TEHRAN (IQNA) – Kama ilivyokuwa katika miaka iliyotangulia, Haram Takatifu ya Imam Ridha AS, Imam wa Nane wa Waislamu wa Madhehebu ya Shia, imepambwa kwa munasaba wa kukumbuka siku aliyozaliwa mtukufu huyo.
Habari ID: 3472917 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/07/01
TEHRAN (IQNA) – Sherehe inayojulikana kama Ajvatovica imefanyika nchini Bosnia na Herzegovina kuadhimsiha mwaka 510 tokea Uislamu uingie nchini humo.
Habari ID: 3472916 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/06/30
TEHRAN (IQNA) - Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa Maulamaa wa Kiislamu (IUMS) ametahadharisha kuhusu njama hatari inayopangwa dhidi ya Yemen na ametaka nchi hiyo inusuriwe.
Habari ID: 3472911 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/06/29
TEHRAN (IQNA) - Misikiti kote Misri inafunguliwa tena kuanzia Juni 27 lakini kwa kuzingatia masharti makali ya kiafya ili kuzuia kuenea ugonjwa wa COVID-19 au corona.
Habari ID: 3472901 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/06/26
TEHRAN (IQNA) – Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani amepongeza uamuzi wa Saudi Arabia wa kupunguza kabisa idadi ya mahujaji na kuwazuia mahujaji wa kimataifa kuingia nchini humo.
Habari ID: 3472897 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/06/25
TEHRAN (IQNA) – Waislamu nchini Australia wameingia na hofu ya kuenea chuki dhidi ya Uislamu baada ya ripoti mpya kubaini kuwa maambukizi mapya ya COVID-19 mjini Melbourne yalianzia katika mjumuiko wa kifamilia wa sherehe za Idul Fitr.
Habari ID: 3472896 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/06/25
TEHRAN (IQNA) – Kituo cha Kiislamu cha Al Azhar nchini Misri kimelaani matamshi ya mwanasiasa wa mrengo wa kulia wa Austria ambaye alivunjia heshima Qur’ani Tukufu.
Habari ID: 3472881 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/06/20
TEHRAN (IQNA)- Mpango wa kila mwaka wa kuwaalika wasiokuwa Waislamu kutembelea misikiti nchini Uingereza mwaka huu umefutwa kutokana na kuibuka ugonjwa wa COVID-19 lakini pamoja na hayo kumezinduliwa mpango wa kutembelea misikiti kupitia intaneti.
Habari ID: 3472877 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/06/18
TEHRAN (IQNA) – Misikiti zaidi itafunguliwa Mayalsia kwa ajili ya swala ya Ijumaa na watakashiriki katika swala watatakiwa kuzingatia sheria za kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19 au corona.
Habari ID: 3472876 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/06/18
Siku kama ya leo miaka 1293 iliyopita Imam Ja'far Sadiq (AS) mmoja kati ya wajukuu wa Mtume Mtukufu Muhammad (SAW), aliuawa shahidi kwa amri ya mtawala dhalimu wa Kiabbasi, Mansur al Dawaniqi.
Habari ID: 3472873 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/06/17
TEHRAN (IQNA)- Mashirika ya Waislamu nchini Marekani yamejiunga na wimbi la malalamiko ya kuishinikiza serikali ya nchi hiyo ifanye mageuzi haraka iwezekanavyo kwa ajili ya kuondoa ubaguzi wa rangi wa kimfumo katika muundo wa polisi ya nchi hiyo.
Habari ID: 3472871 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/06/16
TEHRAN (IQNA)- Mashirika ya kutetea haki za binadamu yamemjia juu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres kwa kuuondoa muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia katika orodha ya makundi yanayokanyaga haki za watoto.
Habari ID: 3472870 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/06/16
TEHRAN (IQNA)- Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki amesema mfumo wa kifedha wa Kiislamu unaweza kutumika kuiondoa dunia katika mgogoro wa kiuchumi uliosababishwa na janga la COVID-19.
Habari ID: 3472866 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/06/15
TEHRAN (IQNA) – Gaidi aliyeuhujumu msikiti nchini Norway amehukumiwa kifungo cha miaka 21 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumuua dada yake wa kambo na kufyatua risasi ndani ya msikiti mjini Oslo, mwezi Agosti mwaka jana.
Habari ID: 3472856 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/06/11
TEHRAN (IQNA) – Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon Sayyed Hassan Nasrallah ametuma salamu za rambi rambi kufuatia kifo cha Katibu Mkuu wa zamani wa Harakati ya Jihadi Islami ya Palestina Ramadan Abdullah Shalah.
Habari ID: 3472849 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/06/09
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi wa Harakati ya Al-Sadr ya nchini Iraq ameitaka Marekani iviondoe mara moja vikosi vyake vyote katika ardhi ya nchi hiyo ya Kiarabu.
Habari ID: 3472848 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/06/09
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa mkono wa pole kufuatia kuaga dunia Katibu Mkuu wa zamani wa Harakati ya Jihadu Islami ya Palestina, Ramadhan Abdullah Shalah.
Habari ID: 3472847 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/06/08
TEHRAN (IQNA) -Katibu Mkuu wa zamani Harakati ya Jihad Islami ya Palestina ameaga dunia hospitalini baada ya kusumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu.
Habari ID: 3472844 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/06/07
TEHRAN (IQNA) – Kamati ya Hija ya India imesema Waislamu nchini humo hawataweza kusafiri hadi mji wa Makka, Saudi Arabia kutekeleza ibada ya Hija kutokana na janga la COVID-19 au corona.
Habari ID: 3472842 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/06/06
TEHRAN (IQNA) –Misikiti katika mji mkuu wa Indonesia, Jakarta, imefunguliwa Ijumaa kwa mara ya kwanza baada ya takribani miezi mitatu, huku nchi hiyo ikianza zuio ambalo limekuwepo ili kupunguza kasi ya kuenea ugonjwa wa COVID-19 au corona.
Habari ID: 3472838 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/06/05