IQNA

10:48 - August 09, 2020
News ID: 3473048
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi wa harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema, kujiweka mbali Waislamu na Uwalii wa Umma ndio sababu kuu ya matatizo uliyonayo Umma wa Kiislamu.

Sayyid Abdul-Malik Badreddin al-Houthi, aliyasema hayo jana Jumamosi katika hotuba kwa mnasaba wa Idi tukufu ya Ghadir Khum na kubainisha kwamba, kuna matatizo mengi katika Ulimwengu wa Kiislamu na wa Kiarabu na kwamba kuna baadhi wanaodhani kuwa, ufumbuzi wa matatizo uko mikononi mwa Marekani na Israel; lakini inapasa Waislamu wote watambue kwamba Marekani na utawala wa Kizayuni wao ndio wasababishaji wakuu wa matatizo katika eneo.

Katibu Mkuu wa Ansarullah ya Yemen amesema, kujiweka mbali na mafundisho ya Mwenyezi Mungu ndiko kulikosababisha maajinabi kuingilia masuala ya Umma wa Kiislamu na kuyaweka chini ya udhibiti wao; na akaongeza kuwa, mambo hayo yamesababisha kuwepo hali mbaya na ngumu katika nchi za Kiislamu.

Sayyid Abdul-Malik al-Houthi amesisitiza kuwa, msingi wa Uwalii wa Umma ndio unaodhamini mwendelezo wa njia ya Mwenyezi Mungu na kuziba mpasuko ili kuweza kukabiliana na uchokozi wa maadui wa Umma wa Kiislamu.

Jana Jumamosi tarehe 18 Mfunguo Tatu Dhil-Hijjah mwaka 1441 Hijria iliyosadifiana na tarehe 8 Agosti 2020 Miladia ilikuwa siku ya Idi ya Ghadir Khum, ambayo ni moja ya Sikukuu kubwa za Waislamu.

Ghadir Khum ni jina la mahali paliko baina ya Makka na Madina, ambako wakati Bwana Mtume Muhammad SAW alipokuwa akirudi Madina baada ya Hijjatul-Wida'a alimtangaza na kumtambulisha rasmi Imam Ali AS, Imam wa Kwanza wa Waislamu wa Kishia, kuwa ndiye atakayekuwa "Walii wa Umma" baada yake.

3915425

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: