chuki dhidi ya uislamu - Ukurasa 3

IQNA

IQNA – Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na Misimamo Mikali kimekemea vikali kitendo cha hivi karibuni cha kuchoma nakala ya Qur'ani kilichofanywa na mwanasiasa mmoja wa Marekani.
Habari ID: 3481147    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/28

IQNA – Kitendo cha kuivunjia heshima na kuteketeza moto nakala ya Qur’an ambacho kimetekelezwa mgombea wa kiti katika Bunge la Kongresila Marekani kwa tiketi ya chama cha kihafidhina cha Republican huko Texas, ambaye ni mfuasi wa Rais wa Marekani Donald Trump, kimeibua hasira kubwa.
Habari ID: 3481142    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/27

IQNA – Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar cha Kufuatilia na Kupambana na Misimamo Mikali kimelaani kitendo cha chuki kilichotokea hivi karibuni katika msikiti wa Oxford, nchini Uingereza na kuonya kwamba matendo ya aina hiyo huchochea uhasama na ni “tishio la moja kwa moja kwa mshikamano wa kijamii.”
Habari ID: 3481120    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/22

IQNA – Mamlaka za Ufaransa zimeanzisha uchunguzi kufuatia jaribio la kuchoma moto chumba cha kusalia cha Waislamu mjini Châtillon-sur-Seine, tukio ambalo maafisa wamelilaani kuwa ni kitendo cha kigaidi cha uoga na chenye chuki dhidi ya Uislamu.
Habari ID: 3481095    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/16

IQNA – Mwanamke mchanga Muislamu aliyevaa hijaab ameshambuliwa na kutishiwa maisha ndani ya basi la jiji la Ottawa, Canada eneo la Kanata, katika tukio linalochunguzwa na polisi kama uhalifu unaochochewa na chuki dhidi ya Uislamu.
Habari ID: 3481079    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/13

IQNA – Viongozi wa moja ya misikiti mikubwa zaidi nchini Australia wamesema wamepokea vitisho vya kuuwawa baada ya kutangazwa mpango wa kuweka vipaza sauti vipya kwa ajili ya adhana.
Habari ID: 3481059    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/09

IQNA-Australia imeingia katika kipindi kigumu cha chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia), hali iliyoibuka kwa kasi tangu kuanza kwa vita vya kikatili vya utawala wa Israel dhidi ya Gaza.
Habari ID: 3481020    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/30

IQNA – Baraza la Mahusiano ya Kiislamu ya Marekani (CAIR) limeitaka kampuni ya uwekezaji ya Sequoia Capital kumwondoa mshirika wake Shaun Maguire, kufuatia chapisho la mitandao ya kijamii lililokosolewa vikali kwa kuendeleza chuki dhidi ya Waislamu.
Habari ID: 3480934    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/12

IQNA – Polisi nchini Uingereza wameanzisha uchunguzi kupitia kamera za usalama (CCTV) kufuatia tukio lililoripotiwa la matusi ya maneno dhidi ya waumini nje ya msikiti ulioko Haverhill, Suffolk.
Habari ID: 3480931    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/12

IQNA – Utafiti mpya umeonesha ongezeko la chuki na chuki dhidi Uislamu (Islamofobia) dhidi ya wahudumu wa afya Waislamu nchini Australia, hali inayowaathiri kisaikolojia kwa kiwango kikubwa.
Habari ID: 3480925    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/11

IQNA-Miaka ishirini baada ya mashambulizi ya 7/7 mjini London, Waislamu wa Uingereza bado wanahisi athari za kihisia na kijamii.
Habari ID: 3480910    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/07

IQNA – Mwanamke Muislamu alishambuliwa kwa ukatili mahali pake pa kazi huko Oshawa, Ontario, Canada katika tukio ambalo viongozi wa jamii wanaitaka polisi kulichunguza kama jinai ya chuki.
Habari ID: 3480893    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/04

IQNA – Mamlaka za Ufaransa zimeripoti ongezeko la asilimia 75 la matukio ya chuki dhidi ya Waislamu katika miezi mitano ya kwanza ya mwaka 2025, huku mashambulizi dhidi ya watu binafsi yakiongezeka mara tatu ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.
Habari ID: 3480892    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/04

IQNA – Kufuatia mashambulizi ya hivi karibuni dhidi ya misikiti nchini Uingereza na Ufaransa, viongozi wa Ulaya wametakiwa kuacha kuchochea chuki dhidi ya Uislamu.
Habari ID: 3480880    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/01

IQNA – Ripoti mpya iliyotolewa Jumatatu imetoa wito kwa serikali ya Uingereza kuweka mkakati wa kitaifa wa pamoja kupambana na kuongezeka kwa cChuki Dhidi ya Uislamu (Islamophobia), ikionya kuwa mgawanyiko unaozidi katika jamii unadhoofisha imani ya wananchi kwa taasisi za umma na kutishia mshikamano wa kitaifa.
Habari ID: 3480819    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/06/10

IQNA – Jumuiya ya Waislamu Duniani (MWL) imekaribisha uamuzi wa mahakama ya Uingereza kumtia hatiani mtu aliyeteketeza moto nakala ya Qur’ani Tukufu mjini London. 
Habari ID: 3480807    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/06/08

IQNA – Malalamiko ya ukiukaji wa haki za kiraia yamewasilishwa kwa Idara ya Haki za Kiraia ya Jimbo la Michigan nchini Marekani dhidi ya tawi la Domino’s Pizza lililoko Waterford, kufuatia ripoti ya ubaguzi wa kidini na uharibifu wa chakula uliowalenga wanawake wawili Waislamu na watoto wao.
Habari ID: 3480803    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/06/07

IQNA – Serikali ya Ufaransa imeshutumiwa kwa kulenga shirika la Ulaya linalojitolea kupambana na chuki dhidi ya Uislamu.
Habari ID: 3480767    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/05/31

IQNA – Chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia) ni janga la kimataifa linaloathiri jamii nzima, si Waislamu pekee, alionya Abdulsamad Al-Yazidi, Mwenyekiti wa Kituo cha Kiislamu cha Ujerumani.
Habari ID: 3480753    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/05/28

IQNA – Mkutano wa kimataifa utakaofanyika Baku mnamo Mei 26–27 utawaleta pamoja wataalamu wa kimataifa ili kujadili changamoto inayoongezeka ya chuki dhidi ya Uislamu yaani Islamophobia.
Habari ID: 3480731    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/05/24