iqna

IQNA

TEHRAN (IQNA)- Mkuu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Siku ya Kimataifa ya Quds ni nembo ya muqawama au mapambano katika Umma wa Kiislamu.
Habari ID: 3475180    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/04/28

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Amir- Abdollahian
TEHRAN (IQNA)- Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Utawala bandia wa Israel ni mkiukaji mkubwa wa haki za binadamu duniani huku akisisitiza kuwa kura ya maoni ni njia muafaka ya kuainisha mustakabali wa Palestina.
Habari ID: 3475179    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/04/28

TEHRAN (IQNA)- Balozi wa mwakilishi wa kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, kuna wajibu wa sheria za kimataifa kuulinda Msikiti wa al Aqsa ili kuzuia kutokea maafa yenye madhara makubwa.
Habari ID: 3475175    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/04/27

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, maadhimisho ya Siku ya Quds ni fursa ya kutangaza kuwa pamoja na wananchi madhulumu wa Palestina ambapo licha ya taifa hilo kudhulumiwa lakini limepata nguvu na kuwa imara.
Habari ID: 3475173    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/04/27

TEHRAN (IQNA) - Katika kampeni iliyoitwa 'Hands Off Al-Aqsa Mosque' (Achaneni na Msikiti wa Al Aqsa), Baraza la Ushauri la Malaysia la Mashirika ya Kiislamu (Mapim) na mashirika 43 yasiyo ya kiserikali (NGOs) yameonyesha mshikamano wao na Wa palestina .
Habari ID: 3475163    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/04/24

TEHRAN (IQNA)- Umoja wa Afrika umelaani hujuma za utawala haramu wa Israel dhidi ya Msikiti wa Al Aqsa mjini Quds (Jerusalem) na Ukanda wa Gaa sambamba na kusisitiza uungajo mkono wake kwa watu wa Palestina.
Habari ID: 3475160    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/04/23

TEHRAN (IQNA)- Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa: Hii leo, hatima ya Palestina itaamuliwa kwa matakwa na irada ya Mujahidina.
Habari ID: 3475159    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/04/23

TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa muda wa Sala ya Ijumaa ya hapa jijini Tehran amesisitizia wajibu wa kujitokeza kwa wingi wananchi wa Iran katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds ambayo ni Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani na kusema kuwa, maandamano hayo yanamtia kiwewe adui.
Habari ID: 3475153    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/04/22

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran
TEHRAN (IQNA)- Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian amesema undumakuwili na kimya cha baadhi ya serikali na duru za kimataifa ndio chanzo cha kupata ubavu Israel katika kuzidisha uvamizi dhidi ya Wa palestina na ukiukaji wa haki zao.
Habari ID: 3475148    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/04/21

TEHRAN (IQNA)- Maafisa wa usalama Saudi Arabia wamemkamata raia wa Palestina aliyekuwa akitekeleza ibada ya Umrah katika mji wa Mtakatifu wa Makka kwa sababu tu aliomba dua ya kukombolewa Msikiti wa Al Aqsa unaokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3475144    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/04/19

Uchambuzi
TEHRAN (IQNA)- Siku ya Ijumaa alfajiri, askari wa utawala haramu wa Israel waliwashambulia Wa palestina ndani ya Msikiti wa Al Aqsa mjini Quds (Jerusalem) ambapo zaidi ya waumini 160 wamejeruhiwa. Jinai hiyo imewapa Wa palestina irada ya kuimarisha mapambano yao dhidi ya adui Mzayuni mtenda jinai.
Habari ID: 3475134    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/04/17

TEHRAN (IQNA)- Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amefanya mazungumzo ya simu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini ambapo wamejadili masuala ya kieneo na kimataifa.
Habari ID: 3475130    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/04/15

TEHRAN (IQNA)- Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imelaani hujuma iliyofanywa na walowezi wa Kizayuni wakisaidiwa na askari wa Israel dhidi ya Msikiti wa al Aqsa.
Habari ID: 3475129    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/04/15

TEHRAN (IQNA)- Wanajeshi wa utawala haramu wa Israel mapema leo wameuvamia Msikiti wa Al Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) na kuwajeruhi waumini Wa palestina ikiwa ni katika muendelezo wa uchokozi unaotolezwa na utawala huo dhidi ya Wa palestina katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Habari ID: 3475128    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/04/15

TEHRAN (IQNA)- Makundi mbalimbali ya mapambano ya Palestina yameitisha kikao cha dharura mjini Ghaza kutokana na utawala wa Kizayuni wa Israel kushadidisha jinai na vitisho dhidi ya wananchi wa Palestina.
Habari ID: 3475123    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/04/13

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema licha ya sera na azma ya Marekani na washirika wake ya kutaka kulisambaratisha suala la Palestina, na kuifanya dunia isahau uwepo kwa taifa hilo, lakini kadhia ya Wa palestina ipo hai na inazidi kuimarika na kupata nguvu kila siku.
Habari ID: 3475120    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/04/13

Kiongozi wa Hizbullah
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon, Sayyid Hassan Nasrallah amesema kuwa, wananchi wa Palestina hawatashindwa katika mapambano yao ya ukombozi dhidi ya utawala ghasibu wa Israel.
Habari ID: 3475118    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/04/12

TEHRAN (IQNA)- Timu ya kitaifa ya Libya ya mchezo wa kushindana kwa vitara au fencing imejiondoa katika ‘Mashindano ya Dunia ya Fencing’ ili kujizuia kukutana na timu ya utawala haramu wa Israel.
Habari ID: 3475116    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/04/12

TEHRAN (IQNA)- Harakati za kupigania ukombozi wa Palestina za Hamas na Jihad ya Kiislamu zimelaani vikali jinai za hivi karibuni za wanajeshi wa utawala haramu wa Israel ambao wamewaua Wa palestina akiwemo mwanamke.
Habari ID: 3475114    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/04/11

TEHRAN (IQNA)- Waislamu na Wakristo wa Palestina wamekuwa wakishiriki katika mpango wa pamoja wa kuadhimisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Habari ID: 3475109    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/04/10