ukanda wa gaza - Ukurasa 6

IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu Uingereza
IQNA - Idadi kubwa ya matukio ya chuki dhidi ya Waislamu na Uislamu yameripotiwa nchini Uingereza tangu kuanza kwa vita vya mauaji ya kimbari vya Israel dhidi ya Gaza, kulingana na kundi linalofuatilia visa kama hivyo.
Habari ID: 3478403    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/23

Indhari
IQNA-Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema utawala wa Israel "utalipa kwa damu" gharama ya mauaji ya hivi karibuni ya raia kusini mwa nchi hiyo, akisisitiza kwamba mauaji hayo hayawezi kuifanya harakati hiyo kuacha kuwaunga mkono Wapalestina katika Ukanda wa Gaza unaozingirwa.
Habari ID: 3478364    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/17

Jinai za Israel
IQNA-Mkuu wa Kitengo cha Asia Magharibi katika Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa amesema: Idadi ya raia na waandishi wa habari waliouawa huko Gaza haina mfano.
Habari ID: 3478363    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/16

Watetezi wa Palestina
IQNA - Hatua za kivita za utawala wa Israel huko Rafah "zinathibitisha" usahihi wa kesi ya mauaji ya kimbari dhidi ya utawala huo katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini amesema.
Habari ID: 3478356    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/15

Kadhi ya Palestina
IQNA-Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imelaani mashambulizi yanayoendelea kufanywa na jeshi katili la Israel dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza na upanuzi wa mashambulizi ya kiholela ya utawala huo kwenye mji wa Rafah, kusini mwa ukanda huo.
Habari ID: 3478355    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/15

Watetezi wa Palestina
IQNA - Siku ya pili ya Kimataifa ya Hatua kwa Ajili ya Gaza itaadhimishwa baadaye mwezi huu kwa maandamano ya mshikamano na watu wa Ukanda wa Gaza.
Habari ID: 3478312    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/06

Watetezi wa Palestina
IQNA - Maandamano yalifanyika mjini Brussels siku ya Jumatatu kupinga jinai ya Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza ikiwa ni pamoja na mauaji ya waandishi wa habari.
Habari ID: 3478311    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/06

Ulimwengu wa Kiislamu
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, anasema wasomi wa Ulimwengu wa Kiislamu wanabeba dhima nzito kuhusiana na matukio yanayojiri huko Gaza na kwamba wanapaswa kuanzisha matakwa ya umma ya kukata uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3478310    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/05

Waislamu Marekani
IQNA - Polisi wameimarisha doria katika nyumba za ibada na "vituo vikuu vya miundombinu" huko Dearborn, jimbo la Michigan nchini Marekani.
Habari ID: 3478304    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/04

Watetezi wa Palestina
IQNA - Watu katika nchi kadhaa za Ulaya walifanya maandamano siku ya Jumamosi kutoa sauti ya mshikamano na watu wa Palestina na kutoa wito wa kusitishwa mara moja kwa vita vya Israel dhidi ya Gaza.
Habari ID: 3478303    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/04

Watetezi wa Palestina
IQNA - Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon amepongeza uungaji mkono wa Iran kwa harakati za muqawama au mapambano ya Kiislamu na kusema uungaji mkono huo unafanyika bila ya kutarajia chochote mkabala wa uungaji mkono huo.
Habari ID: 3478295    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/03

Watetezi wa Qur'ani
IQNA - Washiriki wa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani huko Port Said, Misri, walifanya maandamano ya kuwaunga mkono Wapalestina wanaodhulumiwa wa Gaza.
Habari ID: 3478294    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/03

Mtazamo
IQNA- Ikiwa imepita miezi minne ya mashambulizi ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Gaza, utawala huo umeshindwa kufikia lengo la kuangamiza Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, na pia haujaweza kuvunja azma na irada ya wakazi wa eneo hilo. Hivyo ili kujaribu kufidia kufeli huko, Wazayuni wakishirikiana na baadhi ya waitifaki wao wa Magharibi, sasa wanalenga kusambaratisha Shirika la Umoja wa Mataifa la Msaada kwa Wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA.
Habari ID: 3478288    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/01

Jinai za Israel
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa WHO, Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema katika chapisho la ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X jana Jumapili kwamba kukata ufadhili kwa UNRWA "kutawaumiza tu watu wa Gaza".
Habari ID: 3478278    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/01/30

Watetezi wa Palestina
IQNA - Mamia ya watu walikusanyika katika Kituo cha Kiislamu cha Maine siku ya Jumapili kuwaandikia barua wawakilishi wao, wakiwataka kuunga mkono takwa la kuutaka utawala wa Kizayuni wa Israel usitisha vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina wa Gaza. Wapalestina wasiopungua 26,000 wameuawa shahidi tangua utawala wa Israel uanzishe vita dhidi ya Gaza Oktoba mwaka jana.
Habari ID: 3478273    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/01/29

Jinai za Israel
IQNA - Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi la Palestina UNRWA amesema kuwa uamuzi wa baadhi ya nchi za Magharibi kusitisha misaada ya kifedha kwa shirika hilo ni sawa na "adhabu ya pamoja" ambayo itapunguza misaada ya kuokoa maisha kwa watu milioni mbili huko Gaza.
Habari ID: 3478265    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/01/28

Kadhia ya Palestina
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa: Nchi za Kiislamu zinapaswa kukata uhusiano wao wa kisiasa na kiuchumi na utawala wa Kizayuni kwa kukata mishipa muhimu ya uhai ya utawala huo ghasibu.
Habari ID: 3478242    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/01/23

Jinai za Israel
IQNA-Ripota wa Umoja wa Mataifa anasema utawala wa Kizyuni wa Israel unatumia njaa kama silaha dhidi ya watu Wapalestina wa Gaza ambao wanakabiliwa na mgogoro mkubwa wa chakula baada ya miaka ya vikwazo na vita vya sasa vya maangamizi ya umati vinavyotekelezwa na Israel.
Habari ID: 3478241    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/01/23

Jinai za Israel
IQNA - Wapiga kura wa Marekani wamehimizwa kuandika "Sitisha Vita Gaza" kwenye kura zao wakati wa kuchagua wagombea wa uchaguzi wa rais wa mwezi Novemba ikiwa ni njia ya kubainisha malalamiko kuhusu jinsi Joe Biden alivyoshughulikia vita vya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Gaza.
Habari ID: 3478238    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/01/23

Jinai za Israel
IQNA-Wizara ya Wakfu na Masuala ya Dini katika Ukanda wa Gaza imesema mashambulizi ya vikosi vya utawala katili wa Israel dhidi ya eneo hilo lililozingirwa yamebomoa na kuharibu misikiti 1,000 tokea Oktoba 7 mwaka uliopita hadi sasa.
Habari ID: 3478234    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/01/22