IQNA

Maandamo 150 yamefanyika Bahrain kupinga uhusiano na Israel

17:59 - September 23, 2020
Habari ID: 3473198
TEHRAN (IQNA)- Chama kikuu cha upinzani cha Bahrain kinachojulikana kama Jumuiya ya Kiislamu ya Al Wifaq kimetangaza kuwa kumefanyika maandamano 150 ya kupinga hatua ya watawala wa nchi hiyo kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Taarifa hiyo imesema maandamano hayo yamefanyika katika maeneo 55 katika nchi hiyo ya Kiarabu pamoja na kuwepo ukandamizaji mkali wa vyombo vya dola.

Taarifa hiyo imesema maandamano hayo yalianza tokea siku ya kwanza ya kutangazwa mapatano ya Bahrain na utawala Bandai wa Israel na yangali yanaendelea.

Tarehe 15 mwezi huu wa Septemba mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Bahrain walisaini mapatano ya kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel na Waziri Mkuu wa utawala huo, Benjamin Netanyahu katika ikulu ya rais wa Marekani, White House mjini Washington.  Hadi hivi sasa ulimwengu mzima wa Kiislamu bali hata baadhi ya nchi zisizo za Waislamu, kama Afrika Kusini zinalaani kitendo hicho cha kisaliti cha Bahrain na UAE. Hatua hiyo ya UAE na Bahrain imetajwa kuwa ni usaliti kwa kwa malengo ya ukombozi wa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel.

3472615

captcha