iqna

IQNA

TEHRAN (IQNA)- Msikiti wa kwanza katika mji mkuu wa Ugiriki, Athens umefunguliwa baada ya miaka 14 ya vuta nikuvute na urasimu kupita kiasi.
Habari ID: 3473329    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/11/04

TEHRAN (IQNA) - Wimbi kali la maandamano ya kulaani matamshi yaliyotolewa na Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa akitetea matusi na kuvunjiwa heshima Mtume Muhammad SAW Nchini humo limeendelea kushuhudiwa katika pembe mbalimbali za dunia.
Habari ID: 3473325    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/11/03

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika Hotuba ya Miladj un Nabii SAW
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amezungumzia siasa za kimantiki za kusimama kidete kukabiiliana na sera za kibabe za Marekani na kusema kuwa, sera zenye mahesabu za Jamhuri ya Kiislamu hazibadiliki kwa kuondoka kiongozi na kuja mwingine madarakani huko Marekani.
Habari ID: 3473323    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/11/03

TEHRAN (IQNA)- Serikali ya Saudi Arabia imewaruhusu waislamu wanaoishi nje ya ufalme huo kuingia nchini humo kwa ajili ya kutekeleza ibada ya Umra baada ya kufungwa mwezi Machi mwaka huu kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.
Habari ID: 3473317    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/11/01

Kiongozi wa Ansarullah
TEHRAN (IQNA)-Katibu Mkuu wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema rais Emmanuel Macron wa Ufaranmsa ni kikaragosi kinachochezeshwa na Wazayuni kichukue hatua za kuutusi na kuuvunjia heshima Uislamu.
Habari ID: 3473309    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/30

TEHRAN (IQNA) - Makumi ya maelfu ya Waislamu wa Bangladesh wamefanya maandamano katika mji mkuu Dhaka, kulaani hatua ya Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa ya kuunga mkono kitendo cha kifidhuli cha jarida la Kifaransa la Charlie Hebdo cha kuchapisha tena vibonzo vya kumvunjia heshima Mtume Muhammad SAW.
Habari ID: 3473303    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/28

TEHRAN (IQNA) – Baraza Kuu la Waislamu Uganda (UMSC) limefanikiwa kumiliki televisheni kwa ajili ya kueneza mafundisho ya Kiislamu na harakati za Kiislamu.
Habari ID: 3473298    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/26

TEHRAN (IQNA) – Wanawake wawili ambao waliwashambuliwa wanawake wengine Waislamu waliokuwa wamevaa Hijabu mjini Paris, wamefikishwa kizimbani.
Habari ID: 3473289    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/23

TEHRAN (IQNA)- Waziri Mkuu wa Palestina amelaani kitendo cha kuruhusiwa ujumbe wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kuingia ndani ya Msikiti wa al Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) huku Wapalestina wakizuiwa kuswali katika msikiti huo.
Habari ID: 3473279    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/20

Sayyid Abdulmalik Badruddin al-Houthi
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema mashirika ya kijasusi ya nchi za Magharibi ndiyo ambayo yaliibua makundi ya magaidi wakufirishaji duniani.
Habari ID: 3473278    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/20

TEHRAN (IQNA)- Wananchi wenye hasira nchini Bahrain wameandamana kupinga safari ya ujumbe wa Marekani-Kizayuni katika nchi yao kwa lengo la kutangaza rasmi mapatano ya kuanzishwa uhusiano wa kawaida kati ya Bahrain na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3473276    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/19

TEHRAN (IQNA) - Asilimia 95 ya wananchi wa Bahrain wanapinga hatua ya utawala wa kifalme nchini humo kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel.
Habari ID: 3473272    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/18

Uchaguzi wa rais Marekani 2020
TEHRAN (IQNA) – Mgombea kiti cha urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Democratic, Joe Biden amesema atawateua Waislamu nchini humo katika ngazi zote za kijamii na kisiasa za serikali yake endapo atashinda katika uchaguzi.
Habari ID: 3473269    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/17

TEHRAN (IQNA)- Waislamu nchini Pakistan wamependekeza kuwa siku ya kukumbuka kuzaliwa Mtume Muhammad SAW, ambayo ni maarufu kama Maulid, iadhmishwe pia kama ‘Siku ya Kimataifa ya Rehema”.
Habari ID: 3473266    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/16

TEHRAN (IQNA) – Balozi wa Misri nchini Mauritius amewatunuku wakuu wa jumuiya mbali mbali za Kiislamu Mauritius nakala za Qur’ani ambazo zina tarjama ya lugha mbali mbali.
Habari ID: 3473264    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/16

TEHRAN (IQNA) – Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau amesema chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia) pamoja na misimamo mikali ya mrengo ya kulia ni itikadi ambazo hazina nafasi yoyote katika jamii ya Canada.
Habari ID: 3473260    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/14

TEHRAN (IQNA) – Saudi Arabia imeshindwa kujiunga na Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kufuatia pingamizi la shirika moja la kimataifa.
Habari ID: 3473258    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/14

TEHRAN (IQNA) – Mtaalamu maarufu wa kisiasa Kuwaita amelaani hatua ya baadhi ya nchi za Kiarabu kuanzisha uhusiano kamili wa kidiplomasia na Israel na kutaja hatua hiyo kuwa sawa na ukoloni mamboleo.
Habari ID: 3473257    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/13

Wizara ya Hija na Umrah Saudia imetangaza kuwa watu 250,000 wataruhusiwa kushiriki katika awamu ya pili ya Ibada ya Umrah ikiwa ni katika mpango wa kuanza hatua kwa hatua ibada hiyo.
Habari ID: 3473255    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/13

TEHRAN (IQNA)- Sheikh Ekrima Sa'id Sabri, Mkuu wa Baraza Kuu la Kiislamu katika mji wa Quds (Jerusalem) na khatibu katika Msikiti wa Al Aqsa mjini humo ametahadharisha kuhusu njama ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya kutaka kutwaa sehemu ya msikiti huo ambao ni qibla cha kwanza cha Waislamu.
Habari ID: 3473249    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/11