Chuki dhidi ya Uislamu
TEHRAN (IQNA) -Mkutano wa kimataifa kuhusu chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia) umefanyika nchini Qatar huku mmoja wa waandalizi wake akitoa wito kwa juhudi za pamoja za kukabiliana na ongezeko la chuki dhidi ya Uislamu na athari zake "haribifu".
Habari ID: 3477683 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/10/02
Chuki dhidi ya Uislamu
DOHA (IQNA) - Qatar itakuwa mwenyeji wa mkutano wa kimataifa wa kujadili kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia) kwa namna zote na kuchunguza sababu za kuongezeka kwa chuki hizo.
Habari ID: 3477663 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/09/28
Chuki dhidi ya Uislamu
AMSTERDAM (IQNA) –Rais wa taasisi kuu ya Kiislamu Uholanzi anasema chuki dhidi ya Uislamu inaweza kuonekana katika taasisi zote za serikali nchini humo.
Habari ID: 3477642 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/09/23
Waislamu Australia
CANBERRA (IQNA) – Sajili ya Vitendo vya Chuki Dhidi ya Uislamu Australia (IRA) imepongeza marufuku ya udhalilishaji kidini huko New South Wales.
Habari ID: 3477503 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/08/27
Chuki dhidi ya Uislamu
WASHINGTON, DC (IQNA) - Tishio la bomu lilitolewa dhidi ya Msikiti wa Mohammed (Masjid Muhammad), huko Washington, DC, wakati wa sala ya Ijumaa.
Habari ID: 3477462 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/08/19
Chuki dhidi ya Uislamu
STOCKHOLM (IQNA) - Polisi huko Gothenburg, Uswidi, wanachunguza kesi ya uhalifu wa chuki baada ya msikiti mmoja kupokea bahasha ya kutisha iliyokuwa na unga mweupe siku ya Ijumaa.
Habari ID: 3477460 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/08/19
Waislamu Ulaya
BERLIN (IQNA)-Mamilioni ya Waislamu nchini Ujerumani wana wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa wimbi la chuki dhidi ya Uislamu na hujuma na mashambulio dhidi ya misikiti nchini humo.
Habari ID: 3477456 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/08/18
Watetezi wa Qur'ani Tukufu
WASHINGTON, DC (IQNA) - Baraza la Chama cha Wanasheria wa Marekani (ABA), chombo kikubwa zaidi cha wanasheria nchini Marekani, kimepitisha azimio la kulaani chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia).
Habari ID: 3477413 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/08/10
Chuki dhidi ya Uislamu
LONDON (IQNA) - Matukio ya chuki dhidi ya Uislamu nchini Uingereza yameongezeka zaidi ya mara mbili katika muongo mmoja.
Habari ID: 3477312 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/07/20
Chuki dhidi ya Uislamu
BRUSSELS (IQNA) - Marion Lalisse, mratibu mpya wa Umoja wa Ulaya katika kupambana na chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia), alidai Alhamisi kuwa Umoja wa Ulaya una mipango mahususi ya kupambana na chuki dhidi ya Uislamu.
Habari ID: 3477283 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/07/14
Chuki dhidi ya Uislamu
ISLAMABAD (IQNA) - Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imehimizwa kubuni mikakati ya kukabiliana na chuki inayoongezeka dhidi ya Uislamu duniani kote.
Habari ID: 3477253 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/07/08
Chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia)
WASHINGTON, DC (IQNA)-Msikiti huko Portales, New Mexico, nchini Marekani umeharibiwa kwa mara ya nne katika kipindi cha siku 10 huku polisi wakipuuza hawajazingatia mashambulio hayo yanayorudiwa, ambayo ni pamoja na kuvunjia heshima Qur’ani Tukufu.
Habari ID: 3477249 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/07/07
Chuki dhidi ya Uislamu
MAKKA (IQNA) - Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) Jumatano ilitoa wito kwa nchi wanachama wake kufadhili utayarishaji wa vipindi vya radio, televisheni na vyombo vingine vya habari kwa lengo la kupambana na chuki dhidi ya Uislamu.
Habari ID: 3477246 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/07/06
Rasmus Paludan, mwanasiasa wa Denmark mwenye siasa kali za chuki dhidi ya Uislamu alipigwa marufuku kushiriki katika tamasha la kisiasa la Folkemodet katika kisiwa cha Bornholm.
Habari ID: 3477151 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/06/17
Chuki dhidi ya Waislamu
TEHRAN (IQNA) –Waislamu katika mji wa kati wa Ujerumani wa Goettingen wameeleza "wasiwasi" baada ya msikiti wao kupokea barua ya vitisho yenye nembo ya Kinazi ya Swastika na nembo nyinginezo za Wanazi mamboleo.
Habari ID: 3477047 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/05/26
Chuki dhidi ya Uislamu
TEHRAN (IQNA) – Mashambulizi mengi dhidi ya Waislamu yameripotiwa karibu na Toronto nchini Kanada (Canada) huku polisi wakikamata watu baada ya uchunguzi.
Habari ID: 3477015 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/05/19
Chuki dhidi ya Uislamu
TEHRAN (IQNA) – Chuki dhidi ya Uislamu imeongezeka mara tatu Marekani tokea hujuma za Septemba11 mwaka 2001 huku wanasiasa wakiitumia wakitumia chuki hiyo kuendeleza ajenda zao wenyewe, shirika la haki za kiraia la kutetea haki za Waislamu Marekani linasema.
Habari ID: 3476971 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/05/07
Chuki dhidi ya Uislamu
TEHRAN (IQNA)- Waziri wa Biashara wa Kanada, Mary Ng amelaani shambulio la chuki dhidi ya Uislamu lililolenga msikiti mmoja eneo la Markham, Ontario wakati mtu mmoja alipovunjia heshima nakala ya Qur'ani Tukufu na kujaribu kuwashambulia waumini kwa gari.
Habari ID: 3476842 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/10
Chuki dhidi ya Uislamu
TEHRAN (IQNA) – Mzee wa miaka 73 alivamiwa na majambazi watatu alipokuwa akielekea nyumbani baada ya kuswali kwenye msikiti mmoja katika mji wa Birmingham nchini Uingereza.
Habari ID: 3476790 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/03/31
Sera za Kigeni
TEHRAN (IQNA)- Ofisi ya Uwakilishi wa Kudumu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mashirika ya kimataifa yaliyo na makao makuu yao mjini New York Marekani, imeandika kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya kupambana na Chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia) kwamba: "Iran inasisitiza mshikamano wake kamili na wahanga wa mashambulio yanayochochewa na chuki dhidi ya Uislamu kote duniani."
Habari ID: 3476716 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/03/16