iqna

IQNA

TEHRAN (IQNA) - Kwa mara nyingine tena jarida hilo la Kifaransa la Charlie Hebdo limeamua kwa makusudi kuwafanyia kejeli na istihzai Waislamu na dini tukufu ya Uislamu kwa kuchapisha vibonzo vyenye kuvunjia heshima matukufu ya Kiislamu.
Habari ID: 3473129    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/09/02

Waislamu wa mji wa Arusha nchini Tanzania walijimuika na wenzao duniani katika kukumbuka kuuawa shahidi Imam Hussein AS katika siku ya Ashura.
Habari ID: 3473128    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/09/01

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameitaja hatua ya serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ya kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni kuwa ni kuusaliti Ulimwengu wa Kiislamu, Ulimwengu wa Kiarabu na nchi za eneo na kadhia muhimu ya Palestina.
Habari ID: 3473127    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/09/01

Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Maulamaa Waislamu
TEHRAN (IQNA) - Mkuu wa Umoja wa Kimataifa wa Maulamaa wa Kiislamu amesema kwamba, kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu, ni haramu kuwa na uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3473125    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/09/01

TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito kwa kutatuliwa tatizo la mgogoro wa wakimbizi Warohingya kupitia utatuzi wa chanzo kikuu cha sababu za wao kukimbia makazi yao nchini Myanmar.
Habari ID: 3473113    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/08/28

TEHRAN (IQNA) –Mahakama nchini New Zealand imemhukumu kifungo cha maisha jela gaidi Brenton Tarrant baada ya kupatikana na hatia ya kuwaua Waislamu 51 wakati wa swala ya Ijumaa mwezi Machi mwaka jana katika mji wa Christchurch.
Habari ID: 3473108    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/08/27

TEHRAN (IQNA) – Waislamu Warohingya ambao ni wakimbizi nchini Bangladesh leo wameshiriki katika 'maandamano ya kimya kimya' kukumbuka mwaka wa tatu tokea waanze kufurushwa makwao nchini Myanmar.
Habari ID: 3473102    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/08/25

TEHRAN (IQNA) –Idara ya Polisi katika jimbo la Karbala nchini Iraq imetangaza kuwa ni marufuku kwa watu wasio wakaazi kuingia katika jimbo hilo hadi tarehe 13 Muharram inayosadifiana na 2 Septemba.
Habari ID: 3473099    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/08/24

TEHRAN (IQNA) – Waziri wa Wakfu nchini Misri Sheikh Mukhtar Gomaa, ameamuru kuazishwe kampeni ya kitaifa ya kutayarisha misikiti kote nchini kwa ajili ya Swala ya Ijumaa wiki hii.
Habari ID: 3473094    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/08/23

TEHRAN (IQNA) – Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) limetoa wito wa kutafutulwia suluhisho jipya na la kudumu kwa wakimbizi Waislamu wa jamii ya Rohingya walio ndani na nje ya Myanmar.
Habari ID: 3473092    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/08/22

TEHRAN (IQNA) – Waislamu nchini Uingereza wameitaka serikali ya nchi yao ichukue hatua kali dhidi ya China kutokana na kukandamizwa Waislamu wa jamii ya Uighur.
Habari ID: 3473088    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/08/20

TEHRAN (IQNA) - Ayatullah Ali Taskhiri, mshauri mwandamizi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kuhusu masuala ya ulimwengu wa Kiislamu alikuwa mmoja kati ya walinganiaji wa umoja na ukuruba baina ya madhehebu za Kiislamu.
Habari ID: 3473082    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/08/19

TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kuyakurubisha Pamoja Madhehebu ya Kiislamu amesema kuwa: kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na utawala wa Kizayuni wa Israel ni kuisaliti Qurani Tukufu na kumpa mgongo Mtume wa Mwenyezi, Muhammad SAW
Habari ID: 3473078    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/08/17

TEHRAN (IQNA) – Misikiti imefunguliwa tena nchini Algeria baada ya kufungwa kwa muda wa miezi mitano.
Habari ID: 3473074    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/08/16

Imamu wa saba wa Waislamu wa madhehebu ya Shia duniani, ni Imam Musa bin Ja'afar Al-Kadhim (AS) ambaye ana lakabu ya Babul Hawaij, kwa sababu ya watu kutasawali kwa Mwenyezi Mungu Mola Mweza kupitia kwake.
Habari ID: 3473071    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/08/16

TEHRAN (IQNA) – Maandamano makubwa yamefanyika nchini India kulaani kitendo cha kuchapshwa maandishi yanayomvunjia heshima Mtume Mtukufu wa Uislamu Muhammad, Rehma na Amani ya Allah iwe Juu Yake na Kizazi Chake (SAW)
Habari ID: 3473064    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/08/13

Afisa wa Umoja wa Mataifa
TEHRAN (IQNA) – Mkuu wa taasisi ya Umoja wa Mataifa inayochunguza jinai dhidi ya Waislamu wa jamii ya Rohingya nchini Myanmar amesema Shirika la Facebook limekataa kutoa ushahidi wa jinai za kimataifa hata baada ya kuahidi kushirikiana kuhusu katika kadhia hiyo.
Habari ID: 3473058    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/08/11

TEHRAN (IQNA) - Mahakama moja wa Kiislamu nchini Nigeria imemhukumu kifo mwanamuziki ambaye alikufuru na kumvunjia heshima Mtume Muhammad SAW.
Habari ID: 3473056    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/08/11

TEHRAN (IQNA) – Polisi katika jimbo la Minnesota Marekani wanawasaka vijana wawili ambao walimpiga na kumuumiza kiongozi wa Waislamu katika eneo hilo. Vijana hao wawili wanakisiwa kuwa na umri wa miaka 20 hivi na mmoja ni mzungu huku mwingine akiwa na asili ya Afrika.
Habari ID: 3473050    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/08/09

TEHRAN (IQNA)- Serikali ya Canada imeongeza walinzi wa Ali Saad al-Jabri, mkuu wa zamani wa Idara ya Ujasusi ya Saudi Arabia ikihofia kuuawa na serikali na Saudi Arabia.
Habari ID: 3473049    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/08/09