iqna

IQNA

TEHRAN (IQNA)- Mufti Mkuu wa Misri ametadharisha juu ya njama ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya kuuyahudisha mji mtukufu wa Quds unaokaliwa kwa mabavu, na kufuta kabisa utambulisho wake halisi.
Habari ID: 3473687    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/02/27

TEHRAN (IQNA)- Umoja wa Mataifa umeutaka utawala wa Kizayuni wa Israel usitishe hatua zake zilizoratibiwa na kubomoa nyumba za Wa palestina .
Habari ID: 3473686    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/02/26

TEHRAN (IQNA)- Maeneo yote ya Msikiti wa Al Aqsa mjini Al Quds (Jerusalem) yatakuwa wazi kwa waumini Waislamu kwa ajili ya ibada katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Habari ID: 3473681    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/02/25

TEHRAN (IQNA) – Kadhia ya Sudan kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel inapaswa kujadiliwa upya baada ya mabadiliko katika baraza la mawaziri, amesema mwanachama wa Baraza la Serikali ya Mpito.
Habari ID: 3473665    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/02/19

TEHRAN (IQNA) Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, imelaani kitendo cha utawala haramu wa Israel kuzuia dozi 2,000 za chanjo ya Corona kuwafikia wafanyakazi wa sekta ya afya katika Ukanda wa Ghaza.
Habari ID: 3473654    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/02/16

TEHRAN (IQNA) - Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ametoa mkono wa pongezi na kheri kwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na wananchi wa Iran kwa mnasaba wa maadhimisho ya mwaka wa 42 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.
Habari ID: 3473641    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/02/11

TEHRAN (IQNA) – Uamuzi wa hivi karibuni wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) wa kuchunguza jinai za Israel dhidi ya Wa palestina umeungwa mkono na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) na chuo cha Kiislamu cha Al-Azhar nchini Misri.
Habari ID: 3473631    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/02/08

TEHRAN (IQNA)- Kumekuwa na hisia mseto baada ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC kutoa hukumu kwa manufaa ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni.
Habari ID: 3473626    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/02/06

TEHRAN (IQNA) – Askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamewashambulia Wa palestina waliokuwa wakiandamana katika kijiji cha Beit Dajan katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kupinga ujenzi wa vitongoji haramu vya walowezi wa Kizayuni.
Habari ID: 3473625    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/02/06

TEHRAN (IQNA)- Maulamaa na Maimamu wa Swala za Jamaa wasiopungua 200 nchini Mauritania wametoa Fatuwa inayorahamisha kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawaa dhalimu wa Israel.
Habari ID: 3473612    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/02/01

TEHRAN (IQNA) - Sheikh Mohammad Hussein, Mufti Mkuu wa Quds (Jerusalem) ameulaani vikali utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kuzuia ukarabati wa Msikiti wa Al Aqsa.
Habari ID: 3473597    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/01/28

TEHRAN (IQNA)- Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamebomoa msikiti na majengo kadhaa ya Wa palestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
Habari ID: 3473596    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/01/27

TEHRAN (IQNA) – Wa palestina wameandaman katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kupinga hatua ya utawala haramu wa Israel kuendelea kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni.
Habari ID: 3473585    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/01/23

TEHRAN (IQNA)- Mjumbe wa Harakati ya Jihad Islami ya Palestina nchini Iran Nasser Abu Shariff ametembelea ofisi za Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA) hapa mjini Tehran.
Habari ID: 3473579    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/01/21

TEHRAN (IQNA)- Gazeti moja la Kiebrania limeripoti kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel umetoa sharti kwa Uturuki la kuifunga ofisi ya HAMAS mjini Istanbul ili kuanzisha tena uhusiano kamili na nchi hiyo.
Habari ID: 3473570    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/01/19

TEHRAN (IQNA) - Harakati za kupigania ukombozi wa Palestina za Fat'h na Hamas zimeunga mkono tangazo la Mamlaka ya Ndani ya Palestina kuhusu kufanyika uchaguzi wa bunge la rais baadaye mwaka huu.
Habari ID: 3473561    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/01/16

TEHRAN (IQNA)- Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wamesema utawala wa Israel, kama utawala vamizi unaokali ardhi za Palestina kwa mabavu, unapaswa kuwapa Wa palestina chanjo ya corona.
Habari ID: 3473559    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/01/15

TEHRAN (IQNA) - Mwakilishi wa harakati ya Jihadul Islami ya kupigania ukombozi wa Palestina nchini amepongeza nafasi ya Luteni Jenerali Shahidi Qassem Soleimani katika kuwaunganisha Wa palestina .
Habari ID: 3473552    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/01/13

TEHRAN (IQNA) - Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imetahadharisha kuhusu mpango wa utawala wa Kizayuni wa Israel wa kubomoa sehemu za Msikiti wa Al Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem).
Habari ID: 3473547    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/01/11

TEHRAN (IQNA)- Utawala wa Kizayuni wa Israel umeongeza maradufu kasi ya kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi ulizowapora Wa palestina hatua ambayo itaibua msuguano na serikali mpya ijayo ya Marekani.
Habari ID: 3473545    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/01/11