Sheikh Isa Qassim
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Bahrain amesema jitihada za taifa hilo la Kiarabu katu hazitazimwa na dhulma na ukandamizaji unaofanywa na vyombo vya usalama vya utawala wa kiukoo unaoingoza nchi hiyo kwa mkono wa chuma.
Habari ID: 3473650 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/02/14
TEHRAN (IQNA) - Wakati ukikaribia mwaka wa 10 tokea uanze mwamko wa wananchi wa Bahrain dhidi ya utawala wa ukoo wa Aal Khalifa nchini humo, utawala huo dhalimu umeshadidisha ukandamizaji na utumiaji mabavu dhidi ya wananchi wanaotaka mabadiliko.
Habari ID: 3473644 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/02/12
TEHRAN (IQNA) - Wananchi wa Bahrain leo wameandamana kulaani hatua ya ukoo wa Aal Khalifa unaotawala nchi hiyo kuanzisha uhusiano na utawala haramu wa Israel.
Habari ID: 3473560 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/01/15
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu nchini Bahrain amesema kuwa dhulma na ukandamizaji unaofanywa na utawala wa ukoo wa Aal Khalifa dhidi ya taifa la Bahrain umeifanya nchi hiyo kuwa sawa na gereza kubwa
Habari ID: 3473533 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/01/07
TEHRAN (IQNA) - Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kitendo cha baadhi ya nchi za Kiarabu cha kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel ni kuwasaliti wananchi wa Palestina na umma wa Kiislamu kwa ujumla.
Habari ID: 3473488 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/12/24
TEHRAN (IQNA) - Harakati za kupigania ukombozi wa Palestina zimelaani vikali hatua ya Morocco kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel.
Habari ID: 3473444 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/12/11
TEHRAN (IQNA)- Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imelaani kauli aliyotoa waziri wa biashara, viwanda na utalii wa Bahrain kuhusu azma ya nchi yake ya kununua bidhaa zinazozalishwa katika vitongoji vya walowezi wa Kizayuni kwenye Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan.
Habari ID: 3473421 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/12/04
TEHRAN (IQNA) - Mwanazuoni na kiongozi juu wa Kiislamu wa Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Bahrain amesema kuwa, matokeo ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel yatakuwa hatari na yatasababisha majanga.
Habari ID: 3473414 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/12/02
TEHRAN (IQNA)- Mjumbe wa Mfalme wa Bahrain na wenzake aliofuatana nao wameingia msikiti wa Al Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem), unaokaliwa kwa mabavu na Israel, kwa kujificha wakihofu wasije wakatambuliwa na Wapalestina.
Habari ID: 3473409 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/11/30
TEHRAN (IQNA) - Ufalme wa Saudi Arabia umesisitiza kwamba unaunga mkono uanzishwaji uhusiano kamili na kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3473382 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/11/22
TEHRAN (IQNA) - Waziri wa Mambo ya Nje wa Bahrain ameongoza ujumbe wa ngazi za juu wa serikali ya Manama kutembelea utawala haramu wa Israel ambao uko katika ardhi za Palestina ambazo unazikalia kwa mabavu.
Habari ID: 3473373 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/11/19
TEHRAN (IQNA)- Waziri Mkuu wa Palestina amelaani kitendo cha kuruhusiwa ujumbe wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kuingia ndani ya Msikiti wa al Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) huku Wapalestina wakizuiwa kuswali katika msikiti huo.
Habari ID: 3473279 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/20
TEHRAN (IQNA)- Wananchi wenye hasira nchini Bahrain wameandamana kupinga safari ya ujumbe wa Marekani-Kizayuni katika nchi yao kwa lengo la kutangaza rasmi mapatano ya kuanzishwa uhusiano wa kawaida kati ya Bahrain na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3473276 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/19
TEHRAN (IQNA) - Asilimia 95 ya wananchi wa Bahrain wanapinga hatua ya utawala wa kifalme nchini humo kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel.
Habari ID: 3473272 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/18
TEHRAN (IQNA) – Mtaalamu maarufu wa kisiasa Kuwaita amelaani hatua ya baadhi ya nchi za Kiarabu kuanzisha uhusiano kamili wa kidiplomasia na Israel na kutaja hatua hiyo kuwa sawa na ukoloni mamboleo.
Habari ID: 3473257 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/13
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi wa harakati ya Ikhwanul Muslimin ya Sudan amekosoa hatua ya baadhi ya nchi za Kiarabu ya kuanzisha uhusiano rasmi wa kidiplomasia na utawala wa Kizayuni wa Israel na kusema, hatua hiyo ni usaliti kwa kadhia ya Palestina.
Habari ID: 3473243 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/09
TEHRAN (IQNA) – Mrithi wa Ufalme wa Saudi Arabia, Mohammad bin Salman, ameutembelea utawala wa Kizayuni wa Israel mara kadhaa kwa siri, amefichua afisa wa zamani wa usalama katika utawala huo.
Habari ID: 3473237 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/07
TEHRAN (IQNA) – Wananchi wa Bahrain wameandamana tena Ijumaa katika mji mkuu Manama na miji mingine kupunga hatua ya utawala wa kifalme nchini humo kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel.
Habari ID: 3473228 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/03
TEHRAN (IQNA)- Chama kikuu cha upinzani cha Bahrain kinachojulikana kama Jumuiya ya Kiislamu ya Al Wifaq kimetangaza kuwa kumefanyika maandamano 150 ya kupinga hatua ya watawala wa nchi hiyo kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3473198 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/09/23
TEHRAN (IQNA) - Rais Abdelmadjid Tebboune wa Algeria amesisitiza kuwa, nchi yake inapinga vikali hatua zozote zile zenye lengo la kuanzisha uhusiano na utawala vamizi wa Israel unaotenda jinai kila leo dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina.
Habari ID: 3473190 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/09/21