Balozi wa Palestina Tehran
TEHRAN (IQNA) - Balozi wa Palestina nchini Iran amesema utawala haramu wa Israel unapaswa kusitisha ukaliaji mabavu ardhi za Palestina huku akisisitiza kuwa, Palestina ni lazime irejee kwa Wapalestina.
Habari ID: 3472037 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/07/09
TEHRAN (IQNA) - Mwana wa Sheikh Ibrahim Zakzaky Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu nchini Nigeria ametahadharisha kupitia ujumbe aliotoa kwamba hali ya kimwili ya baba yake ni mbaya sana. Amesema karibu njia zote zimeshindikana kwa ajili ya kunusuru maisha yake.
Habari ID: 3472036 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/07/09
TEHRAN (IQNA) - Shirika moja la anga za mbali la nchini Russia ambalo hutayarisha chakula cha wanaanga (astronauts) kimesema kitaanza kutayarisha chakula halali maalumu kwa ajili ya Waislamu.
Habari ID: 3472033 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/07/07
TEHRAN (IQNA) - Vyuo vikuu vya umma nchini Indonesia vimetangaza kuwa vijana waliohifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu wanaweza kuingia katika vyuo vikuu pasina kufanya mtihani wa kawaida unaohitajika kuingia chuo kikuu.
Habari ID: 3472032 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/07/04
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema serikali ya Saudi Arabia ina wajibu na majukumu mazito ya kulinda usalama wa mahujaji wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu na hadhi yao bila ya kueneza anga ya kipolisi.
Habari ID: 3472031 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/07/03
Mtume Muhammad SAW amesema: Umoja ni chanzo cha rehema na mifarakano inasababisha adhabu. Kanz al Ummal Hadithi ya 20242
Habari ID: 3472027 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/07/01
TEHRAN (IQNA)- Baada ya kupita miaka mitatu na nusu tangu serikali ya Nigeria ianze kumshikilia kinyume cha sheria Mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria, Sheikh Ibrahim Zakzaky na kuendelea kukaidi amri ya Mahakama Kuu ya kuachiliwa huru mwanachuoni huo, hivi sasa hali ya kiongozi huyo wa Waislamu imezidi kuwa mbaya.
Habari ID: 3472021 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/06/29
TEHRAN (IQNA)- Maisan Yahya Muhammad, ni binti wa miaka sita ambaye kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ambaye amehifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu.
Habari ID: 3472020 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/06/28
TEHRAN (IQNA)- Aghalabu ya Wapalestina wanapinga vikali mpango wa Muamala wa Karne na kikao cha uchumi kulichofanyika hivi karibuni mjini Manama, Bahrain.
Habari ID: 3472019 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/06/27
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa lengo kuu la pendekezo la Marekani la kufanya mazungumzo na Iran ni kutaka kulipokonya taifa la Iran silaha na sababu za nguvu na uwezo wake.
Habari ID: 3472018 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/06/26
Sheikh Issa Qassim
TEHRAN (IQNA) - Mwanazuoni maarufu wa Kiislamu nchini Bahrain, Ayatullah Sheikh Isa Qassim amelaani vikali hatua ya utawala wa Manama kuwa mwenyeji wa Kongamano la Kibiashara linalotazamiwa kuanza leo nchini humo kwa shabaha ya kuzindua mpango wa 'Muamala wa Karne'.
Habari ID: 3472017 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/06/25
TEHRAN (IQNA) – ‘Muamala wa Karne’ ambao umependekezwa na Marekani kwa lengo la kuunga mkono utawala wa Kizayuni wa Israel na kukandamiza ukombozi wa Palestina unaendelea kupingwa katika ulimwengu wa Kiislamu.
Habari ID: 3472016 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/06/24
TEHRAN (IQNA) – Msikiti mpya uliopewa jina la Masjid Tawheed umefunguliwa mapema wiki hii katika mji wa Venlo, kusini mashariki mwa Uholanzi.
Habari ID: 3472012 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/06/23
TEHRAN (IQNA) – Mwanazuoni wa Kiislamu nchini Uingereza amechapisha fatwa mpya kuhusu kuchangia viungo vya mwili.
Habari ID: 3472011 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/06/22
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo Tehran ameashiria hatua ya kutunguliwa ndege isiyo na rubani (drone) ya Marekani ambayo ilikuwa imekiuka anga ya Iran na kusema: "Wakuu wa Marekani wafahamu kuwa, Lango Bahari la Hormoz daima litakuwa kaburi la wavamizi."
Habari ID: 3472009 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/06/21
TEHRAN (IQNA) – Mchunguzi maalumu wa Umoja wa Mataifa ametangaza kuwa ushahidi unaonyesha mrithi wa ufalme wa Saudi Arabia na maafisa kadhaa wa ngazi ya juu wa ufalme huo walihusika na mauaji ya mwandishi habariJamal Khashoggi.
Habari ID: 3472008 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/06/20
TEHRAN (IQNA) – Marekani inaendelea kuficha jinai za kivita za utawala wa Saudia Arabia na waitifaki wake ambao wanaendelea na uvamizi wao dhidi ya taifa la Yemen.
Habari ID: 3472007 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/06/19
TEHRAN (IQNA) – Mwenyekiti wa Jumyuiya ya Kimataifa ya Maulamaa Waislamu (IUMS) amezituhumu tawala za Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kuwa zimehusika katika kifo cha rais wa zamani wa Misri Muhammad Mursi.
Habari ID: 3472006 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/06/18
TEHRAN (IQNA) - Vikosi vya Yemen vimetekeleza shambulizi jingine la ulipizaji kisasi kwa kuulenga uwanja wa ndege wa Abha, katika mkoa wa Asir kusini mwa Saudi Arabia. Shambulizi hilo limetekelezwa ikiwa ni katika kulipiza kisasi jinai dhidi ya Wayemen ambazo zimekuwa zikitekelezwa na Saudia na waitifaki wake katika kipindi cha miaka minne sasa.
Habari ID: 3472005 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/06/17
Iran na Hamas zasisitiza:
TEHRAN (IQNA) - Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) zimesema utawala wa rais Donald Trump wa Marekani unalenga kuangamiza taifa la Palestina kupitia 'Muamala wa Karne' ulio kwa maslahi ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika eneo la Asia Magharibi.
Habari ID: 3472004 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/06/16