waislamu - Ukurasa 36

IQNA

TEHRAN (IQNA)- Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imetoa wito kwa Sri Lanka kuheshimu haki za Waislamu kuzikwa kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu.
Habari ID: 3473679    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/02/24

TEHRAN (IQNA) – Benki moja ya Kiislamu nchini Nigeria imezindua mpango wa kuwahimiza Waislamu kuweka akiba ya fedha za kutumika kwa ajili ya kutekeleza Ibada ya Hija ambayo ni katika nguzo za Uislamu.
Habari ID: 3473677    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/02/23

TEHRAN (IQNA)- Wanafunzi zaidi ya 185 wa Qur'ani Tukufu kutoka mikoa 26 ya Algeria ambao wamefanikiwa kuhifadhi Qur'ani katika mafunzo yaliyotolewa kwa njia ya intaneti wameenziwa katika sherehe iliyofanyika mjini Oran, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Habari ID: 3473676    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/02/23

Mkuu wa Kongamano la Kimataifa la Wauyghur katika mahojiano na IQNA
TEHRAN (IQNA) - Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kimataifa ya Jamii ya Uyghur Dolkun Isa anasema serikali ya China inaendeleza kampeni dhidi ya Waislamu wa jamii ya Uyghur kwa kisingizio cha kupambana na misimamo mikali ya kidini.
Habari ID: 3473671    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/02/21

TEHRAN (IQNA) – Idadi ya Waislamu wanaoishi nchini Japan, ingawa ni ndogo, imeongezeka maradufu katika muongo moja uliopita kutoka 110,000 mwaka 2010 hadi 230,000 mwishoni mwa mwaka 2019.
Habari ID: 3473661    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/02/18

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei ameashiria hotuba yake ya hivi karibuni kuhusiana na makubaliano ya nyuklia ya JCPOA baina ya Iran na nchi tano za kundi la 5+1 na kusema kuwa: Iwapo upande mwingine utatekeleza makubaliano hayo, Iran pia itatekeleza vipengee vyake, na mara hii Jamhuri ya Kiislamu haitatosheka kwa maneno na ahadi tupu.
Habari ID: 3473659    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/02/17

TEHRAN (IQNA) – Kituo cha Kiislamu cha Utamaduni cha New York kinajumuisha pia msikiti na kipo katika mtaa wa Harlem, Manhattan mjini New York nchini Marekani.
Habari ID: 3473656    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/02/16

TEHRAN (IQNA)- Algeria imefungua misikiti yote nchini humo baada kwa ajili ya sala za jamaa za kila siku na Sala ya Ijumaa.
Habari ID: 3473655    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/02/16

TEHRAN (IQNA)- Mwenedo wa chuki dhidi ya Uislamu barani Ulaya hususan nchini Ufaransa ungali unaendelea ambapo Waislamu wa nchi hiyo wamekuwa wakikabiliwa na mashinikizo makubwa.
Habari ID: 3473652    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/02/15

TEHRAN (IQNA) – Misikiti mingine 8 imefungwa kwa muda maeneo mbali mbali ya Saudia kufuatia ongezeko la maambukizi ya COVID-19 nchini humo.
Habari ID: 3473649    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/02/14

TEHRAN (IQNA) – Vladimir Gushchin mtafiti katika Kituo cha Utafiti wa Gamaleya nchini Russia ambayo imetengenza chanjo ya Corona ya Sputnik V amesema chanjo hiyo ni halali kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu.
Habari ID: 3473643    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/02/12

THERAN (IQNA)- Mwakilishi wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Asarullah ya Yemen amesisitiza kuwa, Utawala wa Aal Saud unatumia viwanja vya ndege vya Saudia kutekeleza mashambulizi dhidi ya Yemen na kuyatahadharisha mashirika ya ndege kutotumia viwanja hivyo.
Habari ID: 3473642    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/02/11

TEHRAN (IQNA) – Waislamu nchini Sri Lanka wamewasilisha malalamiko kwa Kamati ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa kuhusu sera ya serikali yao ya kuchoma kwa lazima miili ya Waislamu wanaoshukiwa kupoteza maisha kutokana na corona au COVID 19.
Habari ID: 3473636    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/02/09

TEHRAN (IQNA) – Zaidi ya hujuma 900 zimeripotiwa dhidi ya Waislamu na taasisi za Kiislamu kote Ujerumani katika mwaka wa 2020.
Habari ID: 3473630    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/02/08

TEHRAN (IQNA)- Wanawake wawili Waislamu waliokuwa wamevaa hijabu walihujumiwa sehemu mbili tafauti Jumatano mjini Edmonton Canada.
Habari ID: 3473628    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/02/06

TEHRAN (IQNA) – Wizara ya Wakfu ya na Masuala ya Kidini Algeria imesema misikiti nchini humo ambayo ilifungwa kutokana na janga la COVID-19 sasa imeanza kutayarishwa kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Habari ID: 3473627    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/02/06

TEHRAN (IQNA) Wanawake Waislamu nchini Nigeria wamemtaka rais wa nchi hiyo Muhammadu Buhari na magavana wa majimbo watunge sheria za kuwaadhibu wale wanaowabagua wanawake Waislamu kwa sababu tu wamevaa Hijabu.
Habari ID: 3473624    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/02/05

TEHRAN (IQNA)- Msikiti unaoaminika kuwa mdogo zaidi duniani unaojulikana kama Masjid Mir Mahmood Shah au Jinn ki Masjid huko Hyderbad nchini India unahitaji ukarabati wa dharura.
Habari ID: 3473623    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/02/05

TEHRAN (IQNA) - Sera za chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu Ufaransa zimechukua mwelekeo mpya baada ya serikali kuanza kufunga maduka ya Waislamu kwa visingizio mbali mbali vya 'kisheria'.
Habari ID: 3473619    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/02/04

TEHRAN (IQNA) - Jeshi la Myanmar lilivyofanya mapinduzi na kutwaa madaraka ya nchi limetangaza kuwa, lina mpango wa kumfungulia mashtaka ya uhaini Aung San Suu Kyi kiongozi wa chama tawala cha nchi hiyo cha NLD na viongozi wengine kadhaa wa nchi hiyo.
Habari ID: 3473618    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/02/03