waislamu - Ukurasa 40

IQNA

TEHRAN (IQNA)- Ikiwa ni katika kuendeleza kampeni dhidi asasi za Kiislamu, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa Gerald Darminian ametangaza mpango wa kupiga marufuku Taasisi ya Kupambana na Chuki Dhidi ya Uislamu au Islamophobia Ufaransa (CCIF).
Habari ID: 3473378    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/11/20

TEHRAN (IQNA) – Jumba la Makumbusho la Sanaa za Kiislamu Cairo, Misri ni hifadhi kubwa zaidi ya athari za sanaa za Kiislamu duniani.
Habari ID: 3473375    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/11/19

TEHRAN (IQNA) – Mahakama nchini Sweden imeondoa marufuku ya vazi la Kiislamu la Hijabu katika shule za mji mmoja wa kaskazini mwa nchi hiyo ya bara Ulaya.
Habari ID: 3473371    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/11/18

TEHRAN (IQNA) – Qarii mashuhuri wa Misri Sheikh Mustafa Ghalwash katika moja ya safari zake nchini Iran alisoma Qur’ani Tukufu mbele ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Habari ID: 3473369    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/11/17

TEHRAN (IQNA)- Polisi nchini Austrai wamekosolewa vikali kwa kuwasumbua na kuwakera Waislamu ambao wamekuwa wakihujumu maeneo yao na kuwauliza maswali ya dharau.
Habari ID: 3473368    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/11/17

TEHRAN (IQNA) – Wanachama Waislamu katika chama cha Leba cha Uingereza wamesema wameshuhudia chuki dhidi ya Uislamu katika chama hicho kikubwa zaidi Uingereza.
Habari ID: 3473362    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/11/15

TEHRAN (IQNA)- Malefu ya Wapalestina wameshiriki katika Swala ya Ijumaa wiki hii katika Msikiti wa Al Aqsa ulio katika mji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na Israel.
Habari ID: 3473360    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/11/14

TEHRAN (IQNA)- Waendesha mashtaka nchini Ujerumani wamewafikisha kizimbani wanaume 10 wanachama wa mrengo wa kulia wa kibaguzi ambao walikuwa wanapanga kutekeleza hujuma dhidi ya Waislamu na kuipindua serikali ya Ujerumani.
Habari ID: 3473359    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/11/14

TEHRAN (IQNA) - Swala ya kwanza ya Ijumaa baada ya miaka 28 imeswaliwa leo katika msikiti wa kihistoria Yukhari Govhar Agha katika mji wa Shusha eneo linalozozaniwa baina ya Jamhuri ya Azeribajan na Armenia la Nagorno-Karabakh.
Habari ID: 3473357    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/11/13

TEHRAN (IQNA) – Sauti ya adhana imesikika baada ya miaka 28 katika msikiti wa kihistoria Yukhari Govhar Agha katika mji wa Shusha ulioko eneo linalozozaniwa baina ya Jamhuri ya Azeribajan na Armenia la Nagorno-Karabakh.
Habari ID: 3473354    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/11/12

TEHRAN (IQNA)- Msikiti katika mji wa Zaandam kaskazini magharibi mwa Indonesia umehujumiwa katika jinai ambayo imetajwa kuwa ya wenye chuki dhidi ya Uislamu.
Habari ID: 3473350    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/11/11

Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imetoa taarifa ikilaani uhalifu unaoendelea kufanywa na jeshi la utawala haramu wa Israel wa kubomoa nyumba na taasisi za Wapalestina katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.
Habari ID: 3473346    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/11/10

TEHRAN (IQNA) - Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa amedai kuwa Paris inaheshimu dini ya Uislamu na kwamba Waislamu ni sehemu ya jamii ya Ufaransa.
Habari ID: 3473343    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/11/09

TEHRAN (IQNA) – Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameelezea matumaini yake kuwa uchaguzi mkuu wa Novemba 8 nchini Myanmar utaandaa mazingira ya kurejea nyumbani mamia ya maelefu ya wakimbizi Waislamu wa jamii ya Rohingya.
Habari ID: 3473338    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/11/07

TEHRAN (IQNA)- Wasomi, wanafikra, wanaharakati na wanazuoni wa Kiislamu duniani wametoa wito wa kutungwa sheria zinazozuia kuvunjiwa heshima Mitume wa Mwenyezi Mungu, dini za mbinguni na wafuasi wake.
Habari ID: 3473331    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/11/05

TEHRAN (IQNA)- Msikiti wa kwanza katika mji mkuu wa Ugiriki, Athens umefunguliwa baada ya miaka 14 ya vuta nikuvute na urasimu kupita kiasi.
Habari ID: 3473329    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/11/04

TEHRAN (IQNA) - Wimbi kali la maandamano ya kulaani matamshi yaliyotolewa na Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa akitetea matusi na kuvunjiwa heshima Mtume Muhammad SAW Nchini humo limeendelea kushuhudiwa katika pembe mbalimbali za dunia.
Habari ID: 3473325    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/11/03

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika Hotuba ya Miladj un Nabii SAW
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amezungumzia siasa za kimantiki za kusimama kidete kukabiiliana na sera za kibabe za Marekani na kusema kuwa, sera zenye mahesabu za Jamhuri ya Kiislamu hazibadiliki kwa kuondoka kiongozi na kuja mwingine madarakani huko Marekani.
Habari ID: 3473323    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/11/03

TEHRAN (IQNA)- Serikali ya Saudi Arabia imewaruhusu waislamu wanaoishi nje ya ufalme huo kuingia nchini humo kwa ajili ya kutekeleza ibada ya Umra baada ya kufungwa mwezi Machi mwaka huu kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.
Habari ID: 3473317    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/11/01

Kiongozi wa Ansarullah
TEHRAN (IQNA)-Katibu Mkuu wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema rais Emmanuel Macron wa Ufaranmsa ni kikaragosi kinachochezeshwa na Wazayuni kichukue hatua za kuutusi na kuuvunjia heshima Uislamu.
Habari ID: 3473309    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/30