IQNA

Sheikh Mkuu wa Al Azhar atangaza kufungamana na Wapalestina

15:12 - May 09, 2021
Habari ID: 3473892
TEHRAN (IQNA)- Sheikh mkuu wa Kituo cha Kiislamu cha Al Azhar nchini Misri ametoa taarifa na kulaani ‘ugaidi wa Kizayuni’ baada ya wanajeshi wa utawala haramu wa Israel kuwahujumu Wapalestina katika Msikiti wa Al Aqsa mjini Quds.

Katika taarifa kupitia ukurasa wake rasmi wa Facebook,, Sheikh Ahmed El-Tayyeb amelaani vikali hujuma hiyo ya Ijumaa ya utawala haramu wa Israel dhidi ya Wapalestina.

“Kuuhujumu Msikiti wa Al Aqsa ni ukiukwaji wa utukufu wa Sala,” amesema huku pia akilaani uvamizi uliotekelzwa na askari wa Israel dhidi ya wakaazi wa mtaa wa Sheikh Jarrah mjini Quds ambao walikuwa wamekusanyika kulaani amri ya mahakama ya Israel ya kutafa familia kadhaa za Palestina ziondoke katika nyuma zao za jadi eneo hilo.

El Tayeb amesema inaaibisha kuona kuwa jamii ya kimataifa inayamazia jinai hizo za Israel. Amesema Al Azhar inatangaza mfungamano wake na Wapalestina  wakati wote.

Ijumaa ya mwisho ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambayo pia ilikuwa Siku ya Kimataifa ya Quds ilishuhudia hujuma mpya askari wa utawala haramu wa Israel dhidi ya Msikiti Mtakatifu wa Al Aqsa mjini Quds.

3474653

Kishikizo: al azhar ، siku ya quds ، palestina ، israel ، al aqsa
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* :