iqna

IQNA

IQNA – Uturuki imeutaka Umoja wa Mataifa (UM) kuteua mjumbe maalum wa kupambana na chuki dhidi ya Uislamu au Islamofobia, ikisisitiza haja inayoongezeka ya kukabiliana na kauli na vitendo vya chuki na ubaguzi dhidi ya Waislamu.
Habari ID: 3480264    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/02/25

IQNA-Idadi ya matukio na vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu nchini Uingereza iliongezeka kufikia kiwango cha juu zaidi mwaka 2024. Hayo ni kwa mujibu wa taarifa zilizokusanywa na shirika la ufuatiliaji la Tell MAMA, ambalo limesema vita vya Gaza "vimechochea kupita kiasi" masuala ya chuki dhidi ya Waislamu kwenye mitandao ya kijamii.
Habari ID: 3480241    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/02/19

Waislamu Marekani
IQNA - Kundi la kutetea haki za Waislamu Marekani limelitaka Baraza la Seneti kumkataa Peter Hegseth, mteule wa Donald Trump kuwa Waziri wa Ulinzi (Pentagon), kutokana na misimamo yake dhidi ya Uislamu.
Habari ID: 3479761    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/11/16

Chuki Dhidi ya Uislamu
IQNA - Msikiti wa Imam Ridha (AS) umeshambuliwa na kuteketezwa moto huko New Lynn, Auckland, nchini New Zealand kuharibiwa vibaya, huku jamii ya Waislamu ikishtushwa na tukio hilo.
Habari ID: 3479710    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/11/06

Chuki dhidi ya Waislamu Marekani
IQNA - Seneta wa Illinois Sara Feigenholtz anakabiliwa na ongezeko la wito wa kujiuzulu baada ya kutuma ujumbe wa chuki dhidi ya Uislamu kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii.
Habari ID: 3479686    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/11/02

Chuki dhidi ya Uislamu
IQNA-Uchunguzi mpya umebaini kuwepo 'ongezeko kubwa na lenye kutia wasiwasi" la ubaguzi wa rangi dhidi ya Waislamu barani Ulaya hasa baada ya utawala haramu wa Israel wa kuanzisha vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina wanaodhulumiwa katika Ukanda wa Gaza.
Habari ID: 3479641    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/10/25

Chuki dhidi ya Uislamu
IQNA - Rasmus Paludan mwanasiasa wa siasa kali za mrengo wa kulia wa Denmark na Uswidi ambaye aliivunjia heshima Qur'ani Tukufu ameshtakiwa kwa mara kadhaa nchini Uswidi (Sweden) ambapo sasa mekataa kufika mahakamani.
Habari ID: 3479599    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/10/15

Chuki dhidi ya Uislamu
IQNA – Ripoti ya Ofisi ya Mambo ya Ndani Uingereza imefichua ongezeko la karibu 40% ya vitendo vya chuki za kidini huwa zinawalenga Waislamu katika maeneo ya England na Wales.
Habari ID: 3479579    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/10/12

Chuki dhidi ya Uislamu
IQNA - Mwanaume mmoja wa eneo la New Jersey Marekani amekiri kutenda uhalifu wa chuki kwa kuharibu kituo cha wanafunzi wa Kiislamu katika Chuo Kikuu cha Rutgers mapema mwaka huu, maafisa walitangaza Alhamisi.
Habari ID: 3479575    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/10/11

Waislamu Uingereza
IQNA - Takriban mashirika 80 ya Kiislamu na viongozi wa jamii za Waislamu wametoa wito kwa serikali ya Uingereza kuchukua hatua madhubuti ili kukabiliana na ongezeko la chuki dhidi ya Uislamu nchini humo.
Habari ID: 3479352    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/08/30

Chuki dhidi ya Uislamu
IQNA - Mzee wa miaka 75 amepigwa risasi mara kadhaa nje ya msikiti wa Masjid An-Nur kaskazini mwa Minneapolis nchini Marekani siku ya Jumatatu jioni.
Habari ID: 3479309    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/08/21

Waislamu Uingereza
IQNA -Kuna wasiwasi unaoongezeka miongoni mwa Waislamu wa Uingereza kuhusu usalama wao baada ya ghasia za hivi majuzi nchini humo.
Habari ID: 3479295    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/08/18

Chuki dhidi ya Uislamu
IQNA - Mwanaume Myahudi, Izak Kadosh wa eneo la Brooklyn, Marekani anakabiliwa na mashtaka zaidi ya 40, ikiwa ni pamoja na jaribio la pili la mauaji na uhalifu wa chuki, kutokana na vitendo vyake vya chuki  dhidi ya jirani yake Muislamu, Ahmed Chebira.
Habari ID: 3479288    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/08/17

Waislamu Uingereza
IQNA - Mwanamume mmoja amerekodiwa kwenye video akirusha maneno ya chuki dhidi ya Uislamu na kumtemea mate dereva wa basi Muislamu mjini London huku kukiwa na ongezeko la ghasia dhidi ya Waislamu katika nchi hiyo ya Ulaya.
Habari ID: 3479249    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/08/09

Machafuko Uingereza
IQNA: Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza, Yvette Cooper, siku ya Jumatatu alibainisha chuki dhidi ya Uislamu kama kichocheo cha ghasia za hivi karibuni za wazungu wenye misimamo mikali wa mrengo wa kulia katika miji kadhaa, ambayo imesababisha uharibifu mkubwa na karibu watu 400 kukamatwa.
Habari ID: 3479237    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/08/06

Chuki dhidi ya Uislamu
IQNA – Tukio la Muislamu kudungwa kisu katika kituo cha treni cha Blundellsands & Crosby huko Liverpool limeacha jamii ya Waislamu wa jiji hilo katika mshtuko huku Waislamu kote Uingereza sasa wanahofia usalama wao huku kukiwa na maandamano ya magenge ya watu wenye misimamo mikali ya chuki ya mrengo wa kulia.
Habari ID: 3479222    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/08/03

Chuki dhidi ya Uislamu
IQNA - Vichwa vitatu vya nguruwe vimepatikana nje ya shule mbili na kituo cha vijana huko Rainham, Uingereza vikiambatana na maandishi ya chuki dhidi Uislamu.
Habari ID: 3479192    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/07/27

Waislamu Ujerumani
IQNA - Shirika moja lisilo la kiserikali la kimataifa lenye makao yake makuu nchini Iran limelaani vikali marufuku ya Ujerumani dhidi ya Kituo cha Kiislamu cha Hamburg (IZH) na kuitaja hatua hiyo kama ukiukaji wa wazi wa mikataba ya kimataifa, pamoja na haki za binadamu na uhuru wa dini, kujieleza na kukusanyika.
Habari ID: 3479191    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/07/27

Waislamu Ujerumani
IQNA- Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Ali Bagheri Kani amelaani vikali hatua ya polisi ya Ujerumani ya kupiga marufuku Kituo cha Kiislamu cha Hamburg (IZH) na asasi zake tanzu, na kusema kwamba hatua hiyo inakiuka kanuni za kimsingi za uhuru wa kuabudu.
Habari ID: 3479189    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/07/26

Chuki dhidi ya Uislamu
IQNA – Matukio ya chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia) yaliongezeka nchini Luxembourg mwaka jana, kulingana na utafiti uliofanywa na Luxembourg Observatoire de L'Islamophobie.
Habari ID: 3479181    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/07/25