iqna

IQNA

TEHRAN (IQNA)- Mashirika na makundi 250 ya kutetea haki za binadamu yametoa wito wa kuchukuliwa hatua za kisheria utawala haramu wa Israel kwa jinai uliyotenda ya kumuua mwandishi habari wa Televisheni ya al-Jazeera Shireen Abu Aqleh.
Habari ID: 3475245    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/05/13

Kiongozi Muadhamu katika mkutano na Amir wa Qatar
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema dhulma ya miongo kadhaa ya utawala khabithi wa Kizayuni dhidi ya watu wa Palestina ni ukweli mchungu wa historia na pigo kwa ulimwengu wa Kiislamu na Kiarabu na kuongeza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inataraji kwamba ulimwengu wa Kiarabu utaingia wazi wazi katika medani ya kisiasa kukabiliana na jinai hizo.
Habari ID: 3475243    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/05/13

TEHRAN (IQNA)-Mapema jana Jumatano, mwandishi wa habari ya televisheni ya al Jazeera, Shireen Abu Akleh, 51, alipigwa risasi na kuuliwa shahidi kikatili na wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wakati akiwa kwenye kazi yake ya kuripoti uvamizi wa kijeshi wa jeshi la Israel katika kambi ya wakimbizi wa Palestina ya Jenin.
Habari ID: 3475240    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/05/12

TEHRAN (IQNA)- Askari wa jeshi katili lla utawala wa Kizayuni wa Israel wamemuua kigaidi mwandishi mashuhuri na nguli wa televisheni ya al Jazeera, Shirin Abu Akleh alipokuwa katikati ya kazi zake kwenye kambi ya Jenin.
Habari ID: 3475234    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/05/11

TEHRAN (IQNA)- Waislamu nchini Russia wametangaza uungaji mkono jitihada za ukombozi wa taifa linalodhulumiwa la Palestina ambalo linakoloniwa na utawala haramu wa Israel.
Habari ID: 3475220    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/05/07

TEHRAN (IQNA)-Utawala wa Kizayuni wa Israel umezindua mpango haramu wa kujenga nyumba mpya zipatazo elfu nne katika eneo la Ukingo wa Magharibi, Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
Habari ID: 3475219    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/05/07

TEHRAN (IQNA)-Wazayuni wasiopungua watatu wameangamizwa katika oparesheni za ulipizaji kisasi za Wa palestina waliojitolea kufa shahidi.
Habari ID: 3475213    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/05/06

Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran amesema, utawala wa Kizayuni wa Israel umezingirwa na wanamapambano wa Kiislamu walioko Palestina, Lebanon, Iraq na Yemen.
Habari ID: 3475212    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/05/06

TEHRAN (IQNA)- Walowezi wa Kizayuni wameushambulia Msikiti wa Al Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) kwa mnasaba wa utawala haramu wa Israel kukalia kwa mabavu ardhi za Palestina.
Habari ID: 3475209    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/05/05

Katika mazungumzo na Rais wa Uturuki
TEHRAN (IQNA)- Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameyataja matukio ya karibuni katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina kuwa yasiyokubalika na kueleza kuwa: Kuna ulazima wa kufanyika juhudi za kusitisha mashambulizi ya kinyama ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wananchi wa Palestina kupitia msaada wa nchi za Kiislamu na jitihada za kimataifa.
Habari ID: 3475202    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/05/03

Hotuba ya Sala ya Idul Fitr Tehran
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Sala ya Idul Fitr mjini Tehran amesema katika hotuba zake kwenye Swala ya Eidul-Fitri leo hapa mjini Tehran kwamba, maandamano ya Sikuu ya Kimataifa ya Quds yameonyesha kuwa, malengo matukufu ya taifa madhulumu la Palestina yangali hai.
Habari ID: 3475200    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/05/03

TEHRAN (IQNA) - Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema uchaguzi uliopangwa kufanyika nchini humo hautaizuia harakati hiyo kujibu shambulio lolote la utawala bandia wa Israel, akisisitiza kuwa Hizbullah itajibu papo hapo shambulio lolote la utawala huo haramu.
Habari ID: 3475187    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/04/30

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei amesema, Palestina nzima imekuwa uwanja wa mapambano, na kwamba mipango yote ya suluhu na kufanya mapatano na adui Mzayuni imebatilishwa.
Habari ID: 3475185    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/04/29

TEHRAN (IQNA)- Rais Ebrahim Raeisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameupongeza mhimili wa muqawama au mapambano ya Kiislamu kwa kuuzuia utawala wa Kizayuni kutekeleza uharibifu zaidi katika eneo kama walivyofanya magaidi wakufurishaji.
Habari ID: 3475183    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/04/29

Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu
TEHRAN (IQNA)- Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu imetangaza kuwa njia ya kuuangamiza utawala wa Kizayuni ni kuimarisha safu ya Jihadi na mapambano mataifa sambamba na nchi za Kiislamu kutangaza uungaji mkono wao wa pande zote kwa wananchi waliodhulumika wa Palestina.
Habari ID: 3475182    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/04/29

TEHRAN (IQNA)- Mkuu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Siku ya Kimataifa ya Quds ni nembo ya muqawama au mapambano katika Umma wa Kiislamu.
Habari ID: 3475180    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/04/28

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Amir- Abdollahian
TEHRAN (IQNA)- Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Utawala bandia wa Israel ni mkiukaji mkubwa wa haki za binadamu duniani huku akisisitiza kuwa kura ya maoni ni njia muafaka ya kuainisha mustakabali wa Palestina.
Habari ID: 3475179    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/04/28

TEHRAN (IQNA)- Balozi wa mwakilishi wa kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, kuna wajibu wa sheria za kimataifa kuulinda Msikiti wa al Aqsa ili kuzuia kutokea maafa yenye madhara makubwa.
Habari ID: 3475175    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/04/27

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, maadhimisho ya Siku ya Quds ni fursa ya kutangaza kuwa pamoja na wananchi madhulumu wa Palestina ambapo licha ya taifa hilo kudhulumiwa lakini limepata nguvu na kuwa imara.
Habari ID: 3475173    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/04/27

TEHRAN (IQNA) - Katika kampeni iliyoitwa 'Hands Off Al-Aqsa Mosque' (Achaneni na Msikiti wa Al Aqsa), Baraza la Ushauri la Malaysia la Mashirika ya Kiislamu (Mapim) na mashirika 43 yasiyo ya kiserikali (NGOs) yameonyesha mshikamano wao na Wa palestina .
Habari ID: 3475163    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/04/24