iqna

IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema, kuwasha moto wa vita katika nchi kadhaa ikiwemo Afghanistan, Iraq na Syria ni miongoni mwa sababu za kuchukiwa Marekani na akabainisha kwamba, Wamarekani wanaeleza kinagaubaga kuwa 'tumeweka vikosi Syria kwa sababu kuna mafuta'; lakini bila shaka hawataweza kubaki, si Iraq wala Syria. Ni lazima waondoke huko na hakuna shaka kuwa wataondoshwa tu.
Habari ID: 3472777    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/18

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Siku ya Kimataifa ya Quds itaadhimishwa nchini Iran na pia Swala ya Idul FItr itaswaliwa kwa kuzingatia kanuni za afya kuhusiana na ugonjwa wa COVID-19.
Habari ID: 3472770    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/16

TEHRAN (IQNA) – Tokea mwaka 1975, Wakristo nchini Misri wamekuwa wakiwatayarishia Waislamu futari katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Habari ID: 3472769    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/15

TEHRAN (IQNA) - Wizara ya Mambo ya Nje Iran imetoa tamko kuhusu siku ya "Nakba" yaani siku ya nakama ya kuasisiwa utawala pandikizi wa Kizayuni katika ardhi walizoporwa Wapalestina na kusisitiza kuwa, kadhia ya Palestina itaendelea kuwa suala kuu nambari moja katika ulimwengu wa Kiislamu licha ya kufanyika njama nyingi za kulisahaulisha.
Habari ID: 3472767    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/15

TEHRAN (IQNA) – Misikiti nchini Italia itaendelea kufungwa wakati wa Sala ya Idul Fitri ikiwa ni katika muendelezo wa kuzuia kuenea ugonjwa wa COVID-19.
Habari ID: 3472765    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/14

TEHRAN (IQNA) – Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni mwezi wa Ibada ambao huwajumuisha Waislamu kwa lengo moja.
Habari ID: 3472764    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/14

TEHRAN (IQNA) – Misikiti ya London Mashariki nchini Uingereza imeanza kuadhini kupitia vipaza sauti katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ili kuwasaidia Waislamu wajihisi kufungamana na misikiti ambayo imefungwa kwa muda kuzuia kuenea ugonjwa wa COVID-19.
Habari ID: 3472752    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/10

TEHRAN (IQNA) – Misikiti nchini Ujerumani imefunguliwa Jumamosi baada ya kufungwa kwa muda wa miezi miwili kutokana na janga la ugonjwa wa COVID-19 au corona.
Habari ID: 3472751    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/10

TEHRAN (IQNA) – Misikiti 37 nchini Singapore imeungana na kuchanga dola laki sita kwa ajili ya kutoa futari kwa Waislamu wanaofunga saumu ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Habari ID: 3472749    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/09

TEHRAN (IQNA) – Duru ya 28 ya Maonyesho ya Kimataifa ya Qur’ani ya Tehran itafanyika kwa njia ya intaneti.
Habari ID: 3472748    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/09

TEHRAN (IQNA) – Taasisi ya Kiislamu ya Dar Al-Hijrah ya Virginia nchini Marekani inagawa chakula kwa wanaohitajia katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Habari ID: 3472747    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/08

TEHRAN (IQNA) – Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema janga la COVID-19 au corona limeibua 'tsunami ya chuki' na hivyo ametoa wito wa kusitishwa matamshi yaliyojaa chuki duniani.
Habari ID: 3472746    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/08

TEHRAN (IQNA) - Jumuiya ya Misikiti Ufaransa (UMF) imetoa wito kwa Waislamu nchini humo kuswali na kusherehekea Idul Fitr majumbani mwao ili kuzuia kuenea ugonjwa wa COVID-19.
Habari ID: 3472744    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/08

TEHRAN (IQNA) – Waislamu Korea Kusini wameamua kufungua misikiti yao Jumatano baada ya nchi hiyo kutoripoti maambukizi mapya ya corona au COVID-19 kwa siku ya tatu mfululizo.
Habari ID: 3472736    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/05

TEHRAN (IQNA) – Mesut Ozil mchezaji soka mashuhuri wa timu ya Arsenal katika Ligi ya Premier ya England ametoa mchango wa dola laki moja za Kimarekani kuwasaidia Waislamu ambao wameathiriwa vibaya na janga la COVID-19 au corona katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Habari ID: 3472730    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/03

TEHRAN (IQNA) – Asasi za Kiislamu mjini New York nchini Marekani zimeungana na kuanzisha mpango wa kugawa futari kwa wasiojiweza katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Habari ID: 3472726    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/02

TEHRAN (IQNA) – Waislamu nchini Canada wamepata fursa ya kusikia adhana misikitini kupitia vipaza sauti kwa mara ya kwanza kabisa katika historia ya nchi hiyo ya Amerika Kaskazini.
Habari ID: 3472720    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/01

TEHRAN (IQNA) – Chama tawala nchini India, Bharatiya Janata (BJP), kimetoa wito wa umoja na maelewano ya kidini baada ya malalamiko ya kimataifa kufuatia ongezeko la chuki dhidi ya Uislamu nchini humo.
Habari ID: 3472719    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/04/30

TEHRAN (IQNA) -Sayyed Abbas Mousawi, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesisitiza kuwa njia pekee ya kurejesha uthabiti na utulivu Yemen ni umoja na mshikamano miongoni mwa makundi mbali mbali nchini humo.
Habari ID: 3472717    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/04/30

TEHRAN (IQNA) - Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambayo hufanyika kwa njia ya moja kwa moja kupitia Televisheni ya Al Kauthar ya Iran yameanza.
Habari ID: 3472714    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/04/29