IQNA

Wabahrain waandamana kulaani uhusiano wa nchi yao na utawala wa Israel

23:31 - January 15, 2021
Habari ID: 3473560
TEHRAN (IQNA) - Wananchi wa Bahrain leo wameandamana kulaani hatua ya ukoo wa Aal Khalifa unaotawala nchi hiyo kuanzisha uhusiano na utawala haramu wa Israel.

Maandamano hayo yamefanyika baada utawala haramu wa Israeli kumteua balozi wake mdogo atakayetumwa Bahrain. Wananchi wenye hasira wameandamana katika mji mkuu wa Bahrain, Manama ambapo wameteketeza moto bendera za utawala haramu wa Israel.

تظاهرات بحرینی‌ها محکومیت سازش با رژیم صهیونیستی

Maandamano hayo ya Ijumaa yamefanyika pia kwa mnasaba wa mwaka wan ne tokea utawala wa kiimla wa Bahrain uwanyonge vijana watatu ambao ni Abbas al-Samea, Ali al-Singace na Sami Mushaima ambao walinyongwa Januari 15 mwaka 2017.

تظاهرات بحرینی‌ها در محکومیت سازش با رژیم صهیونیستی

Vijana hao walinyongwa baada ya kupachikwa tuhuma za bandia kuwa eti walimuua afisa wa polisi kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu ambaye alikuwa katika kikosi kilichotumwa Bahrain kukabiliana na waandamnaji.

Ikumbukwe kuwa, mwaka wa 2020, nchi nne za Kiarabu ambazo ni Umoja wa Falme za Kiarabu, Bahrain, Sudan na Morocco zilitangaza kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel na hivyo kujiunga na Misri na Jordan ambazo zinautambua utawala huo ghasibu.

Inaaminika kuwa Saudi Arabia nayo tayari ina uhusiano wa siri na utawala haramu wa Israel lakini inahofia kuutangaza uhusiano huo hadharani utaharibu sura yake kabisa katika ulimwengu wa Kiislamu.

3947891

Kishikizo: bahrain israel
captcha