TEHRAN (IQNA)- Viongozi na makundi ya ukombozi wa Palestina wameutaka Umoja wa Afrika (AU) kufikiria upya uamuzi wa mwaka jana wa kuipa Israel hadhi ya kuwa mwangalizi katika umoja huo.
Habari ID: 3474894 Tarehe ya kuchapishwa : 2022/02/05
TEHRAN (IQNA)- Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limeutuhumu utawala wa Kizayuni wa Israel kuwa ni utawala wa baguzi wa rangi wa apartheid. Amnesty Internation inakuwa taasisi ya karibuni zaidi ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu kuitangaza Israel kuwa ni utawala wa apartheid.
Habari ID: 3474881 Tarehe ya kuchapishwa : 2022/02/02
Katika safari ya rais wa Israel nchini UAE
TEHRAN (IQNA)- Rais Isaac Herzog wa utawala haramu wa Israel jana alifika Abu Dhabi mji mkuu wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ambapo alifanya mazungumzo mtawala wa Abu Dhabi Mohammad bin Zayed.
Habari ID: 3474872 Tarehe ya kuchapishwa : 2022/01/31
TEHRAN (IQNA)-Msomi maarufu wa Misri Sheikh Salah Abdul Fattah al Khaledi, msomi mwandamizi wa Palestina katika uga wa sayansi za Qurani na tafsiri amefariki dunia.
Habari ID: 3474866 Tarehe ya kuchapishwa : 2022/01/29
TEHRAN (IQNA)- Askari 100 wa utawala wa Kizayuni wa Israel wameuvamia na kuuvunjia heshima Msikiti wa Nabii Ibrahim AS katika mji wa Al Khalil (Hebron) katika eneo la Palestina ambalo unalikalia kwa mabavu la Ukingo wa Magharibi.
Habari ID: 3474847 Tarehe ya kuchapishwa : 2022/01/24
TEHRAN (IQNA)- Mchezaji maarufu wa tennis kutoka Kuwait amepongezwa kwa hatua yake ya kujiondoa katika shindano moja la kimataifa baada ya kubainika kuwa alitakuwa ashindane na raia wa utawala haramu wa Israel.
Habari ID: 3474836 Tarehe ya kuchapishwa : 2022/01/22
TEHRAN (IQNA)- Sheikh Ahmad El Tayyib, Sheikh Mkuu wa Kituo cha Kiislamu cha Al Azhar nchini Misri amefanya mazungumzo ya simu na Mfalme Abdallah wa Pili wa Jordan.
Habari ID: 3474829 Tarehe ya kuchapishwa : 2022/01/20
TEHRAN (IQNA)- Mashirika ya usalama ya harakati za kupigania ukombozi wa Palestina katika Ukanda wa Gaza yamefanikiwa kumnasa mmoja wa wahusika wa mauaji ya kigaidi ya msomi na mwanasayansi wa Ki palestina aliyeuliwa huko Malaysia.
Habari ID: 3474795 Tarehe ya kuchapishwa : 2022/01/11
TEHRAN (IQNA) - Makumi ya walowezi wa Kizayuni wameuvamia tena msikiti wa al-Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) ambapo wameuvunjia heshima msikiti huo ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu.
Habari ID: 3474794 Tarehe ya kuchapishwa : 2022/01/11
TEHRAN (IQNA)- Spika wa Bunge la Kuwait amesema nchi hiyo itaendelea kuunga mkono taifa la Palestina katika kutetea haki zake.
Habari ID: 3474786 Tarehe ya kuchapishwa : 2022/01/09
TEHRAN (IQNA)- Utawala wa Kizayuni wa Israel umebomoa kituo cha afya na majengo mengine kadhaa katika mji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na utawala huo.
Habari ID: 3474766 Tarehe ya kuchapishwa : 2022/01/04
TEHRAN (IQNA)-Wa palestina wa Ukanda wa Ghaza wamepamba mitaa yao kwa mabango makubwa ya Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani.
Habari ID: 3474755 Tarehe ya kuchapishwa : 2022/01/02
TEHRAN (IQNA)- Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel waliwaua raia Wa palestina wasiopungua 357 mwaka 2021 huku jamii ya kimataifa ikiwa kimya kuhusu jinai hizo dhidi ya raia.
Habari ID: 3474754 Tarehe ya kuchapishwa : 2022/01/02
TEHRAN (IQNA)- Utawala wa Kizayuni wa Israel unaendeleza njama zake haramu za Kuuyahudisha Msikiti wa Al Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na utawala huo ghasibu.
Habari ID: 3474749 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/12/31
TEHRAN (IQNA)- Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amekosolewa vikali kwa kukutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Vita wa utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3474739 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/12/29
TEHRAN (IQNA)- Waliotenda jina katika Vita vya Furqan (vita vya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Ghaza mwaka 2008-2009) hawataruhusiwa kukwepa mkono wa sheria, imesisitiza Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas).
Habari ID: 3474731 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/12/27
TEHRAN (IQNA)- Wananchi wa Morocco wameandamana katika miji mbalimbali ya nchi hiyo na kutangaza tena kupinga nchi yao kuwa na uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel unaotenda jinai kila leo dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina.
Habari ID: 3474716 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/12/24
TEHRAN (IQNA)- Askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamewakamata watoto watatu waliokuwa wanapeperusha bendera ya Palestina katika Msikiti wa Al Aqsa mjini Quds(Jerusalem) Mashariki unaokaliwa kwa mabavu na utawala huo.
Habari ID: 3474703 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/12/21
TEHRAN (IQNA)- Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, Iran itaendelea kuwaunga mkono wananchi wa Palestina hadi pale mji mtakatifu wa Quds utakapombolewa na kuondoka katika makucha ya Wazayuni maghasibu.
Habari ID: 3474697 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/12/20
TEHRAN (IQNA)- Timu ya Taifa ya kandanda ya Algeria imeibuka mshindi katika mashindano ya kwanza ya Kombe la Mataifa ya Waarabu (FIFA Arab Cup 2021) yaliyofanyika nchini Qatar na kuwatunuku Wa palestina kombe hilo.
Habari ID: 3474695 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/12/19