu na wenye kuchukiza.
Habari ID: 3472432 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/02
TEHRAN (IQNA) – Msomi nchini Afrika Kusini amesema jamii barani Afrika zina nafasi muhimu katika kukabiliana na misimamo mikali ya kidini kwani serikali pekee haziwezi kukabiliana na tatizo hilo.
Habari ID: 3472431 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/02
TEHRAN (IQNA) – Iwapo Waislamu nchini Marekani wanataka 'kuonekana' na masuala yao yazingatiwe katika ngazi za maamuzi muhimu, basi wanapaswa kushiriki katika uchaguzi ujao wa rais nchini humo.
Habari ID: 3472430 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/01
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu amekosoa tangazo la mpango wa Marekani na Israel unaojulikana kama 'muamala wa karne' kwa ajili ya kutatua kadhia ya Palestina na kusema nchi za Kiarabu katu hazitaliacha taifa la Palestina peke yake.
Habari ID: 3472429 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/01
TEHRAN (IQNA) – Watetezi wa haki za wahamiaji na haki za binadamu wamemlaani Rais Donald Trump wa Marekani kwa kupanua marufuku ya nchi ambazo raia wake wanakabiliwa na vizingiti vya uhamiaji kuingia nchini humo, hatua ambayo imetajwa kuwa na ajenda ya chuki dhidi ya raia wa kigeni.
Habari ID: 3472428 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/01
Khatibu wa Sala ya Ijuma Tehran
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran ameilaani Marekani kwa kuanzisha njama mpya dhidi ya Waislamu kwa jina la "Muamala wa Karne" na kusema kuwa, njama hizo zitafeli na kushindwa tu.
Habari ID: 3472425 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/31
Wananchi wa Yemen wamefanya maandamano makubwa ya kulaani njama mpya za Marekani dhidi ya taifa madhlumu la Palestina na wamelaani vikali mpango wa Donald Trump wa "Muamala wa Karne."
Habari ID: 3472424 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/31
TEHRAN (IQNA) - Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wameuhujumu Msikiti wa Al Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na utawala huo na kuwajeruhi Wapalestina kadhaa waliokuwa wamefika hapo kwa ajili ya Sala ya Ijumaa.
Habari ID: 3472423 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/31
Ismail Haniya
TEHRAN (IQNA) - Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano (Muqawama) ya Kiislamu ya Palestina HAMAS, Ismail Haniyeh ametuma ujumbe kwenda kwa viongozi wa nchi za Kiarabu na Kiislamu akionya ushiriki wa aina yoyote kwa ajili ya kutekelezwa au kuukubali mpango wa Muamala wa Karne na kubainisha kuwa hilo ni kosa kubwa ambalo kamwe raia wa Palestina hawatalisamehe.
Habari ID: 3472422 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/30
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema pendekezo la Marekani lililopewa jina la 'Muamala wa Karne' katu halitazaa matunda kwa Rehema za Mwenyezi Mungu.
Habari ID: 3472421 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/30
TEHRAN (IQNA) – Kauli mbiu ya Maonyesho ya 28 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran itakuwa ni 'Qur'ani Tukufu Kitabu cha Ustawi."
Habari ID: 3472420 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/30