iqna

IQNA

TEHRAN (IQNA) - Mamilioni ya Waislamu kote duniani hii leo wanaomboleza katika siku ya Ashura ambayo ni siku aliyouawa shahidi mjukuu wa Mtume Muhammad SAW, Imam Hussein AS.
Habari ID: 3472122    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/09/10

TEHRAN (IQNA) – Waislamu kote duniani usiku wa kuamkia leo tarehe 9 Mfunguo Nne Muharram wameshiriki katika vikao, majlisi na shughuli za maombolezo na kukumbuka misiba na masaibu yaliyomkuta mjukuu wa Mtume wetu Muhammad SAW, Imam Hussein bin Ali AS, ndugu na mswahaba zake waaminifu huko Karbala nchini Iraq mwaka 61 Hijria.
Habari ID: 3472121    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/09/09

TEHRAN (IQNA) – India imeweka sheria ya kutotoka nje katika sehemu kadhaa la eneo linalozozaniwa la Kashmir baada ya jeshi kkuwashambulia Waislamu wa madhehebu ya Shia waliokuwa wanashiriki katika maombolezo ya mwezi wa Muharram.
Habari ID: 3472120    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/09/08

TEHRAN (IQNA) - Utawala wa kiimla wa Bahrain umeanzisha wimbi jipya la kuwakandamiza wanazuoni wa Kiislamu wa madhehebu ya Shia katika mwezi huu wa Muharram.
Habari ID: 3472118    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/09/07

TEHRAN (IQNA) - Mijumuiko ya Kimataifa kwa jina la "Watoto Wachanga Wanaonyonya wa Hussein AS" imefanyika leo Ijumaa katika zaidi ya maeneo elfu sita katika Iran ya Kiislamu na katika nchi 45 duniani sambamba na Ijumaa ya kwanza ya mwezi wa Muharram.
Habari ID: 3472117    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/09/06

Inna Lillah wa Inna Ilayhi Rajioun
TEHRAN (IQNA) – Mwanamke wa Russia aliyesilimu na kisha kutarjumi Qur'ani Tukufu kwa lugha ya Kirussia amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 79.
Habari ID: 3472116    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/09/05

Rais Hassan Rouhani
TEHRAN (IQNA) - Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameatangaza kuwa, awamu ya tatu ya Iran kupunguza uwajibikaji wake katika makubaliano ya nyuklia ya Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezwaji (JCPOA) itaanza kutekelezwa Ijumaa.
Habari ID: 3472115    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/09/05

TEHRAN (IQNA)- Mzungu mbaguzi mwenye kufuatia itikadi ya wale wanaoamini wazungu ndio wanadamu bora zaidi duniani, amefungwa jela miaka 12 nchini Uingereza baada ya kupatikana na hatia ya kuchochea mauaji ya Waislamu.
Habari ID: 3472114    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/09/04

TEHRAN (IQNA)- Afisa mkuu wa Umoja wa Mataifa anayesghulikia masuala ya hukumu zisizofuata sheria na pia mauaji ya kiholela, Agnes Callamard, ameilaani serikali ya Nigeria kwa kutekeleza mauaji na kutumia nguvu ziada dhidi ya Harakati ya Kiislamu nchini humo.
Habari ID: 3472112    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/09/03

TEHRAN (IQNA) – Wanajeshi wa utawala ghasibu wa Israel wamebomoa msikiti wa Wapalestina katika mji wa al Khalil eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
Habari ID: 3472111    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/09/03

TEHRAN (IQNA) - Ismail Hania Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amemuandikia barua Ayatullah Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na kushukuru yale aliyoyazungumza katika mkutano wake na ujumbe wa harakati hiyo uliofanya ziara hapa mjini Tehran hivi karibuni .
Habari ID: 3472110    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/09/02

Baada ya onyo kali la Sayyed Hassan Nasrallah
TEHRAN (IQNA) - Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imeangamiza moja ya zana za kijeshi za Israel katika barabara ya al Thakna katika mji wa mpakani wa Israel wa Avivim na kumuua kamanda wa kikosi kimoja wa jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel huko kaskazini mwa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu katika oparesheni iliyotekelezwa na harakati ya Hizbullah.
Habari ID: 3472109    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/09/02

TEHRAN (IQNA) – Jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel limewafyatulia risasi na kuwajeruhi makumi ya Wapalestina waliokuwa wakiandamana kwa amani katika Ijumaa ya 72 ya maandamano ya 'Haki ya Kurejea' huko katika Ukanda wa Ghaza.
Habari ID: 3472107    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/08/31

TEHRAN (IQNA) – Vijana kadhaa waliohifadhi Qur'ani Tukufu nchini Bulgaria wameenziwa na kutunukiwa zawadi.
Habari ID: 3472106    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/08/30

TEHRAN (IQNA)- Washindi katika mashindano ya kitaifa ya kihifadhi Qur'ani wametunukiwa zawadi katika sherehe iliyofanyika Jumatano katika Ukumbi wa Kituo cha Kiutamaduni na Kiislamu cha mji w Gitega.
Habari ID: 3472105    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/08/29

TEHRAN (IQNA) – Mwanaanga wa kwanza wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kufika katika anga za mbali amesema atabeba nakala ya Qur'ani katika safari yake hiyo ya kihistoria.
Habari ID: 3472104    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/08/28

Inna Lillah wa Inna Ilayhi Rajioun
TEHRAN (IQNA) – Yahya (Christian) Bonaud, mwanafikra Mfaransa, msomi na mtarjumi wa Qur'ani Tukufu kwa lugha ya Kifaransa amefariki Jumatatu akiwa na umri wa miaka 62.
Habari ID: 3472103    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/08/27

TEHRAN (IQNA) - Wakimbizi wapatao laki mbili Waislamu wa jamii ya Rohingya wa nchini Myanmar Jumapili walishiriki kwenye kumbukumbu ya mwaka wa pili tangu jeshi la Myanmar lilipowakandamiza na kuwalazimisha kuyahama makazi yao kwa umati na kukimbilia nchi jirani ya Bangladesh ili kunusuru maisha yao.
Habari ID: 3472102    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/08/27

TEHRAN (IQNA) - Sayyid Hassan Nasrallah, Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amehutubu Jumapili usiku mjini Beirut kwa munasaba wa kukombolewa eneo la Juroud Arsal kutoka mikononi mwa magaidi, na katika hotuba yake ametoa radiamali kali kuhusu mashambulizi ya hivi karibuni dhidi ya mhimili wa muqawama na kusema jeshi la Israel lisubiri jibu wakati wowote ule kuanzia Jumatatu usiku.
Habari ID: 3472101    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/08/26

Jarida la Time
TEHRAN (IQNA) – Jarida la kimataifa la Time limetangaza orodha ya 'Maeneo 100 Bora ya Kutembelea Duniani 2019' na Bustani ya Qur'ani ya Dubai ni miongoni mwa maeneo hayo.
Habari ID: 3472099    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/08/25